Nataka kujilipua kuoa

Nataka kujilipua kuoa

Mkuu bora ujipange hadi walau 30-33 ili ujitosheleze kwanza.

Siyo unaoa then unaanza kuishi maisha ya kubangaiza.....Kwa sasa nakushauri utafute pesa kwanza ndoa baadae.

Miaka 30 au 33 unataka agundue nini uko ni phd ya ndoa anachukua ama ni nini iyo..........

Acha mtu aoe maana ilo ni jambo la kheri wee unataka muda wote awe anazini kwa Mungu kesho atajibu nini............?

Aoe ilhali anakipato chake mambo mengine yatakuja yenyewe maisha yenyewe mafupi haya miaka 20 au 30 unakufa kwanini usitumie fursa hii mapema............

Mkuu acha uwogo na maisha
 
Usimshauri mwenzako kuoa kwakufuata instincts zake,subiri apate ushauri wakutosha ili aamue vizuri,hicho kipato anachokipata kwasiku tu,bado kinatia shaka,usitake mwenzako afanye uamuzi wakuoa mwenyewe halafu matatizo aje atatue na watu wake wakaribu au ndugu zake.

Ulitaka matatizo atatue na nani sasa na magufuli au bashite.............?

Embu acha pigo zako wewe uwo ni uwoga wa maisha matatizo hayakimbiwi na matatizo ni sehemu ya maisha yetu uwezi kukimbia labda ufe

Acha jamaa aoe hakuna namna tatizo dunia inawashughulisha kuliko akhera yenu achelewe kuoa alafu awe anazini ndo unataka ivyo
 
Hao ng'ombe huruhusiwi kuwauza mkuu. Kukamua tu.

Elfu 10 ni kubwa. Familia nyingi zinaishi kwa 4000 kwa siku niamini. Atafute mwanamke wa kiwango chake aweke ndani budget watajibana humo humo ndani.

Au JF wote mambo safi nini? Mbona mimi elfu 10 per day pesa ndefu saana hahaha
Swali la msingi
"Hivi jf wote mambo safi nn???
Kwa kipato hicho sidhani kama hakitoshi ila inategemea na sehemu wanayoishi ,kuna sehemu nyingne hiyo elfu kumi kununua chakula cha Siku inatosha na kubaki kwa maisha ya mtanzania wa kawaida tu
Kusema et kipato cha tsh 30 kwa siku Ni pesa kubwa sana hata walioajiliwa na serikali sio wote wanaolipwa kiasi hicho cha mshahara lakin utakuta ameoa na ana familia yake anaishi tu vuzuri
 
Oa riski anatoa Mungu ni jambo la heri la kumpendeza yeye ..Ila kuwa makini na unaye taka kuoa aridhie kipato chako
 
Mapenzi ni hisia na kuoa ni uamuzi,hakuna kujipanga wala nini. Maisha ukisema ujipange utajikuta unafanikiwa at 45+ so we chukua jiko tu. Mi nilioa nikiwa na 24 yrs now familia imekua na tuna watoto, na kuhusu maisha ni namna ulivojipanga tu kwasababu hakuna atakeyesema sasa amefanikiwa na hatafuti tena.so oa na uendelee na Mishe zako,mengine yatajisumbukia yenyewe.

NB.kuoa sio kusogeza huduma ya ngono karibu,ni mchakato na hatua kubwa mno katika maisha ya binadamu. Hivyo basi oa ukiwa umejipanga na kujikamilisha kwa sehemu ya maisha yako binafsi,pia tafuta mke anekusaidia kimawazo na kiuchumi kwa kiasi fulani.

Karibu kwenye ulimwengu wa ndoa
 
Habari zenu mabibi na mabwana,

Ni kijana wenu mwema mwenye umri wa miaka 26.

Kipato changu ni elfu 8 hadi 10 tu kwa siku,
na nimepanga chumba kimoja.
Nimechakata data kichwani,
nikapata wazo la kujilipua kuoa.

Kabla sijaanza mchakato wa kudunduliza mahari,
Nimeona ni vema nije nipate mchango na hekima za wakongwe wa humu juu ya

1.FAIDA
&
2.HASARA
za kujilipua kwenye hiki kitengo.
Wewe oa,ridhki anapanga Mungu na umri wako unatosha kabisa kuwa na mke na kupambana kumtunza,,,kuna watu walijidai hawaoi wanajipanga kimaisha matokeo yake wamefikisha miaka 40 bado hawana maisha yoyote na wanajuta wangeoa hata mapema ili hata kama maisha wangeyakosa ila familia wangekua nayo Oa mapema uzae watoto wako uwalee ukiwa bado una nguvu.All in all muombe Mungu akupe mke mjengaji sio mke mchunaji.
 
Oa tu Mkuu, duniani hakuna na hakutakuwa na copy yako, ni wewe tu uko. Kushindwa kwa mtu wa aina yako kwenye hiyo idara ya ndoa kusikuumize akili maana yeye ni maisha yake. Kwa kipato chako kama mpaka baadae hautakuwa na njia mbadala ya kukiongeza ujue tu utakuwa unatafuta kufa mapema, ila kwakuanzia maisha inawezekana
Kikubwa ni huyo utaemwoa ndo ukuwe makini nae usije ukatembea ukiongea mwenyew barabaran.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom