Nataka kuacha kazi .

Kama hiyo nyumba ipo hapahapa mjini, hao walezi labda wangekupatia chumba hapo ukawa unaishi hapo ukaokoa hela ya kodi.

Kama hawawezi kukupatia hata chumba na kodi yote wanachukua halafu bado wanakuomba msaada, usipowapa msaada naona ni fair

Halafu, inakuaje hadi unapata mshahara wa 220k, ni mkopo ulichukua? Kama ni mkopo, utaisha lini?
 
Hayo ni mapito tu,Maisha yetu yalivyo ni kama uonavyo season za vipindi vya majira katika mandhari zetu kama kuna kipindi cha joto,Masika,vumilia maisha ndivyo yalivyo,Na pia kama unauwezo jaribu kutafuta mume uolewe huenda mawazo yakakupungikia
Uoe singo parent mwenye watoto wawili wa mwanaume mwingine?!!!
 
post yako inaonesha kuna kitu nyuma ambacho ndio shida kubwa kwako na sio hivyo ilivyotaja. Na kwa haraka haraka ni kama unadeni "mkopo" na hauwezi kuulipa kwa wakati.

Pambana, si kuna msemo wa wanawake mnaweza, mara malkia wa nguvu !!?.... Ndio mahali pale hapo sasa, hakuna kukata tamaa.
Btw, ikiwa una muamini Mungu, omba sana, sio kilegevu, omba kwelikweli, omba mpaka kitu kitokee. Mungu hata siku moja hataacha kukukirimia mahitaji yako.
 
usiache kazi, utadhalilika zaidi nashauri uendelee na kaihuku ukitengeneza namna nyingine kama kujiajiri nk ni ngumu sana kupata kazi ya serikali, kazi za watu binafsi watu wanadhalilika zaidi kuliko za serikali
Hiii Chukua kwa Mikono Miwili[emoji818]
 
Nadhani hiyo Plan B. Yako bado inahitaji maandalizi ya kutosha! Endelea kujipanga kwanza.....kwa sasa utadhalilika.
 
pole sana mkuu, hali si shwari biashara zinayumba sana
 
Kitu cha kwanza somesha watoto shule za kawaida mpk mambo yatakapokaa sawa,ishi nyumba ya bei nafuu na nunua vyakula vya jumla.Pia kula ili uishi,acha kula kwa anasa yaani vile unavyovipenda/kuvitamani.
Mungu atakusaidia.[emoji120]
 
Hii Ndiyo Hali Halisi ya Watumishi wa Sasa
Kwanza Usizani Uko peke yako
Tuko wengi mno
Kazi Usiache
Biashara Ingekua Dili Ungeona kila jilani yako mjasiriamali anakua milionea
Nje ya utumishi ndio kugumu sana maana na wao wanawategemea wafanyakaz na mfanyakaz mwenyewe ndio wewe
Hali ya Utumishi kwa sasa ni ngumu sana ila yatupasa kuvumilia coz ni upepo tu huu, utapita mantahofu
Kikubwa Review Mapato na Matumizi yako uyaadjust accordingly, ondoa luxuries
Watoto warudishe kayumba tu mpk hali itakapokaa sawa
 
Jiongeze. Tafuta sehemu jion upike vi-bites, au choma mahindi, au anzisha genge la kichaga, au omba uhamisho uende karibu na kwenu, au omba uhamisho uende sehemu ambayo utafanya shughuri za kilimo.

Ila

Usiache kazi, utakuwa muuza ngozi wa ovyo kabisa. Utapigwa hata kwa buku
 
Daaah!pole sana mkuu,.Nionavyo Mimi ambaye nimechelewa ni mjinga sikusoma tatizo lako la kwanza umekata tamaa. Hope is the last thing you need to lose.if you loose hope you are dead. Ngoja nimuambie kitu binti,
If you want to travel faster than you have to travel light. Acha mzigo mizito mkuu.
Mizito uliyonayo
1.watoto
Najua unawapenda sana kwa sababu ya uchungu uliopata wakati WA kuwaleta duniani, Mpe baba yao,usitake kujua wanatesekaje Kwa mama wa kambo, watakua tu baba yao hawezi kuwaua.

2.Elimu
Kama option one imeshindikana Pliz wapeleke kayumba
3 Nyumba
Kakae nyumba mbaya ya bei rahisi
Mwisho anzisha kampuni ukiwa Kazini ili ufanye tathmini ya uwekezaji wako
Usijiue,watu wanaojiua ni waoga.
 
Mkuu nahitaji tuongee hii ishu
 
Usitegemee kipato cha serikali unakufa masikini.uza uwanja mmoja fungua biashara.niambie upo mkoa gani ntakuambia ufanye biashara.usifikirie kufa kisa maisha mungu akutie moyo wa ujasiri
kwa Mkoa wa Geita Fursa gani
 
pole sana ila kama wachangiaji waliotangulia walivyo kushauri, nyakati ngumu huwa hazidumu milele. usiogope kufungua biashara hata kama ni ya ndizi mbivu unanunua sokoni shilingi hamsini unazivundika alafu unauza kwa sh. 200 au 150. na usiogope fedheha kwa watu na ukiogopa hata kujishughulisha hata ungelipwa milioni ungelalamika tu.
 
Mikopo inatutesa sanaa Watumishi wa Umma.

#YNWA
 
Mkuu kama sijakosea nimeona sehemu umesema una viwanja vitatu? Uza kimoja, fungua kijiofisi simple tu, kisha hapo uza maziwa, popcorn, juisi za matunda, maji na vingine jiongeze mwenyewe, kisha achana na hiyo kazi, utarudi kunishukuru, juice glass 1000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…