Natafuta Dawa ya Panya

Zamazamani

JF-Expert Member
Jun 13, 2008
1,865
782
Wakuu nahitaji dawa effective ya kuua panya kwani nyingi ni fake.... au ninapoweza kupata hata paka/nyau ambaye yuko makini katika kuua na kufukuza panya.......ushauri unaruhusiwa pia..natanguliza shukurani
 
nenda duka la madawa, nunua endosine (dawa ya mifupa kwa binadamu) hiyo haimkopeshi panya changanya unga wake kwenye kipande cha nyama, samaki au dagaa,
 
Sua wanazo tambi Dawa miye natumia sijawahi kuona hao mabaradhuli ndani mwangu. Pale apopo
 
Nialike mimi hiyo mboga mkuu. Mngekuwa mnawala wasingejenga urafiki wa kuhamia majumbani mwenu kutoka kwao porini.
Bahati mbaya kwetu hatuli wa ndani wana mikosi na wao wanatujua hawana hamu ya kuingia ndani mwetu .
 
Simple tu. Nunua cement kilo moja, dagaaa kisha wasage upate unga wake, changanya na chochote unachodhani panya wanapenda sana. Kiwe katika fomu ya unga unga. Wawekee mahali wanapopita sana. Watakuja kula kwa wingi. Chakula hiki kinawafanya wawe na hamu kubwa ya knywa maji. Wakinywa tu watakuwa wametengeneza blocks tumboni kama matofali. Hawana ujanja, ni kufa kwa maelfu!
 
Back
Top Bottom