Nataka kujua kuhusu wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera

Majibu mazur yametolewa tayari labda summarize tu na chukua basi la Trinity ufike mapema
 
Umepata Maelezo mazuri saana. mji wa Ngara ni Mdogo saana uko mlimani.

Kiwanja cha ndege kipo, ndege zinazokwenda huko ni ndege ndogo ukienda kwenye ofisi zao watakujuza gharama na ratiba zao MF AVIC

usafiri wa Bus ,ni kama ulivyoelekezwa kwenda Bukoba itakuwa unazunguka bila sababu.panda mabus mpaka Kahama pale kuna usafiri wa kutosha kuelekea Ngara.

Au panda mabus yanayokwenda Rwanda utashuka kwenye kitongoji kinachoitwa KASULO (BENACO) huu ni mji kabla ya kuingia mpaka wa Rwanda ni eneo la Ngara tayari yawezekana hata ww ofisi yako ikakuelekeza uhudumu hapo.

Kutoka hapo kuelekea Ngara mjini ,usafiri wake ni magari madogo ( mchomoko) ni mwendo wa takribani 20/30 min , huku ukipita vitongoji kadhaa kama 00 (zerozero), Kumnazi, Kasharazi na K9 ( hapa madereva wengi wa magari makubwa ya mizigo kwenda Burundi wanapajua)nk

Hali ya hewa ni baridi ,chakula si tatizo wananchi wa kule ni waangaza mchanganyiko na makabila mengine.ukiwa Ngara mjini ni rahisi saana kwenda mpaka wa Burundi upande wetu tunapaita KABANGA upande wa Burundi wanapaita KOBELO.

Hali ya kiusalama ni ya kubadirika badirika kutokana na mapori yaliyoko matukio ya kutekwa magari, milio ya risasi si vya kushangaza saana.

Shule za viwango vyote zipo wala usiwaze na hata ule mpango wa wazazi kujipanga na kupeleka watoto shule za Bukoba mjini upo MF KAIZILEGE PRIMARY SCHOOL.

Nyumba zipo na bei ni ya kawaida kama Miji yote ilivyo.

Kuna radio station bora kabisa inaitwa RADIO KWIZERA inaburudisha haswa.

Mambo mengine yoooote yanayopatikana unakotoka na Ngara yapo.

Hospital kubwa kabisa inaitwa MURUGWANZA inaendeshwa na Kanisa kwa kushirikiana na serikali.
 
Kuongezea tu na Mimi haina haja ya kwenda Bukoba,panda gari ya Bujumbura shika Ngara (kama Taqwa bado zipo)
Nilikaa sehemu moja inaitwa Rulenge ,aisee hiyo sehemu ni nzuri kuliko 70% ya Tanzania hasa kama unap3nda kuishi mjini na kijijini na kwa wakati mmoja,pana maji ya uhakika ,kuna umeme,barabara ipo ya lami na barabara za mtaa ni full moramu inapitika mwaka mzima.Kuna shule ,kuna hospitali nzuri na kubwa na kabisa lina kama zaidi ya miaka 50, mkuu hadi kuna library.
 
Mzee
Umemuelezea vizuri sana. Yaani kama nakuona vile.
Umesema Kweli tupu, maana mkoa wa Kagera, Burundi na Rwanda kwa kiasi kikubwa ndiko mishe zangu nafanyia.

Umenifurahisha uliposema Wanyarwanda. Sipendi kuoa huku ila wazuri kwa kuwagegeda mno.
Ntapenda tuwasiliane mkuu tutete Nina kitu nataka kukuuliza.
 
Kuongezea tu na Mimi haina haja ya kwenda Bukoba,panda gari ya Bujumbura shika Ngara (kama Taqwa bado zipo)
Nilikaa sehemu moja inaitwa Rulenge ,aisee hiyo sehemu ni nzuri kuliko 70% ya Tanzania hasa kama unap3nda kuishi mjini na kijijini na kwa wakati mmoja,pana maji ya uhakika ,kuna umeme,barabara ipo ya lami na barabara za mtaa ni full moramu inapitika mwaka mzima.Kuna shule ,kuna hospitali nzuri na kubwa na kabisa lina kama zaidi ya miaka 50, mkuu hadi kuna library.
Mheshimiwa weye waishi rulenge?
 
ILA kuna uwezokano watu wakakushangaa unatoka eneo gani la nchi kwa kuwa unaongea kiswahili lafudhi tofauti na wenyeji,usishangae wakakuambia eneo la nchi unakotoka.Kingine hakikisha una nyaraka za kukutambulisha kuwa wewe ni mtanzania,maana kule ni eneo la mipaka na nchi jirani,maafisa ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji wapo macho.
 
Njema Sana aisee huko nako ni Ngara maana mi naenda halmashauri kuna ukaribu kama nafanya kazi hapo na garama za vyumba au nyumba inakuwaje.
 
ILA kuna uwezokano watu wakakushangaa unatoka eneo gani la nchi kwa kuwa unaongea kiswahili lafudhi tofauti na wenyeji,usishangae wakakuambia eneo la nchi unakotoka.Kingine hakikisha una nyaraka za kukutambulisha kuwa wewe ni mtanzania,maana kule ni eneo la mipaka na nchi jirani,maafisa ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji wapo macho.
Doh mambo ya uraia tena nayo yapo
 
Back
Top Bottom