Natafuta bestman

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
2,925
1,827
Awe mkristo, mwenye ndoa ya kikristo, awe Dsm, siku ya harusi ni tarehe 22.10.2011.
Asanteni
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
66,100
126,507
wewe ni wa kipekee, hapa kila siku watu wanatafuta wachumba, tena wengine bila aibu utasikia akisema natafuta mchumba mgumba aliyetalakiwa kwa kuto zaa.
Mungu akujalie na kukubariki, umpate bestman ambaye akiona mkeo amekaa kihasara atayafumba macho yake na kuanza kukemea, ili bikini aliyoivaa mkeo igeuke kuwa bukta. Ma bestman wengi ni wavunja ndoa.
Nakutakia kila la kheri
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,337
mi nadhani best man anatakiwa awe mtu wako wa karibu na awe role model fulani, isiwe mtu ni mtu.... anyway, mi ni mwanamke so ngoja waje
 
Pdraze

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
616
321
We umezaliwa msituni na ndo ulikoishi kwani huna marafiki? Hata mim namashaka kuwa bestman wako coz social capital yako ni zero.
 
Derimto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,307
303
Jamani huyu mtu ameomba msaada kwa ma GT wenzake sasa mnaanza kumtisha kwamba atapata jini hebu jaribuni kuwa waelewa wandugu.

back2 topic ni vizuri kuwa na best unayemfahamu itarahisisha mambo kwa upande wangu nina sifa hizo ila nasimamia harusi tarehe 15 oct. Mbali na hapo ningekusaidia ila nadhani unajua kuwa best kuna gharama ndogondogo ambazo nadhani wengi wanazikwepa kutokana na hali halisi ya maisha.
 
King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,802
24,505
ungeainisha pia kama suti, viatu,shati na kijamba koti utagharamia mwenyewe. ila inashangaza kidogo,kuwa kwenye social network yako ya majirani, ndugu, kazini, marafiki na marafiki wa marafiki zako umekosa best man kabisa? mchumba umepata wapi?
 
babalao

Forum Spammer
Mar 11, 2006
427
56
Endelea na mpango huo utaumia uslinilaumu kuwa nilikuonya huko unakoishi huna rafiki?
 
sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,283
3,099
Best man anatakiwa kuwa analingana na wewe kwa umbo na urefu, ikibidi hata tabia zenu zifanane. Na hata hujasema una umri gani ili tabia zenu zifanane kwa sababu best man ni tofauti na mshenga.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Awe mkristo, mwenye ndoa ya kikristo, awe Dsm, siku ya harusi ni tarehe 22.10.2011.
Asanteni

Duh, hii kali mkuu, huna wanandoa ambao una admire ndoa yao? Hao ndo unatakiwa uwatafute, uwapate, uwaombe wasimamie ndoa yako maana ni watu muhimu sana kwenye ndoa yako, infact ni wazazi kabisa wa kulea na kuwashauri kwenye suala la ndoa.

Suala si kuwa Dar au Mbeya Mkuu.
 
Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Best man anatakiwa kuwa analingana na wewe kwa umbo na urefu, ikibidi hata tabia zenu zifanane. Na hata hujasema una umri gani ili tabia zenu zifanane kwa sababu best man ni tofauti na mshenga.

Usimpotoshe mwezio; ndio maana mnapotea.

Bestman si umbo wala sura, ni zaidi ya rafiki, ni role model, ni mlezi" ni mzazi, na ni mshauri. Bestman mzuri ni yule aliyekomaa na mwenye ndoa imara ya mfano. Ni vema Bestman awe na umri mkubwa ili muwe free kumuhusisha masuala ya ndoa
 
NgumiJiwe

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
871
295
hivi kuwa bestman lazima uwe umeoa?mimi sijaoa lakini kuna rafiki yangu anataka nisimamie ndoa yake,itawezekana?
 
Mamushka

JF-Expert Member
Feb 17, 2010
1,600
97
wewe ni wa kipekee, hapa kila siku watu wanatafuta wachumba, tena wengine bila aibu utasikia akisema natafuta mchumba mgumba aliyetalakiwa kwa kuto zaa.
Mungu akujalie na kukubariki, umpate bestman ambaye akiona mkeo amekaa kihasara atayafumba macho yake na kuanza kukemea, ili bikini aliyoivaa mkeo igeuke kuwa bukta. Ma bestman wengi ni wavunja ndoa.
Nakutakia kila la kheri

Heee tena! Makubwa haya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom