Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
Ama unapotosha au hujajua tofauti ya kujibu "sina clue" kwa swali la anuani na "sina clue" ya jinsi ya ku apply.
Nisichokijua hata chembe ni anuani ya kutuma maombi usalama wa taifa, hiyo haimaanishi kuwa sijui hata chembe namna ya kutuma maombi ya kazi usalama wa taifa. Big difference.
Umekosea tena. Unatumia vibaya, au hufahamu maana, ya neno anuani.
Umekosoa aliyeandika na kuleta JF nia yake ya kutafuta kazi Usalama. Maana yake amekosea pa kupeleka maandishi yake - anuani. Waungwana wakaona umeongea habari njema. Wakakuuliza, haya basi, anuani sahihi ni ipi? Ukasema "huna clue." Ukaulizwa, kama "huna clue" anuani sahihi ni ipi utajuaje isiyo sahihi? Ukajichanganya na mifano isiyotofautisha ufundi wa upishi wa pilau na ingredients zinazoenda kwenye pilau.
Ikaonekana majibu na kosoa zako 'zimechanganya viuongo.' Waungwana wakarudi na swali lile lile mara ya pili: Sasa anuani sahihi ya kutuma maandishi kwa Usalama wa Taifa ni ipi?
Wakuu wanasubiri jibu la pili. Tena lenye "mahesabu" yaliyotulia.