Sitamlaumu Rais kwa kutomudu lugha ya kiingereza lakini najua ni dosari kubwa.
Kwetu sisi Tanzania, official languages (lugha rasmi) ni Swahili na English. English ni lugha rasmi ya nchi yetu lakini pia ni miongoni mwa lugha rasmi za kimataifa. Kiswahili siyo miongoni mwa lugha rasmi za Dunia. Kwa hiyo, hata ndani ya Taifa letu, kwa uzito wake, English ipo juu kuliko Swahili.
1. English ni lugha rasmi ya Taifa. 2 2. 2. English ni lugha ya kufundishia masomo kuanzia ngazi ya sekondari kwenda juu.
3. English ni lugha rasmi ya kimataifa. 4. English ni lugha rasmi ya kisheria ndani ya nchi yetu. Sheria zote hutungwa kwa kiingereza, kisha hutafsiriwa kwa Kiswahili.
Sababu zilizotajwa hapo juu ndizo zinazoifanya English, katika nchi y etu, kuonekana ni lugha ya kitaalam, ni lugha ya wasomi na ni lugha ya teknolojia. Ni sawa na ilivyokuwa wajati wa Yesu Hebrew VS Portuguese.
Kama Rais wetu hamudu English, anamudu lugha gani katika lugha zile za kimataifa? Hata kama mtu una ujuzi wa namna gani, kama huwezi kuwasiliana, ni tatizo.
Tusijilinganishe na Wachina, wao kichina ni miongoni mwa lugha za Kimataifa. Vivyo hivyo kwa Warusi na Wajerumani. Halafu hawa teknolojia yao siyo kama ya kwetu.
Kwetu sisi English ndiyo lugha ya kufundishia masomo. Haitarajiwi yeye aliyesoma kufikia kiwango cha juu asifahamu English japo uhodari wa lugha unaweza kutofautiana miongoni mwetu.
Asante kwa kueleza vema sana.Lakini,nadhani,pamoja na yote hayo,walao huyu hashindwi kumpata mkalimani,tena wa kitanzania na ujumbe wake ukafikia wahusika vema kabisa.Tunao watanzania wazuri sana wa lugha ya kingereza.Hawa wanaweza kuwa wakalimani wazuri tu.Sina hakika sana kama,uchina ambayo miaka hiyo ya nyuma (au hata warusi) kama walizingatia kingereza kwanza hadi walipoendelea kichumi,teknolojia n.k. Kwa hili sina hakika sana.lakini yewezekana kabisa walikomalia lugha zao toka awali.Zaweza kuwa zaongewa na watu wengi,ila ni ndani ya nchi zao zaidi,kwani,China na Urusi hawakuwa na makoloni,labda ujerumani.
Lakini jingine,hebu tuangalie hao viongozi wetu (walao wengi wao kati yao) waliopita ambao kingereza hakikuwa tatizo kabisa kwao,infact wengine walikuwa wajuzi hasa na wasikia raha hata kuwasikiliza wakikiongea kingereza.
Hawa kwa upande wangu,katika vipindi vyao vya uongozi,zaidi ya kuteleza vingereza murua,sioni kama walijua namna,ama kuwa na utashi au walipigania kwa nguvu stahiki maslahi ya nchi au hata kusimamia mambo hadi walao hata hali ya nchi ingebadilika kama ambavyo labda ingewezekana wakati wao.Sisemi hakuna walichofanya,kamwe.Na hakuna kiongozi atakayemaliza kila kitu kwa wakati wake.Lakini,wananchi wanaweza kuona walao,yupi alikazana vya kutosha katika kipindi chake,hata kama tutalalamika kwa namna fulani.Lakini mabovu mengi ambayo yalilazimika kurekebishwa na huyu aliyepo,na ambayo yalikuwa na yamekuwa vikwazo sana kwa mambo mengi ya kimaendeleo na kuwa kero sana kwa wananchi,huyu walao alianza nayo kuyaweka sawa ndipo na mengine yaka/yanafuata.Na yalikuwa mengi kwa kweli na bado yatakuwepo tu,japo yakipungua.
Ndio kusema,mambo mengi ya kuirekebisha nchi na kuiweka sawa,hayakuhitaji sana ujuzi wa lugha ya kingereza.
Asilimia kubwa ya uongozi wa nchi,ni masuala ya ndani ya nchi-Labda mtu akiwa na utegemezi sana wa suluhu za kutoka nje ya nchi.Ndio sababu huko nyuma tulizoea sana kusikia mno kuhusu uchache wa fedha serikalini,malalamiko ya kukosa ufadhili toka nje n.k kutoka viongozi wetu wakati huo.Nadhani ni kwa kuangalia sana suluhu za kutokea nje(ambako lugha ya kingereza,wanaelewana pia).Na sisemi kuwa hakuna kabisa suluhu za kutoka nje ya nchi.Lah!
Ila naunga mkono yote uliyoyasema.Lakini,yupi bora.Kiongozi anayejitahidi kwa lugha hiyo hiyo yenu ya kiswahili au anayejua kutema yai (kuongea kingereza) huku,ama hajui au hajali au hana tu utashi wa kuwawekea mambo ya msingi sawa?
Kujenga barabara,kulipa madeni nje ya nchi,kusafiri nje ya nchi kwa raisi,ni mambo muhimu.Lakini je,yale ya kuleta mapinduzi nchini yalikuwaje?Tunawashukuru kwa yale waliyoweza kufanya.Ila kuna mengi yalimea hadi kuvunda wakati wao licha ya kukijua kingereza kwa ufasaha sana.Sana sana nadhani walikuwa na mwelekeo wa kutazama nje zaidi,huko ambako walikuwa wanaeleweka kilugha ya kingereza.
Nadhani,zaidi ya kuwa na safari nyingi za nje ya nchi na kuongeza gharama za safari,sioni kama vingereza vyao vilitusaidia sana
Ila asante bw.Bams kwa kudadaua vema kabisa.