Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Atatoa tu pongezi kama yeye alivyopewa pongezi wote ni wale wale tu tofauti yao ni njia waliyopitia, kumbuka hata Nkuruzinza wanamtetea lakini aliyoyafanya, anayoyafanya waliyaona, wanayaona na wanayajua katika nchi za Africa hakuna demokrasia na ndio maana Trumph ametamka wazi tunahitajika kutawalaiwa tena na wakoloni ili kuondoa hili tabaka la hawa viongozi wanaong'ang'ania madaraka na kujineemesha na rasilimali za nchi zao huku wanachi wakiendelea kuwa masikini na kukosa uhuru wa kujiamulia mambo ya nchi zao na maisha yao kwa ujumla.
Dwmokrasia ina gharama yake, cameroun akishauri ushoga uhalalishwe kikatiba watu mnalalamika wakati ni sehemu ya demokrasia hiyo! Acha kufikiri kwamba mwisho wa au maana ya demokrasia ni kutotumia ujanja kwa chama tawala kurudi madarakani, demokrasia ina bei yake, tena sio ndogo kwa watu wenye tamaduni zinazokinzana na wazungu.
 
Zamani sana Nigeria kulikuwa na uhuni huni wa aina hii, lakini kwa vile jeshi lao in la wasomi wakaamua kuwa wanaipindua nchi kwa kupokezana mpaka wanasiasa walioojifunza maana ya madaraka ya kuchaguliwa na kurudishiwa mamlaka ya kiraia. Ndio maana wizi wa kura wa kijinga haupo tena na ukishindwa unakabidhi madaraka kwa upole na majeshi hayahusiki na michakato ya uchaguzi
Kwa hiyo waliweza kutatua tatizo bila wazungu?maana wengine wanasema waafrika(manyani) tutawaliwe tena na wazungu ndio tutakuwa sawa.
 
Siamini kama nchi hii inamajipu kama mnavyotaka kutuaminisha,yatakuwa yametoka wapi? Ccm na wanaccm mnaipenda sana Tanzania na watanzania, wapinzani ndio vibaraka tu wa wazungu,sasa hayo majipu yanatokea wapi na nchi hii inaongozwa na ccm kwa miaka yote 55 ya Uhuru wake? Au yaliachwa na wakoloni?
kuna kamsemo kamoja
msafara wa mamba(malizia na utapata maana kwanini kuna majipu)
 
Kwa hiyo waliweza kutatua tatizo bila wazungu?maana wengine wanasema waafrika(manyani) tutawaliwe tena na wazungu ndio tutakuwa sawa.
nimeshindwa kabisa kuwaelewa hawa viumbe wa mungu
 
asimpe pongezi museven kwasababu magufuli alishinda kihalali?africa ulevi na ulafi wa madaraka hautakaa uishe kwasababu sisi wachaguagi tumezidi uoga na upuuziagi.wacha tuburuzwe
magufuli alishinda kihalali,si hata mseveni ameshinda kihalali kama uhalali maana yake ni mwenyekiti wa Tume kumtangaza mshindi
 
JPM akimpongeza Museven na ye atakuwa ni jipu , linalohitaji kutumbuliwa .
 
Na wewe pia mtoa mada tunakuomba urekebishe hapo badala ya kusema sisi wananchi wa watanzania,,,sema mimi binafsi mwananchi wa Tanzania sijaridhishwa na matokeo ya urais ya uganda

Eti anamzuia Rais asiwasemee watanzania, alafu yeye ndiyo amekua msemaji wetu, maana ametusemea sasa.
 
Ukawa sasa hivi hakuna hoja
Mnaegemea zanzibar tu,huijui katiba ya zanzibar iliopitishwa na cuf na ccm mwaka 2010,kina warioba waliipinga kuwa ni kiashiria cha mpasuko wa muungano,mlikaa kimya
Katiba ya zanzibar,imeipa zec mamlaka yote na haiingiliwi na yoyote,ikaitwa tume huru kwa kuwa tu cuf ina mashabiki wake na ccm ina mashabiki wake.
Kwa mujibu wa katiba ya zanzibar,magufuli hana mamlaka ya kuingilia masuala ya uchaguzi zanzibar.

Wangekuwa hawana mamlaka ya kuiingilia uchaguzi usingefutwa sema kauli hiyo inamnufaisha mshindwa (CCM )
 
kuna kamsemo kamoja
msafara wa mamba(malizia na utapata maana kwanini kuna majipu)

Kwa jinsi nchi ilivohujumiwa kwa kiwango cha kutisha chini ya chama kimoja (CCM) hadi kauli ya "mabadiliko" badala ya jina la chama ikawa ndio janja ya ushindi, kamsemo bora ni kuwa "kwenye msafara wa kenge ...".
 
kuna kamsemo kamoja
msafara wa mamba(malizia na utapata maana kwanini kuna majipu)
unataka kusema ndani ya ccm kuna viongozi na baadhi ya wanachama wasioipenda Tanzania?mnawezaje kukaa pamoja sasa? Mimi ninaamini ndege wasiofanana hawawezi kuruka pamoja,na mnaposema ccm ni ile ile huwa , Au sijakuelewa Mkuu?
 
Magu lazima amsuport dikteta mwenzake Museveni ili naye Museveni aje ampe shavu kwa ujinga Magu anaoufanya huku Zanzibar. ni aibu yao maana wote tuna macho na masikio na dunia yote inawaangalia.Magu kazi kwako!
 
Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.
Hata ushindi wa jpm ulitiliwa shaka ampongeze tu, hana ujasiri wa kutopongeza naye chama chake kimepoka ushindi wa cu..
 
Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.
Mkuu umeandika ukweli mtupu ingawa ni msumali wa moto kwa watawala, tulicho shuhudia uganda ni u akwaji mkubwa wa demokrasia na haki za binadamu mkubwa akishirikiana na lubuva wa nchi yake
 
Back
Top Bottom