Kuwa nawanamke zaidi ya mmoja ni baraka, wapuuzeni wanafiki

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Salam sana wana Jf na wasio fungamana na upande wowote kwa imani zenu tofauti tofauti.

Ndugu na waandikia , katika pilika pilika zangu za kimaisha kwenye ulimwengu wa mahusiano na uchumba sugu mimi kama kijana nilikua natesawa na kunyanyaswa sana kijinsia, kingono, kiakili, kiroho na hata kutapeliwa kiuchumi na hawa wanawake niliokua nao tofauti tofauti kwa msimamo wa kua na mwanamke mmoja mmoja.

Ndugu zangu nilikua sina hata pakuchepukia na wala akili ya kutafuta michepuko nilikua sina na hapo hata kunywa pombe kali nilikua sijui bado na ninaona ni anasa tuu za ulimwengu.

Hakika nilikua na nyimwa tendo na mwanamke pasipo kujua sababu ni nini, pesa na toa , huduma zote na toa mpaka huko kwao kwa wazazi wake na ndugu zake, kweli nilikua napitia kipindi kigumu cha kua na mwanamke mmoja.

Uvumilivu wa kujitesa nafsi nilikua nikipitia sana huku nikijiaminisha huyu ni fungu langu na mwisho wa siku najikuta nimeachwa solemba , napitia mateso ya upweke kumuwaza na kumbembeleza arudi lakini wapi.

Ndugu nilikua kama nimelogwa maana nilikua siwazi hata kutongoza upya mwanamke mwingine wa kunipa kitu roho inapenda , nakumbuka pole pole nikaanza kujiingiza kulewa na kujiover dose vile vidonge vya priton ili niweze kulala.

Nakumbuka sana nilikua na chukua priton vidonge vitatu na visaga vinakua unga naweka kwenye redbooll alafu na changanya na bia napiga naona kama vile nipo peponi ulimwengu mwingine

Zoezi langu lilikua linaendelea hivyo hivyo pasi na kujua kulikua na mwanamke (bi-dada) yale maeneo ananitizama sana kila nikifika nilikua na kutana naye sina time nae hatujuani ni mimi naendelea na michanganyo yangu kama kawaida kumbe yeye anafatilia ninachofanya kimnya kimnya.

Ndugu , siku moja nachanganya vilevi vyangu kuondoa stress za mapenzi gafla na shangaa huyo mwanamke chapu kanifata na akakaa kwenye meza yangu ( moyoni na jisemea hawa ni nyoka ni wale wale, shetani kaja karibu yangu alafu busy naendelea changanya ananiangalia jwa huruma alafu na kunywa) .

Aliniomba samahani na kuniuliza jina sikutaka kumwambia nilikua mkali sana ila alitulia na baadae akaelezea jinsi anavyo niona napiga michanganyiko yangu aliniambia maneno magumu sana

Maneno yake yalikua hivi:-_

" kaka kwanini unajiua kwa mateso na wewe bado ni kijana unaonekana uko vizuri tuu, kwa nini umechagua kufa kwa mateso kiasi hiki".

Nilibisha na nae ila upande mwingine yaliniingia sana na sijui kwanini alisema hivyo , basi akawa anajiongelesha na msililiza tuu sijibu chochote na baadae akaaga akaondoka zake

Kama kawaida yangu na hudhuria pale napiga vitu vyangu , pole pole akaanza kunizoea na nikajikuta na mwambia kinacho nisibu ila siongei sana na mwambia sentensi hii tuu-:

"watu wema wapo wanawake ni nyoka na ni mashetani''

Kama mwanamke akawa anaelewa mwisho wa siku nashangaa ananiambia achana na huyo anaye kutesa moyo wako bila yeye kujua kwamba nilisha achwa kitambo.

*Ndugu huwezi amini alinishauri tafuta mwanamke mwingine tena usitafute mmoja kua na atleast watatu pamoja na marafiki wa kawaida wà kike,

* Alini hasa sana kwa kujitolea mfano yeye akisema yeye ni mwanamke ila kamwe nisijedekeza mwanamke, nisimuonyeshe mwanamke kumpenda, nisimwonyeshe kwangu yupo peke yake na pia kamwe nisimpe mwanamke kila anachokitaka wakati mwingine ni mnyime

*Aliniambia pia mwanamke analinganisha maisha na analinganisha wanaume maana kutwa anatongozwa njiani kila siku hivyo mimi kama mwanaume nisikubali kulinganishwa , niwe sieleweki fomula yangu ili anapolinganisha ashindwe kunilinganisha na wanaume wengine pale wanapokutana kuadisiana mambo yao au kutongozwa tongozwa

* Alinisisitiza pia mwanamke ni hatari muda wowote ila nisiamini mwanamke kabisa maana wana tamaa sana na wana danganyika kirahisi sana

* Mwisho kabisa alisisitiza nisiwe na mwanamke mmoja maana wao wana wivu sana na ni wabinafsi hawapendi kushare, hivyo nikiwa na zaidi ya wawili atakua wanashindana ili nibaki upande wa mmoja wao , na hata kama na shindwa kua na wawili kwenye mahusiano basi niwe na igiza kama wapo wawili au nisiache kua na marafiki wa kike watakao kua wanampa competition moyoni mwake


NDUGU HUYU DADA ALIYASEMA HAYO KWANGU BAADA YA HAPO TULIPOTEZANA KABISA NA SIKUWAHI KUJA KUMUONA TENA.

sasa mawazo na shauri zake nilizifanyia kazi japo nimezidisha sana idadi ya wanawake

Niliyo ya faidi ni haya;-

1: Nime barikiwa sana kiuchumi, nina amani moyoni mwangu na pia ninauwezo mkubwa sana wa kufikiria mbali

2: Pombe nimepunguza na afya yangu imerejea imara sana na mchangamfu mno

3: Hakuna mwanamke anayesumbua akili yangu, mmoja akizingua basi mimi na hamia kwa mwezake aliyetulia na maisha yanaendelea

4: Kupelekeshwa kupo ila na uwezo wakupuuza mpaka naonekana asiye jali chochote kiasi kwamba wananilaumu nachukulia mahusiano ni simple sana

5: Kiroho niko poa sana na ibada narfanya na mambo yangu yanaenda sawa kabisa

6: Nimepata uwezo wa kinganisha nyota na mwanamke na kumtambu mwanamke mwenye nyota safi na mwenye nyota mbaya yenye mikosi na ambao hatutaenda, na hii ni real sana naona wazi wazi na ikitokea mwanamke ana nyota mbaya naona ugumu mambo hayaendi, pesa zinapotea potea mtumizi makubwa yasiyo na maana na MPIGA CHINI

7: Amani, furaha na upendo vimeongezeka sana na sana

8: Wapenzi wangu wote wanajuana na wakati mwingine nawatoa wote out kwa pamoja wanakaa wanazunguka meza basi inakua kama marafiki na kampani kubwa na enjoy maisha

9: Wanawake wangu hawaonyeshi kuchukiana, nawapa zawadi za kufanana na zenye thamani moja, na hela nawapa wakiwa wote pamoja tena na hesabu wakiona na hakuna ninaye mpendelea pembeni hii imenifanya kujiona mwamba na kiongozi zidi yao


10: Mmoja akikosea na waambia wenzake wamweke chini wa mkanye na kweli naona wanambiana basi anatulia, sina muda wa kulumbana nao , busy na tafuta hela na maisha uchumi imara kazi za watu zina kwenda na biashara zinakwenda imara sana


MWANAUME KUA NA MWANAMKE ZAIDI YA MMOJA NI JAMBO LA BARAKA NA LA HERI NA AMANI TELE KIKUBWA TUMIA AKILI , WANAWAKE NI WEMA SANA UKIWA NAO ZAIDI YA MMOJA ,

MIMI NI MKRISTO
 
Nina mpango wa kuwa na wake wawili mtu na mdogo wake.
Kilala heri mkuu, ila mtu na mdogo wake siku shauri ni rahisi kuuana atleast mtu na binamu yake au mwanamke mwingine wa mbali hawa watakua wanaonana wachawi na watakua wanalogana ila kuuana ni ngumu kidogo
 
Back
Top Bottom