Nataka biashara itakayonisomesha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka biashara itakayonisomesha.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Black African, Oct 18, 2011.

 1. B

  Black African Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari za leo imani yangu muwazima wa afya,nami namshukuru mungu naendelea vizuri.Naomba maoni yenu,me ni mwanafunzi kidato cha 5 ktk shule moja ya serekali hapa mjini znz,tangu nimefaulu nimekuwa nikajitegemea kwa gharama zote za kusoma pmj na matumizi madogomadogo,nimejipigapiga kutafuta kiasi cha pesa ili uwe ndio mtaji,hadi sasa nimefanikiwa kupata Tsh.100,000 nataka nifanye biashari ila sijuini biashara gani itaniendesha bila ya kuathiri masomo yangu.Ahsanteni
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  haipo biashara ya hivyo, sahau...
   
 3. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Wewe unataka kufanya bishara gani?
   
 4. Erick_Otieno

  Erick_Otieno JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 28, 2010
  Messages: 630
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 180
  Kwa nini haipo biashara kama hiyo na asahau?
   
 5. Senior Boss

  Senior Boss JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 3,285
  Likes Received: 2,025
  Trophy Points: 280
 6. C.K

  C.K JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45

  Acha kujibu majibu negative.., nyie ndo mnakatisha watu tamaa. Kwa nini umjibu mtu hivyo!! SIPENDI MIMI WATU KAMA NYIE! SIPENDI!!!

  "...even a fool is considered wise when he keeps silence"
   
 7. B

  Bonge JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2011
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 865
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 80
  Jaribu kufanya utafiti wa matumizi ya mkaa mitaa unayoishi. Unaweza wakati wa weekend unaenda kununua gunia za mkaa sehemu unapouzwa kwa bei nafuu unakuja uza mtaani kwenu kwa jumla maana rejareja na wewe unasoma itakuwa shida labda uwe na msaidizi.
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Tafuta eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu mfano sokoni..vyuoni.. n.k.. tafitaia mahitaji yao ya vocha... jipenyeze hapo...zungusha mtaji wako..

  Namfahamu jamaa alianza na kulisha ng'ombe wa mtu.... akaajiriwa katika kibda cha chipsi.. akajikusanya akachukua benchi akaliweka stendi ya daladala chuo kikuu UDSM akauza vocha kwa wanafunzi wa chuo(2000,1000,500,250..)... kafanikiwa akanunua pikipiki yake mwenyewe akamwachia mdogo wake kijiwe.. akashika hela akanza kula ngamia... sijui alipo hivi sasa lakini walau unapata picha watu walipoanzia...!Penye nia pana njia...

  Ukikuza mtaji wako rudisha mrejesho humu upewe mawazo mapana zaidi..!
   
 9. B

  Black African Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma.Mkeshahoi.
   
 10. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Uza vocha, na bites ndogondogo kwa wanafunzi wenzako
   
 11. n

  naivasha Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nawashukuru wana JF ambao mmekuwa mstari wa mbele kumshauri huyu mdau. Ndg yangu Black African ushauri umepewa. Kimsingi mtaji ulionao unatosha kuanzisha biashara ya kiwango cha fedha hiyo 100,000/=. Pia soko kwa ajili ya biashara unayotakiwa kuanzisha liko ama katika eneo unaloishi au unakosomea kwani wadau wake ndo wanaotakiwa kuwa wateja wako. Mimi ninakupa ushauri huu:-
  1. Nunua mifuko ya maji/barafu pakiti moja Sh. 1,000/= ambayo ina pcs 100 anafunga maji na kuyapoza kidogo kwenye fridge kisha kuyauza @ mfuko Sh. 50/=. Hapa una uhakika ya kupata gross income ya Sh. 5,000/= . Kazi ya kufunga maji ni nyepesi, haitumii muda mwingi na unaweza kuifanya kulingana na muda wako hata kama ni usiku, kama nyumbani kuna friji unaweka maji yako huko au ukatumia deli. Biashara hii unaweza kuwa unamwachia mtu ama mwenye duka au genge kwa makubaliano ua kumpa Commission. Itakulipa ndg yangu kwa ushauri zaidi tuwasiliane
  2. Anzisha genge dogo kulingana na fedha uliyonayo. Biashara hii inahitaji uwe na msaidizi wakati unapokuwa shuleni au unapokuwa umetingwa na masomo. Pale unapokuwa na muda nawe simamia uongeze nguvu. Chagua vitu vidogo vidogo vinavyotumika sana kila siku majumbani mfano mkaa, vitunguu, mafuta ya kupima, pipi, n.k. Hapa unaweza kuuza vocha pia.
  3. Fanye biashara ya kuuza vocha kwani zinabebeka na unaweza kuifanyia popote. Muhimu ni wateja wako kufahamu kwamba wewe ni muuza vocha.
  Biashara hizi zote ukipata watu wa kushirikiana nao katika kununua mzigo itakupunguzia gharama mbalimbali na kuokoa muda wako. Pia kama unaweza kupata wateja maalum wa kuwauzia bidhaa hizi na nyinginezo kutaokoa muda wako na itakusaidia kukokotoa faida kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kujifunza juu ya ukuaji wa biashara ya soko lako.
  Mi niishie hapo. Ila nawaomba wana JF wengine muendelee kumpa ushauri huyu mwenzetu. Asante sana
   
 12. B

  Black African Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru wote bado naendelea kupokea ushauri wenu.
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  uza MAJI.
  Hayana longo longo.watu huwa hawabishi ktk biashara ya maji.mtaji mkubwa ni USAFI wa maji yako.
   
 14. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  I wish you all the best, kwani wadau wengi wamekupa mawazo mazuri mahali pa kuanzia biashara ni imani uliyonayo wewe moyoni kwako. Jitahidi penye nia pana njia
   
 15. `Detective

  `Detective New Member

  #15
  Oct 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Inawezekana mawazo yenu yakawa sahihi, ila muuliza swali anataka biashara ambayo haitaathiri masomo yake. Yaani ambayo you will earn higher for just few hours
   
 16. A

  Arkad Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Habari nzuri.
  Kama haya uliyoyasema yana ukweli 100% Nimejitolea kukugharamia kidato cha 6 au kukuongezea mtaji ufanye biashara itakayohusisha mtaji mkubwa zaidi , mara baada ya kuhakikisha mimi binafsi kwa kina hayo uliyoyasema ni ya kweli. Nitaamua moja ktk hayo niliyosema.

  Kama huna kipingamizi tuwasiliane. Shule njema..Soma kwa bidii kama unasomea kijiji vile.
  Arkad arkad690@yahoo.co.uk
   
Loading...