Nataka kusafiri kutoka Mwanza kwenda Morogoro kwa pikipiki sanlg 125, naomba ushauri kitaalam

Ushaur wangu beba oil lita 2 kwenye beg;chukua kidumu cha lita 1 kwa ajili ya emergence,usisahau kuvaa makoti makubwa ya kuzuia upepo pamoja na buti,chukua mwamvuli njian hakutabiriki last hakikisha unapumzisha pikipiki atleast kwa kila km 300 pamoja na kuzingatia sheria za barabaran hususani site mirror
Asante mkuu
 
Jamaa kaomba ushauri wa namna ya kufika Moro kwa kutumia pikipiki yake.
Hajaomba ushauri wa kujua pikipiki yake ni Mchina/feki au ni ya Japan/Germany wala Italy.
Tujifunze kujikita kwenye mada husika,la sivyo JF itakuwa kama badoo/Facebook.
Asante mkuu kwa kunisaidia
 
MKuu pikipiki yako inafika ila shida haina vifaa vinavyoisaport kufika,
Mfano unaweza kupasua tairi kama mara mbili hadi ufike, kwa tairi hizo kwa umbali wa km 300-400 kwenye lami tairi haitakuwa yenyewe,
Pia Mnyororo utazingua sana means unaweza katika hata mara tatu kama utakuwa unaunga huohuo

Pia Hiyo pikipiki ina vibration kubwa ambazo zinazidi uwezo wa spring sio nzuri kwa masafa marefu

Pia injini yake inachemka sana mkuu unaweza jikuta ikabust hata ukiwa na mapumziko must upumzishe chombo kwa takribani saa moja na nusu kabla ya safari kuanza tena

Pia sina uhakika mavazi utakayotumia kama yako sahihi sio mambo ya kukariri kuvaa sijui majaketi mazito sijui nini noo
Kuna helment nzuri sana zinazotumika kwa masafa marefu na hazitoki na hiyo pikipiki yako unanunua tu pembeni uziri wa hii helment nikwamba ni imara sana pia inakuwekea mfumo mzuri wa kupumua haikutengenezei joto kama zilizyo zingine

la hatari sina uhakika na uzoefu wa safari ndefu kwa pikpik unahitaji uzoefu kwa usalama wako
bila kupepesa macho unaweza kujikuta unalala hapo hapo juu ya chombo na bado kinatembea na ukija kuamka unajikuta upo ahera

Ushauri DONT TRY THIS MKUU
Unafamilia na Ndugu wanakutegemea na Bado Wanakuhitaji Sana
Pia Sisis Wana JF bado tunakupenda Mno
 
Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu

MKUU MTAFUTE PASCAL MAYALLA yeye atakupa uzoefu
 
Inawezekana inabidi safari uanze alfajiri sana. Kuna jamaa anatoka Mbeya mpaka Tunduru na Fekon karibu kila mwezi.

Kama utatembea mchana itabidi upumzike angalau baada ya Kilometa 200 au 300.

Pikipiki inahitaji umakini sana kwenye safari ndefu ukichoka usisite kupumzika, ubaya wa pikipiki ukizubaa sekunde lazima ikutoe nje ya njia.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Professional driver wa pikipiki wengi ni vijana wa Arusha hiyo safari ya Mwanza-Moro kwa hizo pikipiki za kichina watu wanazo dharau anaenda vizuri tena kwa muda sahihi.

Wanaziita Toyo ukikutana nao wako na hizo Sanlg,Kinglion, Fekon na Huoniao hata za 125cc na anatembea umbali wa Dar-Arusha.
 
Wanaforce sana mkuu hiyo sio salama kabisa
Huyo kwanza anajiua mwenyewe hata sipopata ajali still anajiwekea harmful effect kwa maisha yake mwenyewe
Nimesafiri sana kwa pikipiki mbeya-iringa-morogoro nilikuwa natumia Triumph Tiger ina cc 1250 ina cylinder 3, japo ilikuwa ya kampuni lakini ni moja ya usafiri nikiambiwa basi na hiyo natumia pikipiki
Ina mambo mengi ya usalama, natoka kule kyela matema hadi moro stand ya kwanza kunywa chai tu then mafuta naendelea mbele
kwa hutu tupikipiki twa mchina sio safe nilizunguka ile rungwe kwa san lg nilijuta kwakweli nikama km400 per day nilizozunguka
Nilipigwa na homa kabisa
shida moja kubwa ni kwamba high vibration hiii ni shida sana huwezi jua madhara yake ila wanaojua wanaelewa hatari yake ilivyo
 
mkuu siku ukiamka asubuhi mapemaaa nenda tu nyegezi ukifika toa mafuta yote kata tiketi yako 45k kwa moro inaeza pungua na ya pikipiki haiwezi zidi hata 20k inawekwa kwenye buti we unazama zako ndani moro saa 3 usiku umefika na roho yako na pikipiki yako mkuu kama shida yako ni kufika bora ufike salama kama kuna lingine unalotaka nikutakie kila lakheri.
 
mahitaji ya dharura;
1. oil
2. petrol
3. tairi la akiba
4. pump ya mkono
5. vifaa vya kuziba pancha
6. spana
7. maji ya kunywa
8. chakula kikavu
9. silaha/ kisu/ jambia/mawe
10. mavazi mazito na gloves
11. dawa za maumivu
12. uwe na m pesa kwa ajili ya vifurushi
13. mnyororo
14. line za simu mitandao yote, kuna maeneo mitandao flani haishiki.

zingatia hayo
Eeeeeh hahhaha na mawe
 
MKuu pikipiki yako inafika ila shida haina vifaa vinavyoisaport kufika,
Mfano unaweza kupasua tairi kama mara mbili hadi ufike, kwa tairi hizo kwa umbali wa km 300-400 kwenye lami tairi haitakuwa yenyewe,
Pia Mnyororo utazingua sana means unaweza katika hata mara tatu kama utakuwa unaunga huohuo

Pia Hiyo pikipiki ina vibration kubwa ambazo zinazidi uwezo wa spring sio nzuri kwa masafa marefu

Pia injini yake inachemka sana mkuu unaweza jikuta ikabust hata ukiwa na mapumziko must upumzishe chombo kwa takribani saa moja na nusu kabla ya safari kuanza tena

Pia sina uhakika mavazi utakayotumia kama yako sahihi sio mambo ya kukariri kuvaa sijui majaketi mazito sijui nini noo
Kuna helment nzuri sana zinazotumika kwa masafa marefu na hazitoki na hiyo pikipiki yako unanunua tu pembeni uziri wa hii helment nikwamba ni imara sana pia inakuwekea mfumo mzuri wa kupumua haikutengenezei joto kama zilizyo zingine

la hatari sina uhakika na uzoefu wa safari ndefu kwa pikpik unahitaji uzoefu kwa usalama wako
bila kupepesa macho unaweza kujikuta unalala hapo hapo juu ya chombo na bado kinatembea na ukija kuamka unajikuta upo ahera

Ushauri DONT TRY THIS MKUU
Unafamilia na Ndugu wanakutegemea na Bado Wanakuhitaji Sana
Pia Sisis Wana JF bado tunakupenda Mno
Mnoo
 
Back
Top Bottom