Natafuta mtu wa kufuga nae nguruwe

Natafuta mtu wa kufuga nae nguruwe

NAOMBENI MSAADA WA KUFUGA NGURUWE 500. Eneo kubwa kiasi gani NAHITAJI? Mabanda mangapi? Gharama ya chakula na Dawa.

500 Ni Wengi Sana, Unahitaji Eneo Kama Manzese Yote.
 
Kwa sasa nipo kibaha,
nasikia hali ya hewa pwani ni nzur sana kwa kufuga samaki.

Ni kweli, ukishapita Mail moja kama unakwenda Mlandizi, mkono wa kulia kuna jamaa anafuga vizuri na mwingine kaanza pande zile zile. Kama una nauli nenda Kidogo zero kule Ruvu ukajionee ufugaji wa samaki.

Mimi nimeshaanza.
 
Nguruwe ni mzigo...yahitaji moyo...ila mdudu anafaida nyingi...kwanza ni mtamu kinoma...pili anakata makali ya spirit kama vile smirnoff vodka na kufanya uanze ligi upya...na faida nyingine kedekede...anyway wish you good luck
 
500 Ni Wengi Sana, Unahitaji Eneo Kama Manzese Yote.

siyo kweli mkuu! ukikadiria nguruwe mmoja achukue square meter 5, utahitaji 2500sq.m ambayo ni nusu eka. haya ni makadirio ya juu sana. sasa manzese ina nusu eka tu?
 
Drinkers advert.png
Drinkers advert.png
 
NAOMBENI MSAADA WA KUFUGA NGURUWE 500. Eneo kubwa kiasi gani NAHITAJI? Mabanda mangapi? Gharama ya chakula na Dawa.

Uko serios au unaleta utani. Hujawahi kufuga halafu unataka kuanza na nguruwe mia tano!!? Kama uko serious anza na nguruwe wachache tena ikibidi chini ya 50 wakati ukiangalia na changamoto zake ndio uongeze. Ukianza na hao 500 nakuhakikishia utachanganyikwa na ndani ya muda mfupi huo mradi utakushinda.
 
500 Ni Wengi Sana, Unahitaji Eneo Kama Manzese Yote.

Si kweli,nguruwe 500 ni wachache sana.Kiasi kuwa unaweza ukatumia eneo dogo kama nusu heka,kwa kujenga banda kubwa halafu ukakata vyumba ndani yake.mfano mzuri ni Jamaa wapo vikindu ambao Mimi huwa naamini wanaongoza kwa Ufugaji Wa nguruwe
Hawa Jamaa wana nguruwe zaidi ya 3000 na eneo walilotumia kujenga mabanda yao ni kama heka moja
 
Nawewe unafuga mkuu?
 
Back
Top Bottom