Nataka kuikimbia Dar es salaam

Nataka kuikimbia Dar es salaam

una Option Mbili...Kubaki upigane! Au uondoke na ukapigane..!

Ukibaki Dar utapata hela mapema, tofauti na ukiondoka Dar.

Ukienda Mkoani, uwe na discpline ya matumizi ya hela mno ndo upate hela..otherwise ndo unapoteza kabisa..!

ushauri; Baki Dar, Hama mtaa unapokaa! badilisha njia unazotafutia kazi,na bafilisha aina ya kazi unayotafuta hapa dar!

Wanawake Dar ni wengi na hutawamaliza...! na pesa za Dar ni nyingi ni ww tu kuchagua njia ya kuzipata ambazo zipo nyingi...!

usikubali...Kukata....Tamaa ...Kamwe....

Safari ya mapambano ndo inaanza kaza buti mwanaume....!
 
Hakuna mkoa ninao ukubar kama DSM .kiufupi ni rahisi sanaa kupata pesa ukiwa dar ingawa ni rahisi pia kuzitumia .dar sihami mpaka watu wote wahamee

jiji ni gumu ila ni zuri unasota mwezi ila unapata pesa unapata sehemu ya kuzurura unapata vitu vingi vya kukuliwaza kuliko huko mikoani unakoenda Dar ndiyo tanzania iliko
 
Wakuu, Maisha yamekuwa magumu sana hapa jiji la Dar es salaam.. Tangu nipoteze kazi sababu ya corona imepita miezi 6 sasa sijapata shughuli ya kuniingizia kipato.. Maisha ya wazazi ni duni nimegoma kurudi nyumbani japokuwa ni hapa hapa Dar es salaam, naona ni udhaifu sana..

Maisha hayaendi kabisa!! Nimekuwa nikisubiri fao langu la NSSF ili nifanye kabiashara lakini taarifa nilizopata hawatoi Fao lote.. wanatoa asilimia (8)% tu.

Siwezi kufanya chochote kwa hiyo amount km itakuwa ivyo.. Nimechoka sana very desperate!! Na mpenzi wangu hatuelewani kabisa nadhani sababu ya kukosa kazi na hivi juzi nimehisi amenisaliti.. Nimeumia sana.

Natamani kutoka Dar es salaam nikatafute Maisha mkoa mwingine, au hata nchi nyingine Nafikiria kuuza vitu vya ghetto niondoke tu!!

Sitamani kuendelea kuwa hapa Dar nachanganyikiwa kila kitu hakiendi.

Ushauri
Mzee
Nakutakia kila laheri.
 
Huyo mpenzi lazima aendelee kukusaliti tu hilo jipange kisaikolojia kulipokea. si dhambi kwenda kujaribu maisha kwingine ila ujue tu unaelekea wp na umepanga kwenda kufanya nini.
Dah hii ndo inaniuma sana
 
Unapokuwa na mwanamke anaekimbilia kukusaliti ktk nyakati ngumu tambua ulifanya wrong choice, fikikiria namna ya ku-restore maisha yako acha kufikiria mwanamke.
Lakini hivi kumfuatilia mwanamke wako ni wivu wa kijinga? Au mwanamke anaetaka uhuru wake sana ni muaminifu kweli? Au mimi ndie nimekosea kumfumania!!
 
Mimi huwa nina amini kuwa tunakosa siku ya kwanza lakini tunapata zaidi ya tulivyostahili siku ya pili.
Fuata ushauri uliopewa na wakuu lakini pia usiache na usichoke kuzungumza na Mungu kwa imani yako.
Mungu wetu hachelewi wala hawahi atakufungulia milango mkuu
 
Back
Top Bottom