Kusema kweli sikuuliza ndani sana itakuwaje ila nnavyolewa ukinunua eka nyingi kama 20 kuendelea wanaweza punguza bei. Kwa vile yalikuwepo yaliyojirani na barabara yanauzwa tulichukua hayo ingawa awamu ya pili nitaingia ndani zaidi. Umbali toka barabarani haizidi mita 1000 ni kama dakika 20 kwa kutembea. Pia tulitaka ukaribu na barabara na shule/kijiji ili huduma kama bomba la maji visiwe mbali sana. Ukiwa interested nitakupa namba ya mtu aliyehamia pale kabisa ndio ana taarifa zote kwa usahihi.Inamaana nikiingia ndani zaidi naweza kupata kwa bei nafuu zaidi?
Hapo ulipo wewe umbali gani kutoka barabara kubwa?
Asante sana kwa hizi taarifa kumbe kuna usafiri wa moja kwa moja kwa upande wa Morogoro, sisi tulitumia gari binafsi tukitokea Mwenge. Basi route hii itatufaa foleni ikihamishiwa Bagamoyo rd. Shukrani kwa infoKuhusu usafiri hauna haja ya kupitia Bagamoyo kwa sababu itakulazimu ulipe nauli kubwa na hata unaweza ukaunga mabasi...Kama uko Dar nenda Ubungo pale stand ya vidala dala kwenye njia ya kutokea kule yanakosimama magari ya msasani na mwananyamala pembeni yake utayaona magari ya UBUNGO/MBEZI-MSATA yanapakia..Nauli ni sh 4500/- mpaka hapo Mazizi
Kusema kweli sikuuliza ndani sana itakuwaje ila nnavyolewa ukinunua eka nyingi kama 20 kuendelea wanaweza punguza bei. Kwa vile yalikuwepo yaliyojirani na barabara yanauzwa tulichukua hayo ingawa awamu ya pili nitaingia ndani zaidi. Umbali toka barabarani haizidi mita 1000 ni kama dakika 20 kwa kutembea. Pia tulitaka ukaribu na barabara na shule/kijiji ili huduma kama bomba la maji visiwe mbali sana. Ukiwa interested nitakupa namba ya mtu aliyehamia pale kabisa ndio ana taarifa zote kwa usahihi.
nitaku pmNaomba nirushie kwa private , Thanks
Mkuu nimefuatilia hii kitu imenistusha sana aiseee
Hekari moja ya ardhi inaweza kulisha ng'ombe zaidi ya 500 wa maziwa kila siku kwa mwaka mzima(non stop daily).
Nimeshangaa sana aisee,hii technology imeshafika mpaka Kenya na wako tayari kuoa training kwa mtu yeyote kwa gharama ya Ksh 1500 around Tsh 30,000 na wako tayari kukupeleka mpaka site ukafanya kwa vitendo.
Ni teknolojia simplena nafuu sana hasa kwenye maeneo ya maji na uhaba wa ardhi aisee
Bado nafuatilia, nimejaribu kuwasiliana nao kwa email nafikiri watanijibu soon, ili nipate details nyingi zaidi
Ila naona hii kitu inawezekana sana hasa hapa Bongo.
Nikipata details zote na training yao ntamwaga hapa jamvini data zote ili kila mtu afaidike
Shukrani sana kwa moyo wako mkuu hasa kwa kunipigisha hatua katika ndoto yangu ya kumiliki kiwanda cha maziwa soon.
Sorry namaanisha eka moja inauzwa kwa laki mbili na nusu hadi laki laki tatu kutegemea na umbali na shamba pia
Ni watu binafsi, huku kijiji kiliwagawia hawa wazee na wao njaa wanauza, ila ukiwa na hela nusu unaweza toa ukamalizia mwezi ufuatao ili usipitishe muda mliopangiana watauza na itakuwa hasara kwako vinginevyo kusanya hadi zitimie njoo ushike. Kuna mdau amesema miono kuna mashamba ya kugawiana na kijiji ila mimi sikujui kwakweli.#Mama Joe nilikuwa nahitaji kufahamu kama haya maenei yanauzwa na kijiji au na mtu binafsi.. pia kama wanakubali kuliowa kwa installment!?
Asante
Ukitaka ndani zaidi nenda MIONO, HEKARI MOJA NI LAKI MOJA ADI LAKI NA ISHIRINI,LAKINI KWA KUUZIWA NA SERIKALI YA KIJIJI NI ELFU 1O KWA HEKARI MOJA,THEN UNAFWATA SHERIA ZA KUPIMA MWENYEWE NA KUTAFTA HATI YA ENEO LAKO...KIZURI KULA NA NDUGU ZAKO WATANZANIA.
Habari yako mama Joe kwa kweli nimevutiwa na hili nami nahitaji Shamba niweze kuanza kulima naomba ushirikiano wako ili niweze kupata na Mimi maeneo hayo Shamba tafadhali naomba tuwasiliane ili niweze kujua lini utakuwa na safari za huko ili tuongozane tafadhali. My telephone no. 0756600311
Ukitaka ndani zaidi nenda MIONO, HEKARI MOJA NI LAKI MOJA ADI LAKI NA ISHIRINI,LAKINI KWA KUUZIWA NA SERIKALI YA KIJIJI NI ELFU 1O KWA HEKARI MOJA,THEN UNAFWATA SHERIA ZA KUPIMA MWENYEWE NA KUTAFTA HATI YA ENEO LAKO...KIZURI KULA NA NDUGU ZAKO WATANZANIA.
Ni watu binafsi, huku kijiji kiliwagawia hawa wazee na wao njaa wanauza, ila ukiwa na hela nusu unaweza toa ukamalizia mwezi ufuatao ili usipitishe muda mliopangiana watauza na itakuwa hasara kwako vinginevyo kusanya hadi zitimie njoo ushike. Kuna mdau amesema miono kuna mashamba ya kugawiana na kijiji ila mimi sikujui kwakweli.
Unaweza kufika Miono bila ya shida sana, nenda Ubungo, stand ya daladala za Mwananyamala na mbezi/kimara au ile stand ya pale Ubungo maji, uliza gari za Miono. Nauli ni kati ya Tsh 5000/ mpaka 7000/.
Haya kwa ufupi, Miono iko njia ya Tanga, wilaya ya Bagamoyo. Ukishapita Msata inakuja Mizani ya Magufuli, inafuata Mandela kisha Miono.Toka Msata mpaka Miono kwa daladala ni Tsh 2000/. Na mahindi yanamea sana mitaa ya Miono.
Karibuni sana mitaa ya huku. Na jana na leo mvua imenyesha sana, kijijini kwetu Madesa imeharibu miti na nyumba. Ila Wamasai wapo wengi mitaa hii na mifugo yao.
Asante Malila una contact za mtu hapo Madesa? Hao wafugaji vipi sio wasumbufu? Eka moja inauzwaje? Leo nimetembelea wenzangu wa Kiwangwa eka inafika 1.2ml sio muda ardhi itakuwa haishikiki.
Madesa mimi ni mwanakijiji, nipo kitongoji cha shuleni Madesa. Je unataka kiwanja au shamba. Hapa Madesa wafugaji wako mbali kidogo, kijiji chetu kinapakana na eneo la chuo cha IFM.
Nikupe contacts za dada yangu wa pale Madesa akusaidie? Huyu hata Miono ana ndugu yake wa kuaminika. Kazi ni kwako.
Mkuu bei za maeneo zinaendaje huko madesa karibu na hilo eneo la IFM?
Nitashukuru kupata contacts za mtu anayeuza maeneo huko
Natanguliza shukurani
Kuzunguka eneo la IFM kuna barabara tatu kubwa. Barabara ya Tanga, pembeni kote kumejaa, labda umng`oe mtu, hapo andaa kama 5m kwenda juu ili upate barabarani, line ya nyuma ni chuo. Barabara ya Bagamoyo kuanzia Msata mpaka Kiwangwa imejaa kabisa, ila waweza kumng`oa mtu, opposite na chuo kabisa eka moja line ya pili inacheza 2m kwenda juu. Line ya kwanza mafisadi walishagawana zamani.
Kuna barabara ya upande wa Machweo, inaingia Madesa na Mkoko, kwa mara ya mwisho eka iliuzwa 1m ya usoni na chuo, line ya pili ilitembea kwa laki tano. Upande wa nyuma wa chuo, huko hata laki tano unapata eka moja, shida miundo mbinu kama maji na umeme. Mashamba yaliyo nje ya eneo la chuo tunanunua kwa laki tatu.
Njia ya Bagamoyo, maji na umeme wameweka, njia ya Madesa maji yapo bado umeme.
Kama unaweza kwa bei hizi sema nikupe simu ya katibu wa kamati ya ardhi ya kijiji. Wakati wa kununua kamati nzima inafika shamba na unazunguka nao, kila mmoja analipwa 30,000/ kisha kwa pamoja wanasaini. VEO anapelekewa document na ten percent. Hakuna longo longo.