Nataka kujilipua kuoa

Nataka kujilipua kuoa

Kuoa ni zaidi ya unavyowaza, kama hicho unachopata hakikutoshi vipi ukiongeza hapo mke na mtoto!!! Hebu Jaribu kuongeza hicho unachokipata kwanza ndo ufikirie kuoa
 
Inategemea na mwnamke mwenyewe kama ndo wale wa pesa pesa lazima uandae kuacha ya kutosha,, kwa haraka kwa kuwa umesema shida yako ni mtoto, naona usioe kwanza, utajuta. Ww unaendeshwa na tamaa tu , za kutaka mtoto. Ila hujasema kama unataka mke, watoto wapo tu, mwombe uncle wako akupatie ulee
 
Kabla yakua,jaribu kutathmini sehemu unayoishi vyakula vinanunulika bila kuathiri mfuko wako kwakiasi kikubwa,vipi matibabu unayamudu,unaweza kujitunza wewe pamoja na ndugu za mke wako pamoja na ndugu zako... majibu yakiwa NDIYO,basi una nafasi kubwa yakufanya maamuzi yakuoa.Vilevile jaribu kutathmini kama kipato chako kitaongezeka siku hadi siku kwani kadri siku zinavyosonga magonjwa kama homa ya ini,magonjwa ya figo n.k huweza kukukumba,vilevile tambua umuhimu wa kipato kuongezeka siku hadi siku itakusaidia kuweza kusomesha watoto wako kama ukijaaliwa.
 
Umri wako bado sana arif..mbona unataka kuwai kifungon mapema..nyie nďio mnaokuja kutesa familia zenu..umefika miaka 45 huko unaanza kufanya starehe za umri wa mtu wa miaka 26..usiruke stage dogo!!!!!
 
Mkuu nakushauri oa... huku umasaini unakabidhiwa mke ukiwa na miaka 18 na ng'ombe 15. Unajikata.

Oa mkuu . Oa chukua mke.
Unafanya mchezo na ng'ombe 15...? Bei ya Chini ya ngo'mbe ni 500,000/

Sasa piga 500,000 x 15 =7,500,000/=
Huo ni mtaji kabisa....Sasa yeye kasema kwasiku anaingiza 5000 mpaka 10,000/= so lini atamkuta huyo masai..?
 
Komaa kwanzaa kipato kifike hata elfu 30 kwa siku.Kulipia kodi,umeme,maji chakula..wife kwenda saloon..kuweka akiba na bajet ya maendeleo kwa kipato icho ni shida.Hakuna haja ya kukimbilia kuoa kwa umri ulionao.
Mkuu elfu 30 per day kwa bongo ni pesa moja kubwa saana laki 9 aseeh acha utani. Na familia nyingine hiyo laki 9 wanaishia kuiskia tu kwa mwezi.

Jamaa kama anahamu ya kuoa atafute mwanamke wa kiwango chake aweke ndani.
 
Unafanya mchezo na ng'ombe 15...? Bei ya Chini ya ngo'mbe ni 500,000/

Sasa piga 500,000 x 15 =7,500,000/=
Huo ni mtaji kabisa....Sasa yeye kasema kwasiku anaingiza 5000 mpaka 10,000/= so lini atamkuta huyo masai..?
Hao ng'ombe huruhusiwi kuwauza mkuu. Kukamua tu.

Elfu 10 ni kubwa. Familia nyingi zinaishi kwa 4000 kwa siku niamini. Atafute mwanamke wa kiwango chake aweke ndani budget watajibana humo humo ndani.

Au JF wote mambo safi nini? Mbona mimi elfu 10 per day pesa ndefu saana hahaha
 
jiulize kwanza je, unaweza kutegemewa. ukipata jibu ndo ufanye maamuzi.
 
Oa mkuu ndoa inaongeza msimamo kwa mwanaumme mtafutaji.
Ila akili kumkichwa... uwe makini kwenye chaguo la mtarajiwa wako wengine pasua kichwa!
 
Oa,
La muhimu unaetaka kumuoa aelewe una kipato gani?
Pia kabla ya kioa vizuri ukajua maisha ya ndoa yanakuaje?
Jaribu kutafuta mwanamke mwenye dini, mstahamilivu, asiependa makuuu, mwenye kujielewa na kuelewa maisha n.k
Riziki mtihani ni Mungu, tunafanya sababu ya kuitafuta ila tayari riziki yako ushaandikiwa.
Kuna mifano mingi sana ya waliooa wakawa hawana cha kuwatosheleza, Mungu akawaruzuku zaid ya kile walichonacho.
Mara nyingi gharama zinakuwa kubwa za maisha kwa matamanio na starehe.
Kama utaanza kula kilicho chepesi na kuvaa vilivyo vyepesi na kuacha anasa zote, naamini utaweza kumudu.
Ikisha ukioa utajitahidi tuu zaidi unavyofanya saivi maana unajua una Familia na huku ukimuomba Mungu.
Zingatia hayo kisha kama unayaafiki oa bila ya wasiwasi
 
Usioe tu kwa ajiri ya kutamani mtoto ...Oa kwa kuridhia toka moyoni lasivyo utamtesa tu huyo bidada atakapokuzalia. Thamani yake itaisha pale utakapoona mtoto "

Mimi nmeoa kwa kuridhia na nilimpenda mke wang toka moyoni " kipindi nipo bachela maisha yalikuwa tit sana" saa nyingne nalala njaa sababu ya matumizi mabaya ya fedha ....

Lakini toka nmeoa pesa naithamin ....
Nmeweza kuaminika kwa watu wakubwa, namaanisha
(Wenye mtandao wa pesa)
Sababu ya mke .....napata madili makubwa tofauti na zamani .... Kiukweli mke nae ana neema zake .......

NB: usioe kwa kushinikizwa
Na mtu flan...
Oa ukiwa umeridhia toka moyoni ' ......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom