Nataka kusafiri kutoka Mwanza kwenda Morogoro kwa pikipiki sanlg 125, naomba ushauri kitaalam

ndagalukwetu

Member
Nov 30, 2018
14
9
Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu
 
kuna jamaa yangu alishawahi kutoka nanganga masasi hadi Dar kwa sanlg ila yake ni 150cc.kazi kwako!
 
Ushaur wangu beba oil lita 2 kwenye beg;chukua kidumu cha lita 1 kwa ajili ya emergence,usisahau kuvaa makoti makubwa ya kuzuia upepo pamoja na buti,chukua mwamvuli njian hakutabiriki last hakikisha unapumzisha pikipiki atleast kwa kila km 300 pamoja na kuzingatia sheria za barabaran hususani site mirror
 
Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu
ingekuwa pikpik ya timing chain kama boxer TVS hlx au SINORAY ungefika mapema kuliko bus...kuna jamaa yangu katoka dar juzi saa mbili asubuhi kumekucha na SINORAY ya timing chain kafika NJOMBE saa tisa alasiri umba ni km 700 alitumia takriban masaa 7...timing chain haitetemeshi wala hauchoki unakuwa na mwendo wako wastani kama 100kph unafika mapema kabisa
...ila hiyo sun lg utajuta utaomba kupakia njiani kwenye maroli maana full vibration hata manyoni hufiki utakuwa ushapigwa ganzi
 
Jamaa kaomba ushauri wa namna ya kufika Moro kwa kutumia pikipiki yake.
Hajaomba ushauri wa kujua pikipiki yake ni Mchina/feki au ni ya Japan/Germany wala Italy.
Tujifunze kujikita kwenye mada husika,la sivyo JF itakuwa kama badoo/Facebook.
Okay, Tujifunze kuvumilia na kuthamini mawazo ya wengine Pia. Kumjulisha ubora wa chombo anachotaka kutumia, ni kumsaidia pia namna anavyoweza kuwa salama katika safari yake.
Habari za Feki umezileta wewe. So Tujikite kwenye hoja.
 
mahitaji ya dharura;
1. oil
2. petrol
3. tairi la akiba
4. pump ya mkono
5. vifaa vya kuziba pancha
6. spana
7. maji ya kunywa
8. chakula kikavu
9. silaha/ kisu/ jambia/mawe/mkuki/upinde
10. mavazi mazito na gloves
11. dawa za maumivu
12. uwe na m pesa kwa ajili ya vifurushi
13. mnyororo
14. line za simu mitandao yote, kuna maeneo mitandao flani haishiki.

zingatia hayo kwani safari yako ni ndefu na hatarishi lolote laweza kutokea
 
ingekuwa pikpik ya timing chain kama boxer TVS hlx au SINORAY ungefika mapema kuliko bus...kuna jamaa yangu katoka dar juzi saa mbili asubuhi kumekucha na SINORAY ya timing chain kafika NJOMBE saa tisa alasiri umba ni km 700 alitumia takriban masaa 7...timing chain haitetemeshi wala hauchoki unakuwa na mwendo wako wastani kama 100kph unafika mapema kabisa
...ila hiyo sun lg utajuta utaomba kupakia njiani kwenye maroli maana full vibration hata manyoni hufiki utakuwa ushapigwa ganzi
nimejifunza kitu.
muda mrefu nimetamani kujua why baadhi za pikipiki zina vibrate sana na zingine zimetulia. asante mkuu
 
Back
Top Bottom