Nataka kufuga nyuki kisasa

Habari za asubuhi...baada ya takriban mwaka mmoja sasa naenda kuvuna mizinga yangu 170.Kazi hii taifanya kuanzia tarehe 1.6 .2025 baada ya kupewa taarifa mizinga mingi imeingia nyuki.Wataalamu wananishauri nikavune huku naikagua tena.Mrejesho utakuja hap.Mniombee maana nimeweka zaidi ya 7m
 
Tunakutakia kila la heri,ulete mrejesho tu
 
Kila la kheri Ukiwa field mpe hai msela wetu honeybager
 
Nimefanikiwa kufika shambani,hali inaridhisha kwani mizinga mingi ina nyuki.Hata hivyo haina asali zaidi ya matoto mengi.Tumekubaliana turudi Julai kwa ajili ya kuvuna.Nyuki wakali sana na nimepata sting kama 5 hivi
 
Nimefanikiwa kufika shambani,hali inaridhisha kwani mizinga mingi ina nyuki.Hata hivyo haina asali zaidi ya matoto mengi.Tumekubaliana turudi Julai kwa ajili ya kuvuna.Nyuki wakali sana na nimepata sting kama 5 hivi
Hongera sana mkuu
 
wametengeneza kwa bei gani
 
Nimefanikiwa kufika shambani,hali inaridhisha kwani mizinga mingi ina nyuki.Hata hivyo haina asali zaidi ya matoto mengi.Tumekubaliana turudi Julai kwa ajili ya kuvuna.Nyuki wakali sana na nimepata sting kama 5 hivi
safi road 5
 
MREJESHO
Baada ya mwezi Juni kukuta watoto wengi,nikashauriwa nirudi baada ya mwezi mmoja nimekuta mambo yafuatayo;
1.Nyuki wamekula asali kama yote,yaani ktk mizinga zaidi ya 150 tumepata kama lita 40 tu.
2.Nyuki ni wengi sana shambani na almost kila mzinga wameingia.

WAYFORWAD;
-Inoanekana fundi wangu hajui muda sahihi wa kuvuna,wanasema ukiona matoto mengi usivuke wiki 1 au 2 urudi kuvuna (TUMEPISHANA NA KALENDA)
-Nimevuna masega yote waliyokula asali yake ili angalau nipate nita nirejeshe gharama za wavunaji.
-Nataraji kuvuna tena kama tawahi kuanzia October 2025.

HITIMISHO
-Kazi ya kufuga nyuki sio kutundika mizinga tu,kuna mabo mengi yanahitaji kufuatiliwa na kwa kuzingatia jigrafia ya eneo lako.

ASANTENI
 
Asante sana kwa mrejesho na pole kwa changamoto, hivi ndo inavotakiwa mada ziwe. Uwe mfano wa kuigwa .
 
kazi kazi mkuu changamoto hazikosi
 
Mkuu nimekufuatilia kwa ukaribu sna ahsante sana kwa mrejesho
 
1. Ni eneo gani unakogugia?
2. Na je, umekwenda kuvuna Juni unatambua Nyuki wakiingia lini kwenye Mizinga yako?

**Kuepuka kukuta Asali imeliwa tunashauti kuna na Mizinga yenye vikinga Malkia na madume (Queen Excluder) Hii itakusaidia Sana maana ukiwa na Mizinga Single bos isiyo na Kikinga Malkia hizo ndiyo changamoto zake.
Mzinga unaweza kukuepusha na kulimwa Asali ni aina ya Langstroth (double box) wengine huita ya gorofa na usije kuwekwa wavu Bali Kikinga Malkia.
 

UNAJUA FAIDA YA KUWEKA KIKINGA MALKIA KWENYE MZINGA WAKO?

Wafugaji wengi wamekuwa wakifuga Nyuki kwa kutumia mizinga yenye chemba moja (Single Box) badala ya ile ya chemba mbili (Double Box) maarufu kwa jina la Mizinga ya Ghorofa au kwa jina la kitalaamu la #Langstroth. Ili kutumia Kikinga Malkia lazima mzinga wako uwe wa aina ya Langstroth au (Double Box) na Sanduku hizi kila moja inakazi zake ambapo Sanduku la chini huitwa Blood Chamber (Chemba ya Uzazi) na juu huitwa Super Chamber (Chemba ya Asali).
Kwa kawaida sanduku hizi mbili hutenganishwa kwa katikati kuwekwa Kifaa maalum ambacho kinajulikana kama Queen Excluder (Kikinga Malkia). Chemba ya chini ndiyo inayopaswa kuwa na malango wa nyuki kuingia na kutoka ili Malkia na Nyuki waingie kwanza kuanza kuishi/kufugwa. Wapo baadhi ambao hutumia mizinga yenye chemba mbili (Double Box) lakini huweka wavu wa madirisha ya nyumba.
Kutumia Wavu wa madirisha kama mbadala wa kikinga Malkia (Queen Excluder) kwa lengo la kupata Asali zaidi wakati wa uvunaji lakini wavu huo hausaidii sababu una matundu makubwa zaidi ya mm 4 yanayoruhusu Nyuki dume na Malkia kupita. Lakini Kikinga Malkia kimetengenezwa kwa kipimo ambacho ni size inayozuwia Malkia na madume kupita.
Ukitumia kikinga Malkia tunatarajia kupata faida nyingi ambazo ni;
• Asali ivunwayo katika supers Chamber (Chemba ya Juu) ambako Malkia hafiki huwa safi kutokana kutokuwepo kwa Malkia au mayia, watoto.
•Nyuki hueenea zaidi kwenye masega ya majana (watoto) kuliko masega ya asali hivyo hurahisisha kazi ya uondoaji wa nyuki kutoka kwenye masega ya asali kuwa rahisi na wa haraka.
•Husaidia uchunguzi wa magonjwa na kutambua uimara wa Malkia iwapo anaweza kufikia idadi ndogo ya fremu (viunzi) katika eneo dogo la koloni au laa.
•Masega ya Majana (Watoto) huwa meusi zaidi kutokana na shughuli za uleaji watoto, lakini masega ya chemba ya juu ya asali hutoa Nta Safi na nzuri yanapochakatwa.
•Hata Mfugaji anapochelewa kufuga Asali anaweza kuikuta kutokana na madume walao Asali haraka kuwa chemba ya chini.
Hizi ni sehemu tu ya faida ambazo nimekudokolea leo.
 
 
Asante kwa ufafanuzi wenye faida,Nilienda Sabasaba ya mwaka huu nikakuta kuna mizinga ya Top bar(single box) lakini imewekwa kitenga malikia katikati,je umeshawahi kuisikia na unaizumgumziaje?
 
Reactions: Lax

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…