Hili tango katika picha linatambulika kwa jina la " Bitter melon" lina virutubisho vingi na dawa ya maradhi mengi ikiwa ni pamoja na kupunguza sukari mwilini , maradhi ya tumbo , ngozi n.k. Tango hili linatumiwa sana na ndugu zetu wa asili ya ki- asia. Mahari ambapo kwa uhakika unaweza pata ni ni mitaaya mkunguni au uhindini jijini Dar es salaam . Maeneo hayo kuna wachuuzi wengi wa kitanzania wanauza mbogamboga au vegetables ambazo sio rahisi kuzikuta ktk masoko ya kawaida. Pia sokoni Kariakoo kwenye jengo la zamani sio lile jengo kubwa. Hapo napo unaweza bahatisha kupata . Ingawaje wauzaji wengi hupendelea kwenda mitaa ya uhindini kwani kuna wateja wengi zaidi.. Bahati mbaya muda hautoshi ningweza kukutafutia mbegu zake ili uwe na constant supply