Natafuta wazazi wa hiyari

Maliselo

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
233
30
Wazazi wangu walifariki kipindi kitefu kilichopita, kutokana na changamoto za maisha ya kila siku kuna kipindi nahitaji mawazo ya wakubwa na kufarijiwa kama mtoto kwa wazazi.

Naishi kwa kujitegemea mwenyewe tangu pindi pale 2007 nilipompoteza mama yangu kipenzi , na kubaki yatima, Mungu wangu ndiye aliyekua kimbilio langu, mawazo yenye hekima na kufariji ni muhimu katika maisha.

Naitwa Peter nina miaka 28 kazi askari, elimu form six , dady and mom nawakaribisha katika maisha yangu.
 
Pole sana kaka
Mungu akupe nguvu na ujasiri
Tutakuwa nawe pamoja
Samahan kwani ndugu hauna hata kina baba wadogo
Km unao jitahidi upendane nao na washirikishe mambo yako ni muhimu sana watakusaidia hata kwenye mambo ya ndoa na mengineyo
Usiwapoteze kabisa ndugu
Wekeni mambo sawa
 
Pole Mkuu.. Mungu akutangulie..Leo nimejifunza kitu kutoka kwako, kumbe hata maaskari mnamahitaji ya kihisia Kama binadamu wengine.
 
Pole sana kwa masaibu.
Ina maana hauna ndugu za wazazi wako? Majirani watu wazima ama huko kazini? Mimi siamini kwenye haya mambo ya mazazi wa hiari mnakutana mtandaoni, siku chache tu mnatibuana. Hapo kazini, na nyumbani treat kila mtu kama mzazi ama kaka na dada yako. Wasalimie kwa heshima, wasaidie inapobidi na uwaonyeshe kujali. Vitu vidogo tu kama kuuliza jana ulipoenda hospitali ulipata matibabu? Unaendeleaje? Utapata upendo wa ukweli kutoka kwa watu waliokuzunguka. Usiwasahau pia ndugu zako, wajomba, baba wadogo na mama wadogo. Wakumbuke kwa zawadi na kuwajali. Utapendwa hadi ushangae.
 
Nashukuru sana kwa mawazo yenu mazuri yaliyonifariji pia na kunipa fundsho zuri , nlikua pia nina maana kubwa kuandika hvyo , ndugu wapo bahat mbaya wapo kijijini sana hakuna mawwasiliano ya haraka pindi ninapohitaji ushauri au msaada wowote , yamkini pia hawana ushauri kama wazazi , nilifarakana na ndugu wengi pale wwalipofuja mali za wazazi wangu katikna mirathi na kuniacha sina kitu , nkahangaika mpaka hapa nilipofika , ndugu niliowwaona ni marafiki tu, katika ukuaji wangu
 
Pole Mkuu.. Mungu akutangulie..Leo nimejifunza kitu kutoka kwako, kumbe hata maaskari mnamahitaji ya kihisia Kama binadamu wengine.
Pole Mkuu.. Mungu akutangulie..Leo nimejifunza kitu kutoka kwako, kumbe hata maaskari mnamahitaji ya kihisia Kama binadamu wengine.







Askari ni wajibu katika kazi kama muhasibu au doctor, lakini sote ni binadamu
 
Pole sana kwa hisia ulizonazo.
Kwanza hongera kwa hapo ulipofika, Baba au Mama wa hiari huja automatic kwa jinsi unavyoishi na watu. Ni jinsi watu wanavyokuona ukitenda katika shughuli zako za kila siku. Hayo yaliyotokea nyuma hutakiwi kuyakumbuka tena kwani umeonesha hayapo tena, cha kufanya ni kusamehe na kuanza maisha mapya. Jitume kwa nguvu zako na akili zako kutengeneza future yako na familia yako tarajiwa, tenda jema au likupasalo kutenda bila kumuonea mtu. Utajipatia ndugu wengi sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom