Nataka kusafiri kutoka Mwanza kwenda Morogoro kwa pikipiki sanlg 125, naomba ushauri kitaalam

Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu
Utafka bila shda yoyote ukitoka mwanza pumzika kahama baada ya kutoka kahama kapumzike manyoni singida baada ya hapo dodoma mpaka Moro chakuzingatia speed na kukaa katikt ya barabara kaa pembeni
 
Utafka bila shda yoyote ukitoka mwanza pumzika kahama baada ya kutoka kahama kapumzike manyoni singida baada ya hapo dodoma mpaka Moro chakuzingatia speed na kukaa katikt ya barabara kaa pembeni

Kahama tena mkuu!

Mwanza anakuja Shy, Tinde, Nzega.

Kahama iko pembeni sana.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu
Badili tu oil petrol ya kutosha anza safari ila pikipiki ya mchina ina vibresheni sana ukitembea sana, kama kuna uwezekano pumb. acha nyumbani.
 
mahitaji ya dharura;
1. oil
2. petrol
3. tairi la akiba
4. pump ya mkono
5. vifaa vya kuziba pancha
6. spana
7. maji ya kunywa
8. chakula kikavu
9. silaha/ kisu/ jambia/mawe/mkuki/upinde
10. mavazi mazito na gloves
11. dawa za maumivu
12. uwe na m pesa kwa ajili ya vifurushi
13. mnyororo
14. line za simu mitandao yote, kuna maeneo mitandao flani haishiki.

zingatia hayo
Point
 
ingekuwa pikpik ya timing chain kama boxer TVS hlx au SINORAY ungefika mapema kuliko bus...kuna jamaa yangu katoka dar juzi saa mbili asubuhi kumekucha na SINORAY ya timing chain kafika NJOMBE saa tisa alasiri umba ni km 700 alitumia takriban masaa 7...timing chain haitetemeshi wala hauchoki unakuwa na mwendo wako wastani kama 100kph unafika mapema kabisa
...ila hiyo sun lg utajuta utaomba kupakia njiani kwenye maroli maana full vibration hata manyoni hufiki utakuwa ushapigwa ganzi

hizo ambazo hazina timing chain zinatumia mechanism gani kufungua milango ya mafuta na exaust
 
hizo ambazo hazina timing chain zinatumia mechanism gani kufungua milango ya mafuta na exaust
kuna kitu wanaita push load..sifahamu sana ila ndo hivo kuna pushload na timing chain
kama hizi san lg ni pushlod ndo maana full vibration
 
NAOMBA KUJUA NDUGU ZANGU. HIVI PIKI PIKI MFANO BOXER, YAMAHA, TVS, HONDA ZINAWEZA PIGA RUTI NDEFU MFANO DAR-MOSHI, NA MASAA MANGAPI INAWEZA TUMIA!??!....

NOTE:
naomba majibu halisia tafadhali.......

ASANTENI....
 
Hata mbinguni zinaenda muhimu kuwepo na barabara,na kote ulikokutaja zinafika kwa masaa matatu.
 
We jamaa muoga kweli yaan pikipiki mpaka uombe ushaur
Kuna jamaa anaitwa sukago yeye kila weekend anasafair kwa baiskel ha Anita Kutoka swanga mpaka mikumi pale
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Wakuu habari,nauliza ili nipewe mwanga hapa,naitaji kusafiri kutoka mwanza kwenda morogoro kwa pikipiki sanlg 125 cc,je wataalamu wanisaidie hapa nifanyeje ili nifike vzr na hii pikipiki? Ni mpya ina miezi miwili,

Naombeni mchanganuo nifanye lipi na lipi ili niweze kufika kwa usafiri huu
Utatumia siku mbili but iwe mpya au nzima umwage oil Mara tatu na usiivute Sana tembea mwendo wa kawaida( me nilitoka na fecon kutoka moro kwenda sumbawanga kwa two days)
 
Back
Top Bottom