Natafuta kazi ya ukalimani Ikulu

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Baada ya Rais wetu kuamua kuitangaza lugha yetu ya Kiswahili na kukataa kuongea kiingereza huko Zimbabwe,

Baada ya waandishi wa habari wa Zimbabwe kushindwa kuongea na kutambua kiswahili,

Baada ya viongozi walioambatana na Rais kushindwa kukalimani hotuba yake kwa waandishi wa habari hivyo kupelekea kukosekana kwa mahojiano/maswali kati ya Rais na Waandishi,

Naomba kazi ya kuambatana na Rais katika ziara zake ndani ya nchi zinazozungumza kiingereza ili niwe mkalimani wake. nipo tayari kufanyiwa usaili.

NB. Na ule mdahalo wa kiingereza pale Namibia kwa asilimia kubwa alikuwa anasoma kwenye karatasi. Ningekuwepo angeuendesha kwa kiswahili ili nifanye kazi ya ukalimani.
 
Kukosekana mkalimani lengo hasa ilikuwa ni kukwepa maswali kwani majibu yake yangezua utata zaidi. Wale waliokuwa na shaka kuhusu uwezo wa jiwe kuongea kiingereza nadhani sasa wameelewa kwa usahihi. Ni fedheha lakini huo ndio ukweli.
 
Mimi naweza kusaidia kwa lugha zifuatazo:

1. Swahili
2. English
3. Portuguese
4. Spanish
Nafasi mbona huwa zinatangazwa Sana Sadc ,African Union,Umoja wa mataifa na mashirika yake,Marekani nk watanzania huwa hawaombi sijui kwa Nini Lakini tatizo hawaitumii mitandao kutafuta fursa wanaitumia kwa vitu vya kijinga.Kuna mahali nilienda mkutano wa kimataifa ambako presenter alikuwa akiongea kifaransa mkalimani akawa mkongo anatafsiri kiswahili Cha kikongo tukawa tunalalamika.Waandaa mkutano wakasema tatizo nafasi za ukalimani za kimataifa zikitangazwa watanzania hamuombi.Na si hizo tu nafasi kibao za kazi hutangazwa hata na umoja wa mataifa hata saa hi zipo ingia website ya umoja wa mataifa ya UN jobs ziko kazi kibao . Lakini watanzania huwa hawaombi wanashindia ujinga mitandaoni.Kwa uwezo wa lugha ulionao hukustahili hata kuwa Tanzania ungekuwa mbali mno.Shame on you
 
Back
Top Bottom