Natafuta Mwekezaji katika biashara yangu

Wenzako wanapambana kutafuta dhamana, na baadaye kwenda kuitumia hiyo dhamana (mfano nyumba kupata mkopo wa benki) kwa ajili ya kuongezea mtaji.

Hii njia unayotaka kuitumia kupata mtaji siyo rahisi kihivyo kwa sisi watu wenye ngozi nyeusi. Maana kiwango chetu cha uaminifu kiko chini sana.
 
Kinachomata mda ambao utatumia kupata bank zote hizo nilizoziorodhesha, location nzuri ya biashara na mtu mwenye experience sio unatapeliwa mtaji mzima
Yaani kwa hii statement pekee inaonyesha utakuja kuzingua huko mbele. Maana una point ya kujidai ambayo ni kwamba muda uliotumia kupata bank zote hizo. Me nakushauri ingia benki ukakope kwa jina lako.
 
zakuambiwa changanya na zako ikitokea yani mtaji utaopata, wazee wa kazi majambazi wamekuja wameondoka nao vipi inakuaje hapo? biashara inakua imeisha au tutaweka mlinzi, tutakata na bima au, lakiini una dhamana gani wewe? au ndio huo mlango tu huna hata nyumba, kiwanja jieleze vizuri ndugu usitafute mwekezaji kihuni, kweli jamani line za mpesa ziwe dhamana hii nchi uhuru umepita mipaka kweli yani line tu ndio dhamana, mi nadhani IFIKE WAKATI KUTAFUTA MWEKEZAJI KWA NAMNA HII IWE KOSA LA JINAI.
Mkuu bora na wewe umeona, yaani yeye ana frame tu na registration za hizo kampuni anazozifanyia uwakala, alafu anataka investor kwa kigezo cha mashahidi sjui na mwanasheria. Haya ni maajabu, haha
 
Huo muda wa mtu kuwekeza milioni 10 kwenye uwakala anaona ni bora aanzishe biashara mwenyewe aajiri mtu awe boss wake.

Badala yake onyesha kwanini akutafute wewe ukiwa na sababu za msingi. Jambo la kwanza mtu anatazama return ya hela yake, sio aweke milioni 10 uwe unampa laki tatu kwa mwezi hapo risk inayokuwa involved ni kubwa kuliko return inayotegemewa.

Ulipo una usajiri na uzoefu, vipi una kitu chochote cha kuweka rehani kisheria wakati mkataba unaanza in case hela zake ukazipoteza? Hii itakupa jitihada hela uzitumie kiusahihi na kumpa confidence kuwekeza. Otherwise itokee bahati mtu ajilipue.

Kama huna ni bora utafute investor mnayejuana, sidhani kama ukoo wenu wote na wajomba na baba zako wote wauza yeboyebo. Hapo kama ulikuwa kibaka utotoni shauri yako
 
Wenzako wanapambana kutafuta dhamana, na baadaye kwenda kuitumia hiyo dhamana (mfano nyumba kupata mkopo wa benki) kwa ajili ya kuongezea mtaji.

Hii njia unayotaka kuitumia kupata mtaji siyo rahisi kihivyo kwa sisi watu wenye ngozi nyeusi. Maana kiwango chetu cha uaminifu kiko chini sana.
Mtaani mambo hayapo hivyo. Kuna watu wanakopesha na wanakopesheka sana kutokana na trust tu na background zao. Ila humu mtandaoni sidhani.

Alafu sio kila mtu anazo hizo nyumba za kukopea. Nyumba ujenge milioni 20 kwa kudunduliza benki ije iseme thamani ni milioni 7 ndio ikukopeshe utafika lini.
 
Huo muda wa mtu kuwekeza milioni 10 kwenye uwakala anaona ni bora aanzishe biashara mwenyewe aajiri mtu awe boss wake.

Badala yake onyesha kwanini akutafute wewe ukiwa na sababu za msingi. Jambo la kwanza mtu anatazama return ya hela yake, sio aweke milioni 10 uwe unampa laki tatu kwa mwezi hapo risk inayokuwa involved ni kubwa kuliko return inayotegemewa.

Ulipo una usajiri na uzoefu, vipi una kitu chochote cha kuweka rehani kisheria wakati mkataba unaanza in case hela zake ukazipoteza? Hii itakupa jitihada hela uzitumie kiusahihi na kumpa confidence kuwekeza. Otherwise itokee bahati mtu ajilipue.

Kama huna ni bora utafute investor mnayejuana, sidhani kama ukoo wenu wote na wajomba na baba zako wote wauza yeboyebo. Hapo kama ulikuwa kibaka utotoni shauri yako
Kama ulikuwa kibaka utotoni ...
 
Siku unaamua kutoa Mtaji wako, unauchukua kama ulivyo haipungui hata senti moja kwasababu hii sio biashara ya kununua bidhaa.
Na wewe siku ukisema haunihitaji tena (yaani baada ya miezi mitatu) inakuwaje ?

Pili kama una line ambazo hazipo kwenye makubaliano unazitumia kuzalisha na zile ambazo nazijua ndio unatumia hence kunipa bakshishi ndogo ?

Sisemi kwamba wazo ni baya..., Ni zuri sana sababu hata ukimpa mtu faida ya elfu kumi kama isingepatikana pengine hio ni bora kuliko vinginevyo (5 percent of something is better than 100 percent of nothing) LAKINI ninaonyesha tu loopholes za kuweza kumzunguka mdau.....
 
Back
Top Bottom