Natafuta deal ya pesa nyingi

Natafuta deal ya pesa nyingi

Habari za muda huu wana jf.
Mimi ni kijana mtanzania, jinsia yangu ni mwanaume, elimu yangu ni kidato cha sita, umri wangu ni miaka 27.

Nisingependa kuwachosha sana naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika,

Natafuta kazi au deal yeyote halali au haramu kigezo iwe na kipato au ujira mkubwa, hii nadhani inetokana na kuwahi kumiliki pesa nyingi na zikapotea bila kukamilisha mipango na malengo yangu.

Niliwahi kumiliki pesa nyingi kipindi nipo na miaka 21 hadi 24 na pesa hizo nilitafuta mwenyewe sio kwa kurithi, kudhurumu au kuiba.
Najua wengi mtashangaa na mtanishauri nitumie njia ile ile kupata hizo pesa lakini kwa sasa naona itachikua miaka mingi sana au isiwezekane kabisa.

Njia iliyotumika kupata fedha nyingi,

Niliwahi kusoma chuo cha madini hivyo nina uelewa kiasi kuhusiana na madini especially gold, Wakati nipo chuo mwaka wa pili tulipangiwa field, wakati nipo field nikabahatika kupata dhahabu kiasi ambayo niliiuza na kupata fedha nyingi kwangu, ikapelekea chuo sikumaliza ndio maana nasema nina elimu ya kidato cha sita.

Lakini pia njia hii ilikuwa kama bahati kwa upatikanaji wa fedha hizo ndio maana siwezi kuitumia tena kutafuta pesa nyingi.

Mimi binasfi kutokana na uelewa wangu na kutembea kwangu nimegundua, kazi nyingi haramu au deal nyingi haramu zinaingiza pesa nyingi sana. Ukizingatia pia zina risk kubwa pia ni kama third law of motion ya sir Isack Newton (for every action there is equal and opposite reaction)

Lakini kutokana na kutembea kwangu, akili yangu, skills zangu na efforts zangu nimejiandaa kiakili na kisaikolojia kutafuta deal yeyote ya kuingiza pesa nyingi sana kuanzia sasa.

Najua kuna kusalitiana, kuua au kuuliwa, kukamatwa na kupewa adhabu kali au kuhukumiwa kifungo cha maisha, but am ready with all that maana nimeckoka maisha haya.

NB:
Sio mzuri sana kwenye uandishi lakini nadhani nitakuwa nimeeleweka na kama unaswali au ushauri unakaribishwa
(Nawasilisha)
nanukuu; Natafuta kazi au deal yeyote halali au haramu.

nenda zenji au mombasa kwa maelezo zaidi muone James delicious akakupe muongozo.
 
Unatuambia ulipata dhahabu? Ninavyojua dhahabu sio kama Tanzanite au Rubi au kito cha thamani chochote cha kusema umepata au umeokota. Dhahabu haikotwi. Dhahabu inakuwa extracted kutoka kwenye mwamba au mchanga wenye dhahabu. Dhahabu ni metallic element sio compound.
iko dhahabu ya vipande unakuta mwamba umelala njano tupu, na nyingine inakuwa mbolajjah jiwe linazungukwa na vipande vipande vya dhahabu, so inategemea na mgodi kuna migodi haina vipande lazima ufanye leaching ndo uone dhahabu maana iko kwenye mchanga..
 
Nimeshangaa sana kwa sababu haiwezekani mtu yuko field tu(mazoezi kwa vitendo) ya miezi 2 halafu bin vuu amepata dhahabu kama vile kito cha thamani. Dhahabu inahitaji uwekezaji ili uweze kuchimba na kuextract.
Labda kama alianza kazi zake risk(wizi) siku nyingi. Aseme tu walimuibia mtu dhahabu yake.
pia anaweza kusaga mawe halafu akaosha na mwisho akapata mahomeka akayachukua na kuyakamatisha/pembua kwa mercury anapata dhahabu kama wanavyofanya wachimbaji wadogo..
 
Nimeshangaa sana kwa sababu haiwezekani mtu yuko field tu(mazoezi kwa vitendo) ya miezi 2 halafu bin vuu amepata dhahabu kama vile kito cha thamani. Dhahabu inahitaji uwekezaji ili uweze kuchimba na kuextract.
Labda kama alianza kazi zake risk(wizi) siku nyingi. Aseme tu walimuibia mtu dhahabu yake.
images - 2022-01-11T122442.193.jpeg
images - 2022-01-11T122450.403.jpeg
images - 2022-01-11T122458.369.jpeg

ukigonga gonga hapo na bit ya chorongo unasepa na mzigo..
 
Nimeshangaa sana kwa sababu haiwezekani mtu yuko field tu(mazoezi kwa vitendo) ya miezi 2 halafu bin vuu amepata dhahabu kama vile kito cha thamani. Dhahabu inahitaji uwekezaji ili uweze kuchimba na kuextract.
Labda kama alianza kazi zake risk(wizi) siku nyingi. Aseme tu walimuibia mtu dhahabu yake.
mfano kitunda tabora kule 2017 kulihila dhahabu ya vipande watu walivamia waliokota mpaka mtu mmoja gram 600 wengine 1Kg na ni 99% pure maana kilo ya dhahabu ni kama usawa wa size ya kiberiti au zaidi kidogo...
 
Madili ya kuiba kama unayosema hayo ni ya kishamba na yaliyopitwa na wakati..ya nini kusumbuka na mabunduki kwani uko vitani ?

Hivi unaijua msoga cartel, unaonaje upigaji wao wa madili, very simple, hakuna stress, mikataba tu inacheza, madili makubwa ya maproject ya nchi, unaingia na wazungu huko, kupiga bilioni 1 au 2 kawaida sana, hizo ndio dili..ishu namna ya kujiunga na mtandao huo..

Tatizo connection mkuu
 
Kwanini usiingie kwenye kilimo cha matikiti.Ukipiga hekar zako hata mbili unakuwa milionea kwa miezi mitatu tu.

tikiti moja ukiuza 3k tufanye umepata matikiti 2k
ukipga 2000×3000=6000000 ( milion 6 )

hapo ukitoa gharama za kukod shamba na madawa ni kama 1m tu utajikuta una baki na 5m

Haya ukilima misimu miwili unajikuta una 10m

nb.Hili ni dili haramu na halali ko jitose kamanda huku [emoji23][emoji23].
[emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23]dah kilimo cha kwny daftar kinalipa Sana!!
 
Watanzania sisi tunalaumu tu na kukosoa badala ya kushauri... Mkuu kwa uelewa wangu ..katika kila jambo kuna cha kujifunza unaweza ukapata dili haramu na ikakupelekea ukajifunza na kuachana na dili hizo haramu .. wasikutishe tishe maana wasiwasi ni ugonjwa mkubwa sana kuliko hayo maukimwi.. fanya maamuzi mkuu
Nimekupenda sana mkuu

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom