Natafuta mbwa

Kabachubya

Member
Oct 6, 2009
87
10
Habari wana JF,
Natafuta mbwa wa kununua, aina ya ROTTWEILER au DOBBERMAN mwenye umri wa miezi 10 hadi mwaka mmoja na miezi mitatu. Awe na card yake inayoonyesha amechomwa chanjo.

Kwa mawasiliano: 0717 123464
 
Kuna jamaa anaitwa Anthony Kakoko ni Askari wa mapikipiki anakaa pale Traffic line karibu na Railways sikumbuki ghorofa wala chumba ila anafanyia central Polisi hao mbwa anaowote unaohitaji.
 
Kuwa makini na hao mbwa wangu wamekula sehemu za plastic za gari na hata kukata mabomba usiku nimeenda kwa dr. nikafikiri wanakichaa akasema niwape mafupa lakini wanamaliza ndani ya nusu saa then wananza kula plastic za gari...unajua dawa gani niwape??
 
nenda pale victoria kituoni kuna jamaa huwa wanauza pale wa kila aina
 
duuh kam kuna mtu ana hizo species plaese aweke contacts zake, natafuta sana hawa mbwa,..hasa presa canario
 
Kuwa makini na hao mbwa wangu wamekula sehemu za plastic za gari na hata kukata mabomba usiku nimeenda kwa dr. nikafikiri wanakichaa akasema niwape mafupa lakini wanamaliza ndani ya nusu saa then wananza kula plastic za gari...unajua dawa gani niwape??
Wangu walikuwa wanatafuna sufuria!!
 
Wangu walikuwa wanatafuna sufuria!!

Ha ha ha! Mzee niko serious mbwa wangu ni noma ni kwa vile nyumbani wanawapenda sana ningemgaia mbwombaji bure NILIWAPATA ARUSHA kama ana mtu anamfahamu amtafutie kwa wazungu wa UN
 
Ha ha ha! Mzee niko serious mbwa wangu ni noma ni kwa vile nyumbani wanawapenda sana ningemgaia mbwombaji bure NILIWAPATA ARUSHA kama ana mtu anamfahamu amtafutie kwa wazungu wa UN

Basi mzee na mbwa hao kwenu sitaki tena niwe shemejio...dadako simuwezi!
 
Basi mzee na mbwa hao kwenu sitaki tena niwe shemejio...dadako simuwezi!

Kwa bahati nzuri sista yuko kwenye boksi ataki kurudi huku. Nampga maua aweke kwenye kaburi la mtaalamu wa hip hop 2PAC
 
Kwa bahati nzuri sista yuko kwenye boksi ataki kurudi huku. Nampga maua aweke kwenye kaburi la mtaalamu wa hip hop 2PAC

Duu ngoja nijipange nimzukie unajua ukiwa na shem best friend huwa poa sana!
 
Habari wana JF,
Natafuta mbwa wa kununua, aina ya ROTTWEILER au DOBBERMAN mwenye umri wa miezi 10 hadi mwaka mmoja na miezi mitatu. Awe na card yake inayoonyesha amechomwa chanjo.

Kwa mawasiliano: 0717 123464
Kwenye hii breed ya Rottweiler a.k.a Butcher dog, jiandae na misosi, na kesi...!
Tulikuwa na hii breed, mbwa wawili wanakula hawa balaa, mmoja peke yake anakula zaidi ya kilo nne 4kg. Kila mmoja alikuwa na kilo nadhani arobani na kitu... (40+kg).

Tuliwahi kuwapeleka mafunzo, jamaa akawarejesha kwanza walikuwa wanamtia hasara na pili waliuwa mbwa mwenzao.

Ila ni mbwa wenye kusifika sana kwa akili zao...!

Nikikumbuka jina a aliyetuuzia nitakuwekea hapa.
 
Kuwa makini na hao mbwa wangu wamekula sehemu za plastic za gari na hata kukata mabomba usiku nimeenda kwa dr. nikafikiri wanakichaa akasema niwape mafupa lakini wanamaliza ndani ya nusu saa then wananza kula plastic za gari...unajua dawa gani niwape??

Inawezekana ni njaa, Rottweiler wanakula sana na wanahitaji mafunzo na mazoezi ya kutosha, hii ya kula plastic ni dalili ya frustration na nakushauri ukimuona Rot ameanza hivi bora tafuta mbinu ya kuachana nae, hawa mbwa wana hasira sana na kuna siku atachanganya hasira zake za njaa na frustration za mtu mgeni machoni pake utapata murder case! Kuwa makini sana.

Mkuu Kabachubya unataka hawa mbwa kwa ajili ya Ulinzi? Mimi ningelikushauri utafute German Shepherd, kwa mazingira ya Bongo wana-adapt vizuri na ni rahisi kuwa-train.
Matatizo ya Rotweiller au Dober wanahitaji proper training ama sivyo wanaweza kuwa killing machine na hawapendi mikonomikono mingi kwa hio nakushauri tafuta G.Shepherd.
 
sasa wewe unayesema aende kihesa una matatizo gani?Iringa kuna mbwa wa aina hiyo unafikiri kule kuna mbwa wa nyama tu.Sina hakika sana na hao mbwa ila nakumbuka zamani kuna sista Kunduchi alikuwa anawachukua wadogo sana Nairobi ila wako very expensive plus transport kaka
 
Inawezekana ni njaa, Rottweiler wanakula sana na wanahitaji mafunzo na mazoezi ya kutosha, hii ya kula plastic ni dalili ya frustration na nakushauri ukimuona Rot ameanza hivi bora tafuta mbinu ya kuachana nae, hawa mbwa wana hasira sana na kuna siku atachanganya hasira zake za njaa na frustration za mtu mgeni machoni pake utapata murder case! Kuwa makini sana.
.

Mkuu nakushukuru kwa ushauri mzuri sana, nawapaga kale kamfuko cha super dog siku 2 wanakamaliza na pia tunawapa mafupa mengi ila wnakula si mchezo. Nitafwata ushauri wako. Thanks.
 
nenda pale victoria kituoni kuna jamaa huwa wanauza pale wa kila aina
kaka wale wa victoria wengi koko, sijawahi ona breed nzuri pale na kama huzijui vizuri aina za mbwa unaweza kuuziwa tu jina! kama uko dar pale shoperz plaza mlangoni huwa wanabandika matangazo ya wanaouza mbwa, ila wengi pale ni germany shepheard...kama alivyokushauri kweli hawa gs ni wazuri sana na wanafundishika kiurahisi kuliko hao rw na dm,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom