Natabiri kuna jambo zito sana la siri linaendelea katika siasa za Tanzania

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Nasikia sauti ktk moyo wangu ina niambia kuna jambo lasiri sana linaendelea ktk siasa za Tanzania.

Jambo hili hata mimi sijuwi ila yatupasa kuliombea taifa kwa machozi na damu.

Kuna kimya chakutisha sana tena kutoka kwa wenye roho za hili Taifa, kuna giza nene limeikumba nchi na tunaiyona nembo ya taifa tu ikiwakawaka ktk moyo wa Taifa.

Ukimya huu huwezi kuuwona wala kuhisi kama nimwanadam wakawaida. Ila mimi naona nakuwathibitishia kalitafute neno au andiko la mzee yeyote unaye mjuwa mwenye hekima na alie shiba siri za taifa hili. Ukiliona rudi hapa uniambie mm nitapeli.

Kama ni mchezo wa draft basi mchezeshaji wa hii draft atakuwa na nguvu za ajabu maana draft inameza kete na draft inatoa mlio wa ajabu pindi kete zinasukumwa.
Hakuna anaye shituka wala kudhania kesho yaweza ikawa juu chini na chini juu.

Mtikisiko ulio ikumba Dodoma sasa unaenda kuwa mtikisiko mkubwa zaidi kwakuwa serikali inaongozwa kwa siri na wengi hufa na siri zao.

Basi tuliombee taifa. Epuka kuongea au kumsuta mwenzako ukijuwa unaye msuta hujuwi kama vile wewe hakujuwi.

Nawaona wana kijani wanaongea sana nakudhani kuanguka kwa Ndugai ni fursa ila nataka niwaambie huu ndio mwanzo wa utungu.

Yapo mambo hatuyaoni ila sasa yataonekana.

Yapo mambo hatujuwi ila sasa yatajulikana.

Wakati haya yanaendelea mataifa yenye nguvu duniani yanafuwatilia kwa ukaribu kile kinaendelea ktk siasa za Tz.

Pray for Nation. Amen
 
Amen.

Mungu wa mbinguni atatuvusha!
Hata Ndugai alijua mnazareti rafiki yake atamvusha, kumbe mnazareti alishamchoka kwani aliwahi kumsingizia.

Kamwe siombei wanakijani, natamani kikombe cha Mungu kijae na kumwagika juu yao, CCM inachosha, imejimilikisha nchi, tumetumiwa vya kutosha kama machangu wa Sinza.

Nasema nimeichoka ccm, naomba nisife kabla sijauona mwisho wa enzi yao.
 
Jambo ambalo huwa linanishangaza kwa hawa manabii pori, utabiri wao siku zote ni MABAYA tu🤥

Ina maana hakuna jema hata moja linastahili kwa hii nchi!?

Tabiri zenu ni Majanga, mikosi, balaa, vifo na makorokoro mengine yafananayo na hayo. Tabirini NEEMA sasa.

Tumechoka!
 
Kuna hatari mbele ya Tanzania ambayo ni 666. Ndugai ni spika wa Sita katika orodha ya maspika wote ambaye amejiuzulu nafasi yake kama spika wa bunge tarehe Sita kwenye awamu ya Sita (666) ni ishara ya kuwa makini na hatari iliyopo mbele ya Tanzania. Chunga mazingira yaliyo kuzunguka.
 
153FBEFC-F81E-4A8E-B254-430D92042209.jpeg
Acha bwana?
 
Kuna hatari mbele ya Tanzania ambayo ni 666. Ndugai ni spika wa Sita katika orodha ya maspika wote ambaye amejiuzulu nafasi yake kama spika wa bunge tarehe Sita kwenye awamu ya Sita (666) ni ishara ya kuwa makini na hatari iliyopo mbele ya Tanzania. Chunga mazingira yaliyo kuzunguka.
Naona unataka kutoa single. Ongeza mstari baada ya speaker Samwel SITA kufariki.
 
Back
Top Bottom