Natafuta mwanamke wa kuzaa naye.

Jamesh

Member
Jul 15, 2008
31
2
Tangu nikiwa na umri wa miaka 25 nilitamani kuwa na mwenza lakini kwa bahati mbaya sijajaliwa kumpata ambaye naona tunaweza kuanzisha familia pamoja. Naomba nieleweke kuwa I'm not so selective au sio kila mwanamke hafai au sio mwaminifu katika mahusiano ila mimi kwa bahati mbaya sijajaliwa kumpata wa ubavu wangu, kwani kila nimpataye tunakosa chemistry kabisa huku naona uzee unazidi kupiga hodi. Wakati nasubiri kujaaliwa kupata mchumba nimeamua kutafuta mwanamke nitakayepata nae mtoto tu (kuzaa naye) ili kwa pamoja tuwe na mtoto wetu.

Nina umri wa miaka 32, urefu 180cm na uzito 84kg. Mweusi, nimeajiriwa, kipato cha wastani, nina umbo la wastani na dini yangu ni mkristu. Ninajiheshimu na kuheshimu wengine na tabia ni ya kuridhisha. Ninaishi Arusha maeneo ya Makao mapya. Mwanamke awe mwenye tabia njema ili mtoto aweze kujifunza mazuri kutoka kwa wazazi. Umri wake usiwe zaidi ya miaka 45. Awe anajishughulisha ili asiwe tegemezi kwa asilimia 100 kwani gharama za matunzo ya mtoto tutasaidiana kwa kadiri ya uwezo na tutakavyokubaliana. Awe tayari tukapime afya zetu kabla ya kuanza mchakato pia kupima DNA baada ya mtoto kuzaliwa. Sibagui dini, rangi, elimu, umbile wala kabila.

Kwa mwanamke mwenye hitaji kama langu ambaye yupo serious aniandikie email john.joseph843@gmail.com

You are warmly welcome.
 
wow,kwa nini usizidishe bidii ya kutafuta huo ubavu wako unataka wa kuzaa nae tu??kama ni ngumu kupata mke,unafikiri itakuwa rahisi kupata wa kuzaa nae tu??? something might be wrong with your attitude......tueleze zaidi,yaani uko tayari kuzaa na mtu usiyekuwa na chemistry nae,strange!!! anyway,just thinking loud....Kila la kheri Jamesh!!
 
Hivi katika mazingira tunayoishi kumbe huwa ni ngumu kupata wachumba.
 
7.jpg

UTAWEZA?
 
Hizo bold za red especial za chini zimenichekesha sana anyway nakutakia kila la kheri maana single ladies watakuwa wana note books zao wanaandka details tayari kwa kufanya upembuzi yakinifu.....
 
wow,kwa nini usizidishe bidii ya kutafuta huo ubavu wako unataka wa kuzaa nae tu??kama ni ngumu kupata mke,unafikiri itakuwa rahisi kupata wa kuzaa nae tu??? something might be wrong with your attitude......tueleze zaidi,yaani uko tayari kuzaa na mtu usiyekuwa na chemistry nae,strange!!! anyway,just thinking loud....Kila la kheri Jamesh!!

Asante bibie,

Nimeamua nijaribu kwa hitaji hili labda nitabahatika. Hapo hapahitaji chemistry kwani hakuna mapenzi ya moyoni. Mapenzi yanakuwa kwa mtoto tu labda baadaye itokee kuwa mmekuwa na chemistry na kupendana kwa dhati.
 
kaah! Wewe kweli mkristo? Unafahamu maana ya kuwa au kujiita mkristo? Tafadhali piga magoti, umuombe mungu akupe mke halafu umuombe akupathe watoto
 
kaah! Wewe kweli mkristo? Unafahamu maana ya kuwa au kujiita mkristo? Tafadhali piga magoti, umuombe (M)mungu akupe mke halafu umuombe akupathe watoto

Ndio nafahamu na bado napiga goti kumuomba. Maombi kwa Mungu yanaweza yakajibiwa haraka sana au baada ya milongo kadhaa kwa hiyo bado sijakata tamaa kwa hilo.
 
Asante bibie,

Nimeamua nijaribu kwa hitaji hili labda nitabahatika. Hapo hapahitaji chemistry kwani hakuna mapenzi ya moyoni. Mapenzi yanakuwa kwa mtoto tu labda baadaye itokee kuwa mmekuwa na chemistry na kupendana kwa dhati.

mimi najiamini tutakuwa na chemistry na tutakuwa na watoto na tutawapenda sana.....ila nataka uondoe kwanza hiyo attitude ya kuwa umekosa mwenye chemistry na wewe na sasa wataka kuwa tu na mtoto,nafikiri una tatizo hilo.....!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom