Nataka kufuga nyuki kisasa

BARA BARA YA 5

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
1,127
734
Nimefanikiwa kupata shamba la ekarim kama 50 ambapo kati ya hizo 20 ni msitu, lina chanzo cha maji cha ukakika na nimeshauriwa nifuge nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa.

Niefikiria kuweka mizinga 200 ya kisasa ambayo kwa wastani nipate madumu ya lita 20 kama 150 kila ninapovuna.

Mizinga nitaiweka kwenye banda na nitaweka mtu wa kuishi huko shamba ili awe anaikagua na asali yangu nitauza Dar es Salaam au soko la nje kwa wastani wa TZS 200,000.

Mizinga nitaichona kwa elfu 20m kila mmoja kwa kuwa mbao zinapatikana kwa urahisi na fundi wangu hana bei kubwa.

Mizinga nitaiweka mwezi Desemba 2023 na mvuno wa kwanza utakuwa around June 2024. Soko la asali na nta halijawahi kuwa baya kama utazalisha Quality product.
 
Nimefanikiwa kulipata shamba lenye msitu kama.20 acres.Nitachana mbao kutoka shambani baada ya kukuta magogo yankutosha.Mbao zitaniwezesha kutengeneza hadi mizinga 200
Ukikamatwa na TFS unachana mbao utajuta kujua Urambo. Mtaji wote utaishia huko. Kabla hujafanya chochote hakikisha unakuwa karibu na hilo jeshi usu mkuu!
 
Mkuu vipi ushaweka Mizinga?Alafu fanya kama unatupatia bei kwa ekari 1 pande za huko,hata kama siyo bei halisi basi makadirio +-.
Mkuu vipi ushaweka Mizinga?Alafu fanya kama unatupatia bei kwa ekari 1 pande za huko,hata kama siyo bei halisi basi makadirio +-.
Bei haizidi laki tatu kwa acre moja. Huko porini hata kwa laki na nusu unapata
 
Nimefanikiwa kupata shamba la ekarim kama 50 ambapo kati ya hizo 20 ni msitu, lina chanzo cha maji cha ukakika na nimeshauriwa nifuge nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa.

Niefikiria kuweka mizinga 200 ya kisasa ambayo kwa wastani nipate madumu ya lita 20 kama 150 kila ninapovuna.

Mizinga nitaiweka kwenye banda na nitaweka mtu wa kuishi huko shamba ili awe anaikagua na asali yangu nitauza Dar es Salaam au soko la nje kwa wastani wa TZS 200,000.

Mizinga nitaichona kwa elfu 20m kila mmoja kwa kuwa mbao zinapatikana kwa urahisi na fundi wangu hana bei kubwa.

Mizinga nitaiweka mwezi Desemba 2023 na mvuno wa kwanza utakuwa around June 2024. Soko la asali na nta halijawahi kuwa baya kama utazalisha Quality product.
Hongera kwa kuwa na wazo zuri, lakini naomba nikutahadharishe nimeona umeandika Mizinga 200 unawekeza na umesema mavuno Juni 2024. Hutoweza kuvuna mzinga hiyo sababu kuwa na Mizinga ni jambo moja lakini kuijaza nyuki ndiyo hatua ngumi zaidi kuliko zote.
Fanya utagiti zaidi kuhusu ufugaji nyuki na ukiweza itafute elimu ya nyuki. Vinginevyo utapata presha.

Mimi nafuga leo mwaka wa 5 sasa. Karibu kwa ushauri kwangu +255622 642620 au tembelea chuo cha Nyuki Tabora wakushauri.
 
Screenshot_20231214-174154.png

MIZINGA BORA AU WA KISASA NI UPI?

Pengine nawe ni mmoja wa watu wanaojiuliza swali hili au unachanganywa na matagazo yetu wafanyabiashara kiasi cha kutokujua mizinga wa kisasa ni upi!
Kwanza naomba tukubaliane kuwa kuna aina 3 za mizinga ambazo ni;
a) Mizinga ya Asili
b) Mizinga ya Kisasa
c) Mizinga ya Mapambo

MIZINGA YA ASILI:
Sitozungumzia zaidi kuhusu Mizinga ya Asili sababu ni mizinga isiyo na tija ambayo ukivuna unalazimika kukata masega your na wakati Mwingine ukivuna mizinga huharibika.

Mizinga hii ilitengenezwa kwa vyungu, magome ya miti hata majani. Kasoro yake kubwa ni wakati wa uvunaji na haimpi nafasi mfugaji kuangalia iwapo kuna asali au laa sababu haina viunzi.

MIZINGA YA KISASA:
Kwa sasa watu wengi wamekuwa wakiamini kila mizinga wa mbao ni mizinga ya kisasa. Lakini kuna mizinga ya mbao lakini ndani yake ukiwa na muundo wa mizinga wa Asili hivyo nataka tukubaliane siyo kila mzinga wa mbao ni mzinga wa Kisasa.

Sifa ya mzinga wa kisasa lazima uwe na viunzi au frem ndani yake hii ndiyo itautofautisha na mizinga ya asili.

KIUNZI/FREMU: Kazi kubwa ya Viunzi au Fremu katika mizinga ni kuwaongoza nyuki kujenga masega yao juu yake hivyo kurahisisha ukaguaji wa masega au asali bila kuathiri mazalia ya nyuki.

Hivyo mizinga aina ya Top Bar, Kamala, KCH na nyinginezo ni mizinga ya Kisasa lakini ikitayariswa bila Viunzi au Fremu haitakuwa ya Kisasa pia.

MIZINGA YA MAPAMBO: Hii pia ni mizinga ya kisasa lakini mingi imekusudiwa kwa ajili ya Mapambo hivyo hutayatishwa uliwa na Mambo tofauti tofauti.
Sifa kubwa ya mizinga hii ni kuwa kivutio na humuwezesha mfugaji kuwaona nyuki wakiwa ndani ya mizinga hivyo mingi huwa na kioo pia. Aina hii pia hutumika hata kwa ajili ya utafiti.

MZINGA BORA:
Sasa baada ya kujua aina zote hizi naomba nikueleze mzinga bora ni upi kwa ufugaji wa Kisasa na wenye tija! Mzinga wenye Viunzi au Fremu na kikinga Malkia huu ndiyo mzinga bora kwa sasa na wenye tija.
Sifa za mzinga huu ni kwamba lazima Sanduku (Chemba ya chini) iwe kubwa kuliko ya juu (Chemba ya juu).

Mzinga huu unafaida zaidi kwani;

• Asali ivunwayo katika supers Chamber (Chemba ya Juu) ambako Malkia hafiki huwa safi kutokana kutokuwepo kwa Malkia au mayia, watoto.

•Nyuki hueenea zaidi kwenye masega ya majana (watoto) kuliko masega ya asali hivyo hurahisisha kazi ya uondoaji wa nyuki kutoka kwenye masega ya asali kuwa rahisi na wa haraka.

•Husaidia uchunguzi wa magonjwa na kutambua uimara wa Malkia iwapo anaweza kufikia idadi ndogo ya fremu (viunzi) katika eneo dogo la koloni au laa.

•Masega ya Majana (Watoto) huwa meusi zaidi kutokana na shughuli za uleaji watoto, lakini masega ya chemba ya juu ya asali hutoa Nta Safi na nzuri yanapochakatwa.

•Hata Mfugaji anapochelewa kufuga Asali anaweza kuikuta kutokana na madume walao Asali haraka kuwa chemba ya chini.

Aina hiyo ya mzinga imekuwa ikijulikana kama mizinga ya ghorofa au Langstroth huu ndiyo mzinga bora wa kisasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom