Tatizo lipo wapi kati ya TBC na BAKITA?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Kupitia TBC tulimsikia Mh Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa wadau wa kilimo na chakula.

Katika mkutano huo waliandaa jukwaa kwaajili ya vijana kumuuliza maswali Mh Rais Samia.

Swali langu kama dhumuni la TBC lilikuwa kwaajili ya Watanzania kuelewa kinachoendelea, kwanini waliruhusu itumike lugha ya Kiingereza badala ya Kiswahili, au hamkuwaalika BAKITA kwaajili ya ukalimani?

Nimewahi kusikia viongozi wetu wakisema tukiuze Kiswahili kwasababu imekuwa ni bidhaa duniani, pia tunalalamika kuwa Wakenya wanatuzidi kutafuta vyuo humo duniani kwaajili ya kufundisha.

Namalizia kwa kumpongeza Rais William Ruto wa Kenya kwa kuwafundisha Kiswahili wageni waliohudhuria kwenye mkutano wa kimataifa uliohusu hali ya hewa na tabia nchi huo palepale ukumbini.

Nayeye wiki hii alikuwa anawageni Marais takribani 8 kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye alipata nafasi ya kuwahutubia kwa kusema penye changamoto ndio kuna fursa.
 
Back
Top Bottom