Soon wakati naanza job nilipewa corolla 111 na B mkubwa inisaidie movement za mjini,,, nikawa nalalamika gari haina swaga si unajua ujana nini nikakopa hela somewhere nikanunua GX 110 mbona nilikoma kuanzia mafuta, spares mpaka nikaikumbuka corolla yangu niliyoirudisha home kwa kejeli..
Mambo yalivyozidi unga nikaliuzilia mbali tena kwa bei ya hasara nikarudi home kinyonge kuifata corolla yangu ya zawadi,, ndo nasukuma nayo mpaka leo mwaka wa pili huu lakini kama mpya, nakaa mwenge nafanya kazi town budget ya mafuta 20,000 wiki nzima na sishushi kioo,, vifaa bei rahisi mbaya nikagundua kweli ukubwa dawa,,, na sina mpango wa kubadilisha kabisa maana sitaki stress.. Nimeshaapa sitanunua magari ya mbwembwe mpaka nakufa nawashangaa tu vijana wanavyokimbilia Verossa nowdays,,, nawacheka tu na corolla yangu haina stress za mafuta mda wote unakula A.C kitu lita moja una km almost 15 za ac,,
Ila raum 2004 ina shape nzuri na inatumia spare za corolla haina stress kabisa,,