Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Nasubiria kumsikia Magufuli akimpongeza Museveni

Dunia nzima imeona,waganda wameona na watanzania tumeona democrasia ikibakwa Uganda.Ni kweli,kama Magufuli anataka kumpongeza Magufuli ampongeze kama yeye,sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania.Isipokuwa hata hapo tutamuona ni mnafiki asiyeitendea haki nafsi yake.Ila kama hakutendea haki nafsi yake Zanzibar,si ajabu asiitendee haki Uganda.
Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa wala kuheshimiwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.

Kwa wale mnaouliza kwa nini nawasemea watanzania wote .
 
ni jambo jema kuona besigye akishinda. museveni anatakiwa kulinda heshima yake kwa kuondoka madarakani.
Kwa Uganda unayaona hayo lakini kwa Tanzania unashabikia wanayoyafanya CCM, unaweza kutofautisha hayo ya Museven wa Uganda na yaliyotokea Zanzibar? ya CCM na Zanzibar unayatetea ya Uganda unayakemea wewe kweli msukule haujielewi kabisa NYAMBAAAFUU!!!
 
Wanaoona kuwa Mu7 hana haki ya kuwa rais ndio haohao waliyosema ccm wameiba kura hivyo Magufuli nae hana haki ya kuwa rais.
Sasa leo mnapopiga kelele za Magufuli asitoe pongezi kwa M7 si inakuwa upumbavu mtupu.
 
Chenge na Tibaijuka ni wabunge waaminifu na huyo chenge ccm mmethububutu hata kumpatia nafasi nyeti ya kuliongoza bunge,alafu bado bila ya aibu unakuja hapa jamvini ku mbwelambwela, una maanisha nini?ccm ni majizi
Kashifa ya ESCROW ilitoa faida moja ya kutuonyesgha tulivyokuwa taifa la wanafiki na kimsingi uelewa mdogo wa siasa,walio pewa mgao ulio kwapuliwa bank kuu ndio tunawaita wapiga dili.Walio piga dili na kukwapua pesa hizo kutoka bank kuu tuko kimya,hivi ni ujinga?au chuki binafsi kwa watu walio gawiwa kihalali?wivu ndio unatutuma kuandika inaonesha na sisi tukipata nafasi iyo iyo tutakua wapiga dili.TUNATAKA LIST YA STANBIC BANK
 
Mkuu upo sahihi kabisa lkn hata iweje hakuna mtu atakaye kubali kutoa hiyo list ya watu walio chukua mpunga kupitia hiyo bank,maana ukiwagusa mafisadi nchi itayumba
 
Mode, tutengenezee jukwaa la walalamishi ili tukienda huko tunajua ni lawama na matusi.
 
Africa Demokrasia imebaki jina tu ,kiongozi kabla ya uchaguzi anaagiza magari ya maji ya kuwasha tena kwa pesa nyingi tu za walipa kodi wakati hospitali hazina madawa na vifaa mbali mbali.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Uchaguzi uganda umekwisha , Tume ya uchaguzi Uganda imemtangaza Museven kuwa ameshinda kiti cha uraisi kwa asilimia 60.75 .

Dunia nzima imeona kilichotokea Uganda , Museven katumia mabavu kurudi madarakani , demokrasia imebakwa , maamuzi ya wananchi hayajatekelezwa wala kuheshimiwa , wapinzan wamenyanyaswa kipindi chote cha kampen na wameendelea kunyanyaswa mpaka hata baada ya uchaguzi . Kipindi chote cha uchaguzi alifungia mawasiliano ya mitandao ya kijamii ( FB , Twitter , WhatsApp etc ) , mpaka miamala ya pesa kwa njia za simu pia ilifungiwa.

Raisi wangu Magufuli , najua ni itifaki kwa wewe kama mkuu wa nchi kutoa pongeza kwa jiran yako Museven kwa ushindi aliopata , tafadhali sisi kama wananchi tunakuomba ukiwa unatoa hiyo pongezi , itoe kama mtu binafsi na sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania . Kwa sabab sisi kama watanzania hatujakubaliana na kilichotokea Uganda , hatuwezi kuwa wanafiki au kuwa kimbelembele kupongeza wakati demokrasia na haki ya msingi ya majirani zetu ikikandamizwa.

Kwa wale mnaouliza kwa nini nawasemea watanzania wote .
Rais alishasema....."Msema kweli ni mpenzi wa Mungu na mimi nitasema ukweli daima watanzania niombeeni" Rais akasema..." Kama kunamtu hakubaliani na ZEC aende mahakamani na atakaeleta fyokofyoko atashughulikiwa kikamilifu" Rais akasema...." Anataka Elimu bure na anamaanisha bure na anataka tanzania ijitegemee isiwe ombaomba iwe na uwezo wakutoa misaada nje, pia serikali yake imekusanya kodi kwakiwangu kikubwa" Ila alikuwa mstari wa mbele kwenye harambee ya kuchangia Elimu Kinondoni
Na tunamkubali sana Rais wetu na Tunamuombea kwa Mungu kwan ni Mfano wa dunia. Hivyo Mkuu usishangae akituma salamu za pongezi tukamshangilia kwakuwa "waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba"
 
It is very true.

Nchi kama Burundi, Uganda, Zimbabwe, Rwanda bila kuiacha TZ, hazipaswi kujiita ziko katika mfumo wa vyama vingi wakati katika hali halisi zingali katika mfumo wa chama kimoja.

Tuchukuliane mfano nchini kwetu kwa yaliyotokea Zanzibar.

Uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki na uthibitisho wa hilo ni taarifa za waangalizi wote wa uchaguzi huo kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi waliothibitisha kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa ZEC naye alitangaza matokeo kwa siku 2 mfululizo kwa majimbo 31 kati ya jumla ya majimbo yote 54 ya Unguja na Pemba.

Wasimamizi wa uchaguzi huo nao wakiwapa vyeti vya ushindi wawakilishi kwemye Baraza la wawakilishi.

Lakini kwa mshsngao mkubwa tarehe 28/10/2015 ambayo Mwenyekiti wa ZEC ndipo alipaswa kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais, badala yake akaibukia ZBC tena bila kuambatana na makamishina wenzie ws ZEC akitangaza kuwa uchaguzi ule na mayokeo yake yote ameyafuta kwa mamlaka aliyopewa na 'watawala' wake!

Kwa bara la Afrika kuondokana na viongozi hawa ving'ang'anizi' tulionao ambao hawako tayari kuyaachia madaraka kwa kupitia sanduku la kura ni kuombea tu kule Marekani ambayo ni 'kiranja' wa dunia kwa mgombea wa Republican Donald Trump apewe ridhaa na wamarekani ya kuliongoza Taifa hilo kubwa ili awashikishe ' adabu' viongozi hawa ambao wanaziona nchi wanazozitawala kama their own properties!
...unajua sana siasa siku hizi wewe
 
Dunia nzima imeona,waganda wameona na watanzania tumeona democrasia ikibakwa Uganda.Ni kweli,kama Magufuli anataka kumpongeza Magufuli ampongeze kama yeye,sio kwa niaba ya wananchi wa Tanzania.Isipokuwa hata hapo tutamuona ni mnafiki asiyeitendea haki nafsi yake.Ila kama hakutendea haki nafsi yake Zanzibar,si ajabu asiitendee haki Uganda.

Siyo kweli kuwa Dunia nzima imeona kuwa demokrasia 'imebakwa' huko Uganda. Na siyo kweli kuwa Watanzania wote wameona demokrasia 'imebakwa' huko Uganda.
 
Siyo kweli kuwa Dunia nzima imeona kuwa demokrasia 'imebakwa' huko Uganda. Na siyo kweli kuwa Watanzania wote wameona demokrasia 'imebakwa' huko Uganda.

We umeonaje .?
 
MIMI NAMPONGEZA MBOWE KWA KUONGOZA NYUMBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Kikombe alichonywea yeye ndio alicho nywea Museveni acha wapongezane.
 
Unasema Magufuli kawa rais kwa wizi wa kura lakini umeshindwa kuzuia hilo,leo hii ukiuliza rais wa Tanzania utaambiwa ni Magufuli. Ajabu tena wewe ndio umzuie Magufuli kutoa pongezi.
 
Unasema Magufuli kawa rais kwa wizi wa kura lakini umeshindwa kuzuia hilo,leo hii ukiuliza rais wa Tanzania utaambiwa ni Magufuli. Ajabu tena wewe ndio umzuie Magufuli kutoa pongezi.

Unajua kusoma wewe , embu rudia kusoma hicho nlichoandika hapo juu , afu useme ni wapi nimemzuia raisi kutoa pongezi .! Nimesema akitoa pongeza asitumia neno "sisi" kama mwenzie Uhuru , aseme tu "nakupongeza" kwa kushinda , na sabab ya mimi kusema hivyo , nimeieleza hapo juu , na wengine wengi wakaifanunua kwa ufasaha zaid .
 
Demokrasia ni mfumo wa hovyo sana unaotumika kuongoza dunia ila huko baadae vizazi vijavyo vitakuja kutushangaa sana kwamba tuliwezaje kujitawala kwa mfumo wa hovyo kama huu..!!!
 
Back
Top Bottom