Natafuta marafiki wa kiroho. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta marafiki wa kiroho.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, May 5, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Nataka niwe karibu na sana na mungu.
  Mimi ni mkristo natafuta marafiki walio okoka,
  watakao nifanya nisiambatane na yale makundi niliyokuwa naongozana nayo.
  Yale ya walevi.
  Nimejaribu kuwaacha, lakini najikuta nimekuwa mpweke sana, kiasi cha kuwapigia simu na kurudi tena kwenye ma jack daniel's, konyagi, barcadi na mijitu mingine ya aina hiyo.
  Asanteni sana.
   
 2. Bon

  Bon Senior Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ongera sana kwa kuokoka. nitafute
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ubarikiwe na bwana ....
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukipata wa kimwili naomba unipigie pande.
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Firstlady, I love your quotation hapo chini kuhusu kitabu cha Malaki. may God bless you.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  heri waliokamili njia zao,
  waendao katika sheria ya BWANA ...Zab 119
   
 7. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Naona hii itakuwa sawa na Mwanafunzi kurushwa madarasa kutoka STD 1 hadi STD 7.
   
 8. T

  Tall JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  haleluuuuuuuuya.
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuuuu!!! anajua katika methali imeandikwa:
  Ajitengae na wenzake, huyo hutafuta matakwa yake binafsi
  \hushindana na kila shauri jema!!

  Buji hebu rudi wafuate wenzako wapo pale rose garden wana-do ze nedful kwenye gordon
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hongera kwa kufunuliwa na bwana!... ila chunga tu shetani asije akakufunika!!!
   
 11. M

  Mpalisya Imbogo Member

  #11
  May 5, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nenda Tanganyika Packers utakuta kanisa kubwa la Glory of Christ pale ndani. Utapata marafiki wengi na utaachana na tabia zote mbaya. nenda hata asubuhi utawakuta wachungaji watakusaidia.
   
 12. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Kanisa lolote linalokiri wokovu wa Bwana na kuzikubali nguvu za Roho wake ingia hapo. Wote waliopo mahali hapo ni ndugu na dada zako na hivyo ni rafiki. Ubarikiwa Buji kwa maamuzi ya busara, ningelikuwa Bongo kwa sasa ningekupa company. pdidy vipi umeiona hii post?
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  kaka usifanye utani kwenye neno la mungu - sidhani kama umeamua kuokoa kweli.
   
 14. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  OOOh Amen. Nitafute mimi namba zangu unazo twende tukaihubiri injili ya bwana kwenye mataifa na yamjue Mungu mwenyeenzi
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Ameen.
   
 16. P

  Preacher JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu kuwaacha, lakini najikuta nimekuwa mpweke sana, kiasi cha kuwapigia simu na kurudi tena kwenye ma jack daniel's, konyagi, barcadi na mijitu mingine ya aina hiyo.

  Heri Mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
  Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha; Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo; Na sheria yake huitafakari mchana na usiku; ................................ZABURI 1: 1-2 . Kama kweli umeamua inabidi uvunje vikao na mabaraza yote ya kilevi.... etc.
  Marafiki tu?? YESU ni Rafiki yako namba moja - yeye hana kigeugeu wala habadiliki - usijisikie mpweke - kuwa na muda wa Kusoma Biblia, anza kuomba na kuombea wengine; anza kumsifu Mungu kwa nyimbo, etc. na anza kuhudhuria vipindi mbali mbali Kanisani - anza kusikiliza Gospel songs kwenye dvd yako kama unayo - anza kusikiliza radios kama WAPO radio na PRAISE Power - eventually Mungu atakupa marafiki wema wenye imani sawa nawewe - na hapa JF naamini wapo wengi tu .... Mungu akubariki sana - karibu kwenye UFALME WA MUNGU
   
 17. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  amen ubarikiwe sana umefanya maamuzi mazuri ambayo utajuta maishani mwako. kuhusu marafiki umefanya jambo la maana kutafuta kwani marafiki si kwalazima ni kwa kuchagua natumaini kama umeokokea kanisa la kiroho simama hapo hapo na utapata marafiki wema watakoendana na imani yako ubarikiwe
   
 18. M

  MathewMssw Member

  #18
  May 6, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Barikiwa na bwana YESU! Pale Dar es Salaam Pentecostal Churh Kinondon karibu na soko la TX huwa kuna Kusifu na kuabudu kila siku ya jumapili ya mwisho wa mwezi. Hubu tembelea siku moja nawe huta kaa usahau uzuri wa bwana!
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  hongera kwa kufunuliwa na kujua umuhimu wa kuongozana watu wanaotii amri za mungu,cha msingi wape taarifa marafiki zako wa zamani,kuwa unaingia ktk mstari wa waamcha mungu,labda utapata kondoo wa kuambatana nao,
  usiwe mlokolowe wa kunyáta ,kwani bwana alisema wanaomuonea haya hapa duniani naye hatowatambua muda ukifika
  amen, and may god guide you in every step u take towards his kingdom
   
 20. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #20
  May 7, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Usimkatishe tamaa wala usimhukumu.Kwa waliookoka ni jambo la kawaida sometimes kuzongwa na mambo ya zamani.Kujazwa Roho wa Bwana mpaka matunda yatokee its a process kama vile ambavyo matunda huwa yanapandwa mpka kukomaa.Buji2 umefanya sahihi.endelea mbele na ongeza bidii utashinda
   
Loading...