Nataka kumuacha mke wangu


No way No....unamuacha make wako na wewe ndo ulimpeleka akajifungulie nyumbani kwa Mama yako?
Hii hapana....huo utovu wa nidhamu ni upi mbona unashindwa kuuweka wazi? kama kutoelewana kati ya mkeo na mama yako ni kawaida sana...Kiushauri usimwache labda kama ulisha muacha zamani na ulimpeleka kwa mama kutafuta justification that's sound Great....

kuhusu sheria subili mahakama ya kadhi......kadhi mkuu anahusika hapo......
 

wew mwache tu kwan unazaliwa nae? ila kabla hujamwacha njo chukua copy ya the law of marriage Act bureeee
 

Ilikua ni lazima akajifungulie kwenu? kwa nini asingebaki kwake akajifungulia hapo? Wakati mwingine watu muwe mnawaza,hivi nikikwambia wewe na mama yako mnamnyanyasa huyo dada utakataa? kwa nini usikilize upande mmoja,kaa na mama yako pamoja na mkeo muongee muone shida iko wapi,mama zenu huwa hawakosei,kutwa kusimanga wake zenu kisa mama mkwe.
 

Kimsingi, nafahamu kuwa sinta mtendea haki maana ni haki yake kupata malezi toka kwa wazazi wote wawili lkn mama kichanga ndo msababishaji, na nafikiri hii ndo adhabu inayo mfaa ukilinganisha na jitihada nyingi nilizozifanya kumrekebisha kabla ya hili ambazo hazikuzaa matunda.
 
Ivi kweli unafikiria kiume? Kwani huyo mkeo hana kwao mpaka umpeleke kwa mzazi wako? Huyo Ni mkwewe mzazi anataka kukandwaa kutizamwa kwanini wasifanye hayo mambo watu wa kwao? Au ubahili? Bora umuwache hustahili kua na mke..

Hilo swala la kumpeleka kwetu nimeshalijibu kwenye page za nyuma kidogo jaribu kuzirejea utapata mengi
 

mkuu nakubaliana na wewe kabisa....... think about the kid only......makosa ya mama haadhibiwi mtoto.....angalizo hawa wanawake akijua unampenda mwanao (watoto), huwa wanaona ni nafasi ingine ya kukuzingua.... fanya kwa umakini....
 
acha upimbi wewe .. mama yako hawezi kumtreat in good way hata siku moja sisi ndiyo wanawake bwana unafki mbele.. trust me mama yako ndiyo mwenye shida ndiyo maana now days tukijifungua bora kukaa na wazazi wetu kuliko mama mkwe ... KOMA HUNA HAYA WEWE MAMA YAKO NI MALAIKA MKEO KUKAA KIMYA UNADHANI NI MPUUZI AU ANAVUMILIA TU..
 

sasa nimejua...hii ni justification kumbe ulishamuacha zamani....
 
Bro usimwache mke eti kisa ameonesha tabia ya upotevu wa nidhamu, basi kama sisi tuliooa tungekuwa kama tungea kila wiki na kutimua, pls usimwche mkeo kaa nae vzr atabadilika

Nami alipoanza tabia ya domo chafu niliamini ipo siku atabadilika.....nikajaribu kuongea nae polepole na kumrekebisha bila mafanikio na sasa ameenda kuchafua ukweni (highest rank in the family) je niendelee kuvumilia akiidhalilisha familia yangu?
 
Mke uliowa mwenyewe,
Ukisikiliza ya kuambiwa utakuwa unaacha wake kila siku.

Mengine yanavumilika mengine yanafundishika;

Lisilovumilika ni kumfumania tu.
 

Mkiona vingine hataki kuweka bayana mumuelewe labda ana sababu zake msiazimishe.
Uzito wa kosa ameshaupima yeye, sio hadi akuambie na wewe ili uupime umsaidie kuamua.
 
Duuh..!hapo hamna husband material,kabla ya kufanya hvyo mulze na mkeo aliona mapungufu yep kwa ma mkwe!!
 
Hilo swala la kumpeleka kwetu nimeshalijibu kwenye page za nyuma kidogo jaribu kuzirejea utapata mengi

Kua muwazi hilo sio kosa la kumuwacha mkeo, tena umezaa nae na huyo mtoto umemfikiria?
 
kwanini hukubaki nawe wewe....?sio mantiki yoyote hapa eti kawakosea adabu kwenu, je umemuuliza tatizo nini...?

Kulingana na eneo nnalo ishi, kituo kinachotoa huduma za afya hakihudumii akina mama wanao jifungua mtoto wa kwanza na watano na kuendelea, hivyo ikalazimu kupelekwa sehemu nyingine ambako mm nilipendekeza kwao kwa mama yake ambako ni mkoani, kuna hospitali kubwa....wazazi wake walikataa kwa hoja ya mila haziruhusu, ndipo nili poamua kumpeleka nyumbani kwetu ambako pia ni mkoani.
 
Binafsi sikushauri umuache mkeo kwanza inakupasa uelewe kwamba mwanamke anapokuwa mjamzito siku zote haswa anapokuwa anakaribia kujifungua huwa wanakuwa na hasira sana hilo lak wanza ulielewe na hapo anapomjibu mbovu Mama yako jua sio akili yake zile ni hasira nakueleza hivi hata mimi binafsi nina mke na watoto wa 4 hii hali nishaizoea sasa nawewe kama mwanaume haswa inabidi changamoto hizi uzikabili sio kukurupuka kumtimua sasa kama ukimtimua unategemea Mtoto wako akija kukua atakupenda? Hatokuwa na mapenzi na wewe hata siku moja kwasababu hapo unakuwa unafanya kama kumtelekeza na mwisho wasiku ndo hao akijaga kukua anakuja kuwa mtu maarufu kama rais au msanii etc wakati huo umechoka hauna kitu utamtafuta nayeye atakupa makavu.
Ni jambo la kukaa na mkeo mkaya maliza huu ni wakati wake wa kudeka kwanza inapaswa uwe mdogo tu umdekeze maana hali aliyokuwa nayo sio ya marumbano unaweza ukamkosa mtoto pamoja na mama yake sikushauri umuache yule ni mkeo chaguo la roho yako na mmeapa kuwa mtashirikiana mpaka kufa kila mtu ana mapungufu yake so jitahidi kukaa nae chini kidogo kidogo atajirekebisha hizi ni changamoto kila mtu yalimkuta haya hata mimi binafsi yalinikuta na ni jambo dogo sana kurekebishika
 
Duuh..!hapo hamna husband material,kabla ya kufanya hvyo mulze na mkeo aliona mapungufu yep kwa ma mkwe!!

Nimekwisha muuliza na akajibu hajadhalilishwa kwa lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…