Nataka kuanzisha shamba la korosho 32 acres

SamWise

New Member
Aug 28, 2018
1
20
Nimefurahishwa na uzi huu. Bahati mbaya nimeingia wakati umeshaenda sana lakini natumaini mchango wangu unaweza kusaidia. Mimi ni mmoja wapo wa watu waliohamua kuingia kwenye hiki kilimo cha Korosho. Ni mmoja wapo wa walipata ardhi Manispaa ya Lindi na kupambana na kusafisha misitu. Mpka sasa hivi bado tuko site tunapambana maana kazi ya kusafisha misitu si kazi lelemama.
Huko tunaambiwa na wataalamu kuwa tupande kwa upana wa 12m x 12m, hivyo tunaweka miche 25 kwa ekari. Miche wanatoa bure.
Naweza kukubaliana na Lumumba nadhani ni kweli tunapoteza ardhi kwa kupanda miche 25 kwa ekari lkn ni ngumu kutofuata masharti ya wataalamu na Board ya Korosho wanaotoa miche.

Nadhani wazo la kupanda mingi alafu ukapunguza ikianza kushikana ni wazo zuri kabisa. Ntajaribu kuwauliza wataalamu na kuleta mrejesho.
Kagalala - Uliweza kupata mrejesho juu ya hili suala - kama wataalamu wa bodi ya korosho wanaridhia kupanda miche 120 kwa ekari (kwa upana wa mita 5-6 x 6-7)? Nauliza kujua kama ukiomba miche yao (ile wanayogawa bure) kama watakubali kukupa miche zaidi ya kipimo chao cha 25 kwa ekari
 
fungafunga

Member
Mar 30, 2010
84
125

Kwanza hakuna miche ya bure this year hiyo ilikuwa ni programme ya 2017/2018. Sina hakika na idadi ya miche unayoweza pewa kwa ekari ila wanasisitiza miche 28 tu kwa ekari!
 
Englishlady

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
1,671
2,000
Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
Hapa

Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho?? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa...nimekatishwa tamaa lkn bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa....
 
fungafunga

Member
Mar 30, 2010
84
125
Hapa

Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho?? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa...nimekatishwa tamaa lkn bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa....
Ni kweli! Ushauri wa mama yetu upo sahihi kabisa! Uwekezaji wowote unahitaji usimamizi (supervision) ya hali ya juu! Kumbuka kuwekeza ni jambo moja na kusimamia uwekezaji wako ili kufikia malengo uliyojiwekea ni jambo jingine!
Kuhusu kuibiwa wakati wa mavuno hiyo ni kweli ila inategemea na nguvu kazi uliyojiwekea katika hicho kipindi cha miezi miwili ya mavuno ili kuhakikisha hakuna upotevu mkubwa kwa njia hiyo!
Bado nakusisitiza amka na ifuate NDOTO yako!
All the best!!!!
 
Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
2,973
2,000
Hapa

Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho?? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa...nimekatishwa tamaa lkn bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa....
Hata Mimi pia nishapanda toka December na korosho zimeanza kuota, ila kazi zinabana sana yaan hapa napiga hesabu za kwenda pasaka,
Kitu ambacho nakiona shamba linaweza lisikulipe awamu ya kwanza au ya pili ila siku likija kukulipa utashangaa sana, Shamba langu lipo masasi nami nipo Zanzibar/Dar es salaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PatriceLumumba

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
411
1,000
Kwa ardhi ya kagera naweza lima korosho?
HABARI,
"hazard Don,
Hongera kwa Swali zuri ambalo jibu lake litawasaidia wengi,Kwa kifupi Tanzania karibu 75%ya eneo lote mazao mengi ya biashara yanakubali mojawapo ikiwa korosho sasa kwa mkoa wa Kagera kuanzia Nsunga,Kyaka,Kyerwa,Nkwenda,Kayanga,Omurushaka,Kamachumu,Rushwa,Kashasha,Nshamba,Muleba,Nyakasanza,Nyabugombe,Nyonga,Muzani,Bihararumo,Ruhuma Na maeneo mengi ya Nyanda za huko Korosho inakubali kama Singida na Dodoma mikoa yenye mvua chache korosho inakubali huko hakuna shida kabisa .
LUMUMBA
 
hazard Don

JF-Expert Member
Oct 9, 2017
696
500

Akhsante kwa majibu mazuri.
 
nsa ji

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
288
250
Wana jamvi! Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote!
Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!
Natanguliza shukrani!
Habari
Fungafunga; Unaendeleaje na mradi? ulifanikiwa kupanda shamba lote?
nawiwa kufahamu hatua uliyopiga kwakuwa nipo mbioni kuchukua mkondo huu pia... Ahsante

Sent from my SM-J330F using JamiiForums mobile app
 
fungafunga

Member
Mar 30, 2010
84
125
Habari
Fungafunga; Unaendeleaje na mradi? ulifanikiwa kupanda shamba lote?
nawiwa kufahamu hatua uliyopiga kwakuwa nipo mbioni kuchukua mkondo huu pia... Ahsante

Sent from my SM-J330F using JamiiForums mobile app
Nilifanikiwa aise namshukuru MUNGU! Nilianza usafi kwa kufyeka msitu mwezi julai 2018 na kufikia novemba nikawa na 50 acres ambapo nilichoma moto kupiga mashimo na kupanda ekari zote 50 ilipofika january 2019. Nimepanda mikorosho kwa ushauri wa ndugu zetu wa chuo cha kilimo Naliendele na mpaka hivi sasa inaendelea vizuri sana!

Mwezi julai tena mwaka huu ntaendelea tena kumalizia kipande cha msitu kilichobaki ili 2020 januari nimalizie eneo lililobaki!

*KARIBU SHAMBANI BROTHER*
 
Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,156

Mkuu umetumia kiasi gani kwa acre kusafisha pori?? Nataka kusafisha pia mwezi wa Saba, ila watu wa huku wavivu sijapata ona, Niko pwani.
 
fungafunga

Member
Mar 30, 2010
84
125
Mkuu umetumia kiasi gani kwa acre kusafisha pori?? Nataka kusafisha pia mwezi wa Saba, ila watu wa huku wavivu sijapata ona, Niko pwani.
Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu
1. Aina ya msitu/miti iliyopo.
2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili...)
3. Aina ya wafanyakazi unaowatumia. Utatumia wenyeji au wageni wanao toka mbali na eneo husika (Hapa kuna vitu vingi tena vya kuviangalia na changamoto zake)

Ila kwa kifupi garama zilizopo sokoni kwa sasa ni kati ya Tshs 280,000 hadi 320,000 kwa ekari moja ukiondoa garama ya kununua mashine (chain saw), vifaa vya kazi ikiwamo mapanga, tupa,na buti, kupiga mashimo, miche na kupanda.

Ila usiogope bro karibu sana..
 
Mimi sidhani kama nahitaji chainsaw, wachoma mkaa walishanisaidia kwa Hilo, vimebakia vichaka vichaka tu.

Asante though.
 
Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
2,973
2,000
Mimi natumia elfu 70 kwa heka hapo miti mikubwa bado ambayo inahitaji chain saw so roughly kama laki 1 hivi nataka kukata hiyo miti ili July nisafishe na kuchoma moto,
November nawahi kupanda,
Shamba langu lipo Masasi
Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu
1. Aina ya msitu/miti iliyopo.
2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili...)
3. Aina ya wafanyakazi unaowatumia. Utatumia wenyeji au wageni wanao toka mbali na eneo husika (Hapa kuna vitu vingi tena vya kuviangalia na changamoto zake)

Ila kwa kifupi garama zilizopo sokoni kwa sasa ni kati ya Tshs 280,000 hadi 320,000 kwa ekari moja ukiondoa garama ya kununua mashine (chain saw), vifaa vya kazi ikiwamo mapanga, tupa,na buti, kupiga mashimo, miche na kupanda.

Ila usiogope bro karibu sana..
 
nsa ji

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
288
250
Mimi natumia elfu 70 kwa heka hapo miti mikubwa bado ambayo inahitaji chain saw so roughly kama laki 1 hivi nataka kukata hiyo miti ili July nisafishe na kuchoma moto,
November nawahi kupanda,
Shamba langu lipo Masasi
Mkuu ninashamba masasi pia, lkn maafisa wa misitu wanakataza kutumia chainsaw kuangusha miti, hivyo tunalazimika kutumia moto na misumeno baridi kwako hali ipoje?
 
Mandison

Senior Member
Mar 10, 2017
177
225
Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
Changamoto nyingine kubwa kwa shamba jipya ni nyani! Hawa wanyama wanaweza kukutia hasara hadi ukashangaa maana huwa wanafukua miche ya mikorosho na kuing'oa. Labda Kama kuna utaalam wa kuwathibiti tofauti na kuweka mtu wa kulinda tusaidiane ujuzi tafadhali
 
Top Bottom