Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Njia aliyotumia Museveni kurudi madarakani ndiyo hiyo hiyo aliyotumia Magufuli kuingia madarakani.

Hapana mkuu, Museven kavunja rekodi, haijawahi kutokea demokrasia ya namna hii dunia.

Alafu kumbuka magufuli aliingizwa madarakan, Museven kajirudisha madarakan
 
Haha #WhatWouldMagufuliDo

Ni fact kwamba ikiwa H.E Dr Pombe atampongeza Mhisani mkubwa wa Uganda ndugu Museveni inabidi atumie Mtandao kwa muda wa dakika kumi nukta sifuri tatu,muda ambao unatosha kabisa kutumbua majipu mawili nukta saba mbili huku akiokoa vocha ya shilingi 3000 nukta moja!
 
It is very true.

Nchi kama Burundi, Uganda, Zimbabwe, Rwanda bila kuiacha TZ, hazipaswi kujiita ziko katika mfumo wa vyama vingi wakati katika hali halisi zingali katika mfumo wa chama kimoja.

Tuchukuliane mfano nchini kwetu kwa yaliyotokea Zanzibar.

Uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki na uthibitisho wa hilo ni taarifa za waangalizi wote wa uchaguzi huo kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi waliothibitisha kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa ZEC naye alitangaza matokeo kwa siku 2 mfululizo kwa majimbo 31 kati ya jumla ya majimbo yote 54 ya Unguja na Pemba.

Wasimamizi wa uchaguzi huo nao wakiwapa vyeti vya ushindi wawakilishi kwemye Baraza la wawakilishi.

Lakini kwa mshsngao mkubwa tarehe 28/10/2015 ambayo Mwenyekiti wa ZEC ndipo alipaswa kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais, badala yake akaibukia ZBC tena bila kuambatana na makamishina wenzie ws ZEC akitangaza kuwa uchaguzi ule na mayokeo yake yote ameyafuta kwa mamlaka aliyopewa na 'watawala' wake!

Kwa bara la Afrika kuondokana na viongozi hawa ving'ang'anizi' tulionao ambao hawako tayari kuyaachia madaraka kwa kupitia sanduku la kura ni kuombea tu kule Marekani ambayo ni 'kiranja' wa dunia kwa mgombea wa Republican Donald Trump apewe ridhaa na wamarekani ya kuliongoza Taifa hilo kubwa ili awashikishe ' adabu' viongozi hawa ambao wanaziona nchi wanazozitawala kama their own properties!
Mkuu Mimi kura yangu kwa Trump
 
ni sawa tu na aliye tayari na atawale
hao wakina besigye ni wanafiki na wazandiki wawazungu wanapiganiwa kwa maslahi fulani
Mkuu kwa mfano Tz ccm ipo kwa masilahi ya nani? Na nini chanzo cha majipu mnayotuaminisha yanayotumbuliwa sasa
 
Mkuu kwa mfano Tz ccm ipo kwa masilahi ya nani? Na nini chanzo cha majipu mnayotuaminisha yanayotumbuliwa sasa

Watu kama hao , hua napata muda mgumu kuelewa ni nin hasa msimamo wao
 
Ukawa sasa hivi hakuna hoja
Mnaegemea zanzibar tu,huijui katiba ya zanzibar iliopitishwa na cuf na ccm mwaka 2010,kina warioba waliipinga kuwa ni kiashiria cha mpasuko wa muungano,mlikaa kimya
Katiba ya zanzibar,imeipa zec mamlaka yote na haiingiliwi na yoyote,ikaitwa tume huru kwa kuwa tu cuf ina mashabiki wake na ccm ina mashabiki wake.
Kwa mujibu wa katiba ya zanzibar,magufuli hana mamlaka ya kuingilia masuala ya uchaguzi zanzibar.
Lakini kupeleka jeshi na kutesa watu anao mamla hayo sasa mm nashindwa kuelewa kama kiongozi unaruhusu vipi katiba na sheria za nchi zinavunjwa?he vipi kura za magufuli ziwe halali na Sefu ziwe kharamu wakati watu wamepiga kura Sikh moja na daftari LA kura moja kweli sisi waafrica tumeumbwa tuwe watumwa tumeshidwa kutafautisha nyekundu na nyeupe
 
Mkuu kwa mfano Tz ccm ipo kwa masilahi ya nani? Na nini chanzo cha majipu mnayotuaminisha yanayotumbuliwa sasa
je??huamini katika utumbuaji majipu
je??humuamini raisi wako na baraza lake lote
 
Museveni mikononi mwa donald trump atamkamata na kumsweka ndani asilogwe tu akasogelea usa
 
Hapana mkuu, Museven kavunja rekodi, haijawahi kutokea demokrasia ya namna hii dunia.

Alafu kumbuka magufuli aliingizwa madarakan, Museven kajirudisha madarakan
kiongozi wrote wa Africa wanaingia madaraka ni kwa wizi wa kura mijizi mitupu
 
Lakini kupeleka jeshi na kutesa watu anao mamla hayo sasa mm nashindwa kuelewa kama kiongozi unaruhusu vipi katiba na sheria za nchi zinavunjwa?he vipi kura za magufuli ziwe halali na Sefu ziwe kharamu wakati watu wamepiga kura Sikh moja na daftari LA kura moja kweli sisi waafrica tumeumbwa tuwe watumwa tumeshidwa kutafautisha nyekundu na nyeupe
aliye tayari atawale
 
Tufike wakati uchaguz webasi ' watara waendele kutawara hakuna HAKI kama ingekuwepo Leo hii asingekuwa madarakan MUSEVEN wala MAGU.
 
Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.
Uchaguzi wa Tanzania walimwibia kura Lowasa lakini hawakuwa na vitendo vya kuwanyanyasa wapinzani kuwapiga kuwafungia ndani, kuwatesa Kama Uganda ndiyo maana walipokwenda The Hague ikawa vigumu kufungua kesi. Lakini Uganda Unyama waliotendewa wapinzani umeonekana kote Duniani na kama ni ushahidi upo mwingi wa kutosha nashangaa ni kwa nini hawaendi kushitaka kwenye Mahakama ya Uhalifu ya kimataifa?
 
Wako under house arrest mpaka sasa , no one is allowed in or out of the house , dada yake peke yake ndo aliyeruhusiwa kuingia jana , pia kakatiwa mawasiliano ya internet hapo nyumban kwake
 
Zamani sana Nigeria kulikuwa na uhuni huni wa aina hii, lakini kwa vile jeshi lao in la wasomi wakaamua kuwa wanaipindua nchi kwa kupokezana mpaka wanasiasa walioojifunza maana ya madaraka ya kuchaguliwa na kurudishiwa mamlaka ya kiraia. Ndio maana wizi wa kura wa kijinga haupo tena na ukishindwa unakabidhi madaraka kwa upole na majeshi hayahusiki na michakato ya uchaguzi
 
je??huamini katika utumbuaji majipu
je??humuamini raisi wako na baraza lake lote
Siamini kama nchi hii inamajipu kama mnavyotaka kutuaminisha,yatakuwa yametoka wapi? Ccm na wanaccm mnaipenda sana Tanzania na watanzania, wapinzani ndio vibaraka tu wa wazungu,sasa hayo majipu yanatokea wapi na nchi hii inaongozwa na ccm kwa miaka yote 55 ya Uhuru wake? Au yaliachwa na wakoloni?
 
Back
Top Bottom