Nataka kuacha kazi, biashara gani inalipa kutoka Tanzania kwenda Malawi na Zambia?

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,556
45,859
Jamani maisha magumu bongooo. Mimi nataka kuacha kazi nianze biashara ila nimeona hapa bongo kwa sasa hela hamna bora nitoke kidogo. Naombeni ushauri ni biashara gani inayolipa ya kufanya huko Malawi au Zambia. Pia mtaji wangu ni mdogo tu kama milioni sita hivi.

Pia kama kuna mtu anahitaji partner tupige kazi nipo tayari ila kama wewe ni tapeli wala usipoteze muda wako maana huwezi nitoa hata mia, hapa kazi tu.

2023 mrejesho
Nimejikuta kwenye hii post baada ya mtu kuniquote
Mrejesho soma anzia post 244
 
Zambia usipeleke mahindi, wao wanalima mahindi misimu miwili na wana mahindi mengi sana kwani baada ya mugabe kuwafukuza settlers walihamia zambia na wana mashamba makubwa
ndo maana nimemuuliza huyo jamaa alosema nipeleke mahindi zambia. maana najua kule wana mahindi sana. kwaiyo nipeleke nini mkuu? nguo za wanawake,watoto ,viatu italipa?
 
peleka nguo zambia,ila zile nzuri ambazo ziko on demand bongo,wazambia wana akili fulani sijui ni mbaya au ni nzuri,wanaamini mbongo ndio anajua kuvaa nguo nzuri na kila nguo inayompendeza mbongo uzuri wake unatokana na bei kubwa ya hiyo nguo,yaani kwa lugha nyingine wanaamini nguo ili ikupendeze lazima inunuliwe bei ghali,basi tunduma wanawapiga sana wafanya biashara wa nguo wa pale
 
kama nini mkuu? nini naweza kuchukua kariakoo nipeleke kule?
Bidhaa kwa malawi hasa vyombo vya ndani utauza kuanzia muzuzu, chitipa na maeneo mengine, ngano pia kwenye hizo nchi utauza maana nilikua nafika kuanzia chinsali hadi kitwe zambia nakuta ngano ya bongo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom