Natafuta mtu wa kunishika mkono

Natafuta mtu wa kunishika mkono

imekaa kimkakati sana kwakua ni ke bas Kuna msaada utaupata ila ungekua Me bado ngoma ingekua ngum sana
 
Kwa vile ni demu watu watakusaidia ,ila ungekuwa dume wangekuambia urudi Kijijin ukalime
 
Tafadhali saidia wengine Kama upo kwenye mazingira ya kumsaidia mtu.
Wewe unaweza ukawa Ni daraja la mtu fulani kufanikiwa. Yawezekana kwake ikawa mlima Ila kwako Ni mteremko.

Think of this,
How does it feel when there is someone out there standing on his feet because of the support you gave him.

Natafuta mtu wa kunishika mkono katika safari yangu ya kujitafutia kipato, nitakuheshimu, utakuwa na nafasi kubwa sana katika maisha yangu. Utakuwa baba ama mama ama Kaka katika maisha yangu.

Please nilelekeze tu kwamba fanya ABC , nitajituma kadri niwezavyo , nitafuata njia utakazonielekeza ili mradi tu iwe njia ya halali ili niweze kujiingizia kipato. Hapa nilipo Nina 200K tu nliyobaki nayo. Mimi Ni KE, Ninapatikana Dar, kinondoni. Nimesoma Bachelor of Science in Agricultural Economics and Agribusiness. Nimefanya internship kwa miaka mitatu kwenye taasisi tofautitofauti.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Namba yangu ya simu 0713237228.
Please call me Kama imekugusa.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Struggle is real utapata wa kukushika mkono
 
Please Kama , unadhani Kuna utapeli hapa, Kama unadhani Kuna janja janja ya aina yeyote , Sina nia hiyo, nimeweka namba kwa sababu PM zimefungwa sikuhizi na moderators, email yangu siwezi weka kwa sababu Ina majina yangu mawili halisi , na Ni njia rahisi ya kufikiwa.

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Kwanin moderator wamefunga pm zako
 
Nimekumbuka Uzi wako ulioomba ushauri kuwa uwaambie rafiki zako kuwa umepoteza kazi.

Na ukawe ushuhuda mahali hapa kwa kuwa unalopita nalo wewe tayari ni mshindi.
 
Habari chukua hii business idea kupitia hiyo 200k uliyonayo

Kanunue ulezi 5kg = 10000

Mchele 2kg = 6000

Karanga 1.5 = 8000

Mahindi 2.5 kg = 5000

Mbegu za maboga 1kg = 4000

Ukishavipa vyote vitayalishe kwa kuviosha vizuri na uvianike, karanga na mbegu za maboga zikaange vikishakauka vizuri kavisage.

Kusaga = 2000

Jiko la mkaa =10000

Mkaa = 5000

Sukari 2kg = 4000

Blueband = 8000 ile kubwa

Chupa za chai zile kubwa 3 karikoo= 60000

Vikombe vya robo lita 20 = 10000

Sufuria kubwa 1= 25000 kariakoo

Pilipili manga = 5000

Total 157500

Pika uji kwakuwa unapatikana kinondoni uza kinondoni studio mpaka mkwajuni kila siku jioni

Kikombe kimoja uza 500

Kwa siku ukitengeneza vikombe 60 vya uji utakuwa unapata 30000

Ni biashara ambayo inafaida sana uji wako ukizoeleka unaajiri ata na wadada wenzio

Ukiifanya hii biashara na mtaji wako ukakatika nitakurudishia pesa yako 200k
 
Back
Top Bottom