Natafuta Kazi Usalama Wa taifa

Status
Not open for further replies.
WanajamiiF kazi hizi za usalama wa taifa zipo ila ni kwa nini wewe uone kazi ni usalama wa taifa tu......baba yangu ni mkulima wa mpunga na mahindi na yeye pia ni usalama wa taifa...''he is a national security officer to secure the nation from being affected by famine okey you can judge yourself under any aspect like my father as well as me myself I am a carpenter''....msing'ang'anie kazi huenda Mungu anataka kukuepusha na uuaji...because si wote wanashika peni wengine wanashika bastola kuwaua wema.

kazi kweli kweli mtu anaomba kazi wewe unamtishia
 
duniani kote hawa jamaa wanaitwa intelligence officers bila shaka kama unataka kazi huko ni muhimu kwanza ukajipima how much you are intelligence to fit in there kabla ya kujiua namna ya kupata kazi huko. naamini hawa jamaa wako kila mahali mwaga CV yako hapa JF wanaweza kukuona na kukutafuta
 
napenda kujua wadau jinsi ya kujiunga na usalama wa taifa ......wanaaangalia vigezo gani
 
Huingii huko bali unafuatwa pembeni. Ukiwa unataka kuingia huko motive yako itakuwa questioned - unataka kuingia huko ili iweje? Inawezekana wewe unaona kwamba ni kazi tuu lakini wao wanaweza kuona kwamba motives zako za kuwa usalama wa taifa ni tata, yaani kwa nini unataka uingie huko? Una yako mengine?

In short, kama hujafuatwa mbaka sasa hivi basi changamkia ajira zingine.
 
Hyo kazi mpaka uwe kwenye system ya familia ya kijesh au kimagamba hapo ndo unaweza ukapata kwani uwa wanawaulizia kama una ndugu mlete tumuoji aingie usalama mi kuna jamaa yangu form 4 failure yupo huko sema yeye dingi yake ana cheo jeshini
 
Simple, Nunua kadi ya CCM ilipie ile sh 120 ya mwezi kwa miaka mitatu kuonyesha uko committed halafu kaongee na balozi wako wa nyumba kumi juu ya nia yako. Au ulifikiri kuna kaaaazi! Wala. Cha muhimu tu onesha chuki kwa wapinzani kwa kila jambo, hususan maandamano.
 
Hizi nafasi huwa hazitafutwi kama unavyoulizia kijana.Ni uwanja mpana sana na mpaka hapo ulipofikia umeshapoteza sifa zake yaaani haufai.Labda kwa wale wenye sifa kamili but siyo wewe basi wanaweza kwanza kupitia JKT ,then JWTZ Baada ya hapo watafanyiwa usahili na kama watakuwa fit kwelikweli ndo watakwenda kwenye hayo mafunzo ya usalama wa Taifa.UKIMALIZA Mafunzo utakuwa chini ya uangalizi kwa muda wa 3yrs.THEN utaruhusiwa kufanya kazi ktk taasis mbalimbali za serikali na za watu binafsi.So usikariri kuwa ni kufanya kaz ikulu km wengi wanavyojua.Na wala si member wa ccm wala cdm. MIMI nakushauri wewe tafuta kazi nyingine na huko utaweza kuilinda nchi yako kwa kuwa mzalendo,kwa kukutaa RUSHWA na kujituma zaidi.ONYO usipende fedha za harakaharaka.Harafu usiniulize kuwa mafunzo yao ufanyikia wapi kwani kufanya hivyo utazid kupoteza sifa kabisa.TAKE CARE......
 
Simple, Nunua kadi ya CCM ilipie ile sh 120 ya mwezi kwa miaka mitatu kuonyesha uko committed halafu kaongee na balozi wako wa nyumba kumi juu ya nia yako. Au ulifikiri kuna kaaaazi! Wala. Cha muhimu tu onesha chuki kwa wapinzani kwa kila jambo, hususan maandamano.

Mhhh! umejaliwa sana fix na chuki bila sababu!!! hebu jifikirie upya huyo dogo kakukosea nini na kwa kuomba msaada, pili mbona akina DR slaa ni watu wa usalma wa taifa? mrema inamaana huwajui? na wao leo ndio wanaoongeza mageuzi unayoona sasa.
 
Kazi hiyo haihitaji kufanya application kama hizi tunazofanya na wala usidhani kuna interview kama hii tunayoifanya.Nilikuwa na rafiki yangu wakati tunasoma naye sekondari miaka ya 1980 aliitwa na maafisa toka serikalini kupitia kwa mwalimu mkuu wa sekondari.Wale jamaa waliondoka maye na walimuhoji karibu masaa 5 na hatimaye kumrudisha jioni.Aliporudi nilijitahidi kumuuliza hao jamaa waliokuchukua ni akina nani na walikuwa wanataka nini,yule rafiki yangu alinidanganya kwamba ni kaka yake mkubwa.Baadaye sana kama miaka 12 nilikuja kukutana naye ndipo aka disclose kuwa walikuwa ni watu wa usalama wa taifa walikuwa wanahitaji aingie katka hiyo kazi ila walimuapisha asiseme kabisa kwa mtu hata kwa wazazi wake.Swali kwamba walimjuaje mimi sijui lakini ninadhani hata waalimu katika sekondari wengine wao ni njagu huwa wanaangalia mienendo ya tabia za wanafunzi na kuwa identify kama possible candidates wa usalama wa taifa.Otherwise,sijui kwa sasa wantumia vigezo gani vya kuwapata.
 
Achana na hili mpwa jiandane kuwekeza mchango wa lowassa kuingia madarkani ukale mema ya nchi
 
wewe acha kufikiria mambo ya mwaka 1980 kwani huko tulishatoka ck nyingi na sasa ni mwaka 2011 huu.Narudia kwa mara ya mwisho kwamba kwasasa hv usahili ni lazima ili kupata fit person na kama haitakuwepo basi wangepatikana unfit person na wala kusingekuwa na competion kuingia kwenye IDARA hii.Kumbuka hii ni IDARA kubwa tu na inataratibu zake.
 
Ukiona gamba JK anasoma risala sehemu wafuate mmoja kati ya wale jamaa karibu yake ambao masikioni wameweka vifaa vya mawasiliano.ongea nao fresh watakupa mchongo.
Mi nipo huko lakini nipo na msanii mtoto wa mkulima.ila uwe ni mnafiki haswa,mmbea vilivyo na damu yako ikichanjwa iwe ya kijani sio nyekundu.
 
Ukiona gamba JK anasoma risala sehemu wafuate mmoja kati ya wale jamaa karibu yake ambao masikioni wameweka vifaa vya mawasiliano.ongea nao fresh watakupa mchongo.
Mi nipo huko lakini nipo na msanii mtoto wa mkulima.ila uwe ni mnafiki haswa,mmbea vilivyo na damu yako ikichanjwa iwe ya kijani sio nyekundu.

kwa hyo na wewe ni mbeya na mnafiki sio?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom