Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.
Uzi umeandika peke yako halafu unasema sisi watanzania..................!
 
Baada ya 2020, serikali ya CCM itabadili katiba kuondoa ukomo wa mtu kugombea urais. Magufuli ataka kuendelea kuwa rais. Mark my words.
Kwa hiyo, Magufuli atatoa pongezi murua kwa Museveni bila shida yeyote.... Mark my words.
 
Njia aliyotumia Museveni kurudi madarakani ndiyo hiyo hiyo aliyotumia Magufuli kuingia madarakani.
 
Waajemi wa Iran wangekuwa na akili fupi kama hii wangeendelea kumng'ang'ania rais Ahmed Amenihjad kama wewe unavyotaka akina Museveni,Mugabe waendelee kutawala kwa kisingizio kwamba wanawachukia Wazungu,maana Amenihjad naye alikuwa hazipendi kabisa nchi za magharibi.Bahati nzuri sana Waajemi wana akili pana kuliko sisi Waafrika,waliangalia changamoto za kimaisha zinazowakabili wao kama wananchi,wakati wa uchaguzi wakampiga chini Amenihjad na sasa wanavuna matunda mema ya matumizi mazuri ya kura zao,Iran imeondolewa vikwazo vya kiuchumi sasa wapo huru kufanya biashara na nchi yoyote ulimwenguni,ni hatua moja muhimu ktk kuelekea kulitatua tatizo la ajira kwa kuwa milango ya kibiashara imefunguliwa sasa,Wairan wafanyabiashara watafanya biashara zao nje na wale wawekezaji wa kigeni wataanza kufurika ndani ya taifa la Iran. Hizi ndizo siasa za kuangalia mbele,siasa zetu za kudhani kuwachukia na kuwatukana Wazungu ndio tumemaliza kila kitu.
ni sawa tu na aliye tayari na atawale
hao wakina besigye ni wanafiki na wazandiki wawazungu wanapiganiwa kwa maslahi fulani
 
It is very true.

Nchi kama Burundi, Uganda, Zimbabwe, Rwanda bila kuiacha TZ, hazipaswi kujiita ziko katika mfumo wa vyama vingi wakati katika hali halisi zingali katika mfumo wa chama kimoja.

Tuchukuliane mfano nchini kwetu kwa yaliyotokea Zanzibar.

Uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki na uthibitisho wa hilo ni taarifa za waangalizi wote wa uchaguzi huo kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi waliothibitisha kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa ZEC naye alitangaza matokeo kwa siku 2 mfululizo kwa majimbo 31 kati ya jumla ya majimbo yote 54 ya Unguja na Pemba.

Wasimamizi wa uchaguzi huo nao wakiwapa vyeti vya ushindi wawakilishi kwemye Baraza la wawakilishi.

Lakini kwa mshsngao mkubwa tarehe 28/10/2015 ambayo Mwenyekiti wa ZEC ndipo alipaswa kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais, badala yake akaibukia ZBC tena bila kuambatana na makamishina wenzie ws ZEC akitangaza kuwa uchaguzi ule na mayokeo yake yote ameyafuta kwa mamlaka aliyopewa na 'watawala' wake!

Kwa bara la Afrika kuondokana na viongozi hawa ving'ang'anizi' tulionao ambao hawako tayari kuyaachia madaraka kwa kupitia sanduku la kura ni kuombea tu kule Marekani ambayo ni 'kiranja' wa dunia kwa mgombea wa Republican Donald Trump apewe ridhaa na wamarekani ya kuliongoza Taifa hilo kubwa ili awashikishe ' adabu' viongozi hawa ambao wanaziona nchi wanazozitawala kama their own properties!
Ukawa sasa hivi hakuna hoja
Mnaegemea zanzibar tu,huijui katiba ya zanzibar iliopitishwa na cuf na ccm mwaka 2010,kina warioba waliipinga kuwa ni kiashiria cha mpasuko wa muungano,mlikaa kimya
Katiba ya zanzibar,imeipa zec mamlaka yote na haiingiliwi na yoyote,ikaitwa tume huru kwa kuwa tu cuf ina mashabiki wake na ccm ina mashabiki wake.
Kwa mujibu wa katiba ya zanzibar,magufuli hana mamlaka ya kuingilia masuala ya uchaguzi zanzibar.
 
Waajemi wa Iran wangekuwa na akili fupi kama hii wangeendelea kumng'ang'ania rais Ahmed Amenihjad kama wewe unavyotaka akina Museveni,Mugabe waendelee kutawala kwa kisingizio kwamba wanawachukia Wazungu,maana Amenihjad naye alikuwa hazipendi kabisa nchi za magharibi.Bahati nzuri sana Waajemi wana akili pana kuliko sisi Waafrika,waliangalia changamoto za kimaisha zinazowakabili wao kama wananchi,wakati wa uchaguzi wakampiga chini Amenihjad na sasa wanavuna matunda mema ya matumizi mazuri ya kura zao,Iran imeondolewa vikwazo vya kiuchumi sasa wapo huru kufanya biashara na nchi yoyote ulimwenguni,ni hatua moja muhimu ktk kuelekea kulitatua tatizo la ajira kwa kuwa milango ya kibiashara imefunguliwa sasa,Wairan wafanyabiashara watafanya biashara zao nje na wale wawekezaji wa kigeni wataanza kufurika ndani ya taifa la Iran. Hizi ndizo siasa za kuangalia mbele,siasa zetu za kudhani kuwachukia na kuwatukana Wazungu ndio tumemaliza kila kitu.
stori ndefu pumba tupu
 
magufuli alisababishiwa ashinde
.yeye alikua ajui kitu ila kuanzia mwinyi.mlapa.jk.ndio waliompa njia
 
Uchaguzi wa Uganda umeonyesha ni jinsi gani viongozi wa Africa walivyo na uchu wa madaraka na kutumia nguvu za vyombo vya dola (kodi za wananchi) na wapambe wasiojua walikuja duniani kufanya nini wakikandamiza haki za wananchi
Mi nadhani kama mabo yenyewe ndio hayo hawakuwa na sababu ya kupoteza muda na mapesa meengi kufanya uchaguzi
 
Magufuri huyu aliyeshindwa kusimamia haki Zanzibar ndiye unafikiri ataacha kujitutumua kutoa pongezi!? Namsubiri Donald Trump.
 
It is very true.

Nchi kama Burundi, Uganda, Zimbabwe, Rwanda bila kuiacha TZ, hazipaswi kujiita ziko katika mfumo wa vyama vingi wakati katika hali halisi zingali katika mfumo wa chama kimoja.

Tuchukuliane mfano nchini kwetu kwa yaliyotokea Zanzibar.

Uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki na uthibitisho wa hilo ni taarifa za waangalizi wote wa uchaguzi huo kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi waliothibitisha kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa ZEC naye alitangaza matokeo kwa siku 2 mfululizo kwa majimbo 31 kati ya jumla ya majimbo yote 54 ya Unguja na Pemba.

Wasimamizi wa uchaguzi huo nao wakiwapa vyeti vya ushindi wawakilishi kwemye Baraza la wawakilishi.

Lakini kwa mshsngao mkubwa tarehe 28/10/2015 ambayo Mwenyekiti wa ZEC ndipo alipaswa kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais, badala yake akaibukia ZBC tena bila kuambatana na makamishina wenzie ws ZEC akitangaza kuwa uchaguzi ule na mayokeo yake yote ameyafuta kwa mamlaka aliyopewa na 'watawala' wake!

Kwa bara la Afrika kuondokana na viongozi hawa ving'ang'anizi' tulionao ambao hawako tayari kuyaachia madaraka kwa kupitia sanduku la kura ni kuombea tu kule Marekani ambayo ni 'kiranja' wa dunia kwa mgombea wa Republican Donald Trump apewe ridhaa na wamarekani ya kuliongoza Taifa hilo kubwa ili awashikishe ' adabu' viongozi hawa ambao wanaziona nchi wanazozitawala kama their own properties!
Kwa taarifa tu tangaz o la jecha si live na lilitengenezwa sehemu kule ZBC imeenda cd/flash tu!
 
Africa ndo inabalehe kwa iyo lazima viongozi wawe na uchu na madaraka hapa trump ndo tegemezi
 
Kama wale weusi wachache waliyopo kwa akina Trump wanapigwa shaba je,vp wakija kutawala huku tulipojaa watu weusi?
Itakuwa powa tu kaka bars LA Africa ni utumwa na kwenda mbele tumeshidwa kujitawala
 
Hivi gharama ya kumpongeza Museveni inaweza kujenga kilomita ngapi za reli kwa kiwango cha lami?
 
Sitashangaa siku moja kusikia serikali za Africa zinafungia mitandao ya kijamio moja kwa moja, kama demokrasia zenyewe ndo za namna hii.

Kuna watu hapa wanapingana na mimi kuhusu nlichoandika, nashindwa kuelewa ya kuwa wao wanakubaliana au hawakubalian na hicho kilichotokea Uganda

Mpaka sasa ni marais wawili tu ambao washampongeza Museven, Uhuru Kenyata alikua wa kwanza, leo nimeona tweet ya
dictactor Nkurunziza nae akimpongeza.
 
ni jambo jema kuona besigye akishinda. museveni anatakiwa kulinda heshima yake kwa kuondoka mad mad at a man Iarakani.
Unaongelea uchaguzi upi kama matokeo tayari huyu pimbi kishatangazwa mshindi na tume yake!?
ni jambo jema kuona besigye akishinda. museveni anatakiwa kulinda heshima yake kwa kuondoka madarakani.
Unaongelea uchaguzi upi kama matokeo tayari huyu pimbi kishatangazwa mshindi na tume yake!?
 
Sijui atampongeza?? Maana ule ulikuwa Ni uchafuzi dhahiri wa shahiri....
 
Back
Top Bottom