Wasiliana nasi sasa kwa mahitaji ya miche bora ya korosho kwa shilingi 1000 tu.
WhatsApp/call/text
0766006128
0655715184
0683433440
Ofisi zipo kilombero &kibaha (opening soon).
Vile vile tuna miche mbali mbali ya mbao kwa shilingi 400 tu
Nimefurahishwa na uzi huu. Bahati mbaya nimeingia wakati umeshaenda sana lakini natumaini mchango wangu unaweza kusaidia. Mimi ni mmoja wapo wa watu waliohamua kuingia kwenye hiki kilimo cha Korosho.
Ni mmoja wapo wa walipata ardhi Manispaa ya Lindi na kupambana na kusafisha misitu. Mpka sasa hivi bado tuko site tunapambana maana kazi ya kusafisha misitu si kazi lelemama.
Huko tunaambiwa na wataalamu kuwa tupande kwa upana wa 12m x 12m, hivyo tunaweka miche 25 kwa ekari. Miche wanatoa bure.
Naweza kukubaliana na Lumumba nadhani ni kweli tunapoteza ardhi kwa kupanda miche 25 kwa ekari lkn ni ngumu kutofuata masharti ya wataalamu na Board ya Korosho wanaotoa miche.
Nadhani wazo la kupanda mingi alafu ukapunguza ikianza kushikana ni wazo zuri kabisa. Ntajaribu kuwauliza wataalamu na kuleta mrejesho.
Kagalala - Uliweza kupata mrejesho juu ya hili suala - kama wataalamu wa bodi ya korosho wanaridhia kupanda miche 120 kwa ekari (kwa upana wa mita 5-6 x 6-7)? Nauliza kujua kama ukiomba miche yao (ile wanayogawa bure) kama watakubali kukupa miche zaidi ya kipimo chao cha 25 kwa ekari
HapaKatika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!
Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!
Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!
Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.
Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.
Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!
Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!
“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
Hapa
Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa, nimekatishwa tamaa lkn bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa.
shukrani mkuu.
Habari LumumbaHABARI,
"Mandison,
Gharama za kuanzisha kilimo cha koroso sio kubwa sana haizidi laki moja kwa heka,Korosho ni zao linalokubali katika mikoa mingi hapa tanzania ukiacha mikoa yenye umaarufu, MTWARA, LINDI, PWANI, TANGA, iko mikoa mipya.
KamaTABORA,SINGIDA,DODOMA,SOGWE,RUKWA huko kote zao la korosho linastawi vizuri fanya mawasilianano na kituo cha utafiti wa kilimo cha naliendele. Watakupa maelekezo mengi sana nadhani maswali yako yote utapata majibu pale.
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI)
Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com
LUMUMBA
Asante kwa taarifa Je, mkuu msimu wa kupanda ni miezi ipi ambayo kuna mvua. Nahitaji kujuaKwa kuwa unataka kuanza kupanda habari ya madawa sitakueleza.Tafuta shamba maeneo ya kusini mwa Tanzania(lindi ,mtwara,tunduru).Miche tunapanda kipindi cha mvua ambapO halmashauri husika wanagawa niche kupitia serikali za vijiji.Kumbuka mbegu wanayotoa ni ya miaka mitatu,ila mavuno yanaongezeka kadri ya umri wa mti unavyoongezeka.Uzoefu unaonyesha kuwa mashamba mengi yanamilikiwa na Wazee,hivyo kuna umuhimu wa vijana kuanza kupanda miti mipya kwenye maeneo mapya ili kutransfer uchumi uje kwetu.Kwa wale wanaonunua mashamba yenye miti iliyozeeka wanachofanya no kupanda niche mipya na kukata ya zamani pale mipya inapoanzaa kuzalisha.
Mkuu ulishapata shamba?Huu uzi umenipa mwanga, hata mimi nina mpango wa kununua mashamba huko kusini ili nilome zao hili. Hii ni moja ya ndoto zangu