Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, May 5, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wajumbe,
  Huku tukiendelea kusikitika na baraza lisilo na uwakilishi wa watanzania, huenda tukapata misiba mingine very soon!  SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri Mbwambo (36), kuuawa kwa kuchinjwa Aprili 27 mwaka huu, Mbunge wa Jimbo hilo, Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wamedai kupokea ujumbe wa maneno kwenye simu ya kiganjani unaowatishia kuwaua.

  Akizungumza mjini hapa, Nassari alisema amepata ujumbe wa kumtishia kumuua na viongozi wa matawi wa jimbo la Arumeru Mashariki ambao walikuwa mstari wa mbele kumpigania kupata ushindi kwenye kampeni.

  Alisema ujumbe huo aliupata kupitia simu yenye namba 0753-211 367, ambapo namba hiyo ilituma ujumbe wa kuwatishia kuwachinja, kwa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Gadiel Mwanda, Katibu wa Wilaya hiyo, Totinan
  Ndonde.

  Mwenyekiti wa Kata ya Seela Sing'isi, Simba Kimunto na aliyekuwa Mkuu wa operesheni ya ushindi wake, John Mrema.

  Nassari alisoma ujumbe huo kuwa ni, "Tumekuona unabeba jeneza kwenye gazeti, tunakuhakikishia utabeba majeneza Arumeru Mashariki, mpaka ukimbie Ubunge na baada
  ya Mwenyekiti Usa (Msafiri Mbwambo) kumchinja, sasa ni Simba Kimunto muda usiojulikana, utabeba jeneza lake, Jimbo hili tutalichakaza ndani ya miezi sita, nakutakia mazishi mema ya mfululizo."

  Alisema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo akiwa anausoma ukaingia ujumbe mwingine kwa namba hiyo hiyo ukisema, "Bado wewe na Wenyeviti Chadema kwenye kata zako,"
  Nassari alisema kuwa mtu huyo asiyejulikana alituma ujumbe kwa Godbless Lema usemao, "Wewe ng'ombe kama Kimunto alikuwekea Wameru 300 kukulinda Arumeru, sasa wewe utamwekea Wachaga wangapi?

  Kwa sababu baada ya m/kiti Usa River tunamchinja yeye." Alisema Lema naye akiwa
  anatafakari ujumbe huo uliingia mwingine ukisema," Baada ya Mwenyekiti wako wa Usa atafuata Mwenyekiti wa kata ya Seela-Sing'isi Samba Kimunto huyu amekuwa kero wilaya hii ya Arumeru Wenyeviti wa Jimbo hili tutakabiliana nao mwezi huu mtamzika sambamba Kimunto unalo la kusema."

  Aidha alisema kuwa baada ya kupata ujumbe huo alifanya mawasiliano na Katibu wa chama chake wa wilaya hiyo, Totinan Ndonde, ambaye alikwenda kituo cha Polisi cha wilaya hiyo, kutoa taarifa na alipewa RB yenye namba USR/RB/1671/2012.

  Naye Katibu wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde alipopigiwa simu kuulizwa kuhusiana na hilo, alikiri kupokea ujumbe huo wa vitisho vya kuuliwa na wenyeviti wake wa kata na akatoa taarifa Polisi kwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo, John Marona kupewa RB namba USR/RB/1671/2012.

  Sosi: HabariLeo | Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo
   
 2. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nassari, Lema wadaikutishiwa kifo
  SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama chaDemokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, Jimbo la ArumeruMashariki, Msafiri Mbwambo (36), kuuawa kwa kuchinjwa Aprili 27 mwaka huu,Mbunge wa Jimbo hilo, Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa chama hicho,wamedai kupokea ujumbe wa maneno kwenye simu ya kiganjani unaowatishia kuwaua.

  Akizungumza mjini hapa, Nassari alisema amepata ujumbe wakumtishia kumuua na viongozi wa matawi wa jimbo la Arumeru Mashariki ambaowalikuwa mstari wa mbele kumpigania kupata ushindi kwenye kampeni.

  Alisema ujumbe huo aliupata kupitia simu yenye namba 0753-211367, ambapo namba hiyo ilituma ujumbe wa kuwatishia kuwachinja, kwa aliyekuwaMbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, GadielMwanda, Katibu wa Wilaya hiyo, Totinan
  Ndonde.

  Mwenyekiti wa Kata ya Seela Sing’isi, Simba Kimunto naaliyekuwa Mkuu wa operesheni ya ushindi wake, John Mrema.

  Nassari alisoma ujumbe huo kuwa ni, “Tumekuona unabebajeneza kwenye gazeti, tunakuhakikishia utabeba majeneza Arumeru Mashariki,mpaka ukimbie Ubunge na baada
  ya Mwenyekiti Usa (Msafiri Mbwambo) kumchinja, sasa ni SimbaKimunto muda usiojulikana, utabeba jeneza lake, Jimbo hili tutalichakaza ndaniya miezi sita, nakutakia mazishi mema ya mfululizo.”

  Alisema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo akiwa anausomaukaingia ujumbe mwingine kwa namba hiyo hiyo ukisema, “Bado wewe na WenyevitiChadema kwenye kata zako,”
  Nassari alisema kuwa mtu huyo asiyejulikana alituma ujumbekwa Godbless Lema usemao, “Wewe ng’ombe kama Kimunto alikuwekea Wameru 300kukulinda Arumeru, sasa wewe utamwekea Wachaga wangapi?

  Kwa sababu baada ya m/kiti Usa River tunamchinja yeye.”Alisema Lema naye akiwa
  anatafakari ujumbe huo uliingia mwingine ukisema,” Baada yaMwenyekiti wako wa Usa atafuata Mwenyekiti wa kata ya Seela-Sing’isi SambaKimunto huyu amekuwa kero wilaya hii ya Arumeru Wenyeviti wa Jimbo hilitutakabiliana nao mwezi huu mtamzika sambamba Kimunto unalo la kusema.”

  Aidha alisema kuwa baada ya kupata ujumbe huo alifanyamawasiliano na Katibu wa chama chake wa wilaya hiyo, Totinan Ndonde, ambaye alikwendakituo cha Polisi cha wilaya hiyo, kutoa taarifa na alipewa RB yenye nambaUSR/RB/1671/2012.

  Naye Katibu wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde alipopigiwasimu kuulizwa kuhusiana na hilo, alikiri kupokea ujumbe huo wa vitisho vyakuuliwa na wenyeviti wake wa kata na akatoa taarifa Polisi kwa Kaimu Mkuu waUpelelezi wa Wilaya hiyo, John Marona kupewa RB namba USR/RB/1671/2012.

  SOURCE; HABARI LEO
   
 3. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nafikiri mambo haya si ya kuyapuuzia, kunahitajika hatua za haraka. Na Polisi waliosema ahiusiani na siasa kiko wapi?
   
 4. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 80
  hapa ndipo napoona faida ya kusajili namba ya simu. Hawa watu lazima watapatikana sababu jamaa wa voda wameshawasajili namba zao
   
 5. t

  thengoshahimself Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ngumu anaweza tumia jna la uongo
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  inaonyesha jinsi gani hii nchi ina umafia sana..unaua watu kwa sababu jimbo limeangukia kwa upinzani? kwa hiyo yale majimbo ya ccm wapinzani nao waanze kuwachinja wenyeviti wa wilaya wa ccm? aisee huku tunakoelekea ni kubaya...l

  America kiongozi wa chama/MBUNGE au wa nchi akitishiwa maisha FBI wanaingilia...UK viongozi wa nchi au wa vyama wakitishiwa maisha scotland yard wanachunguza..hapa bongo viongozi wa vyama wanatishiwa ilitakiwa usalama wa taifa or polisi makao makuu kuchunguza hili swala ila badala yake nasikia eti wameenda polisi huko meru kureport.....IT CAN ONLY HAPPEN IN BONGO :angry:
   
 7. k

  kiche JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Haya mambo yasipochukuliwa hatua mapema itakuwa ile hadithi ya mwakyembe na sms za vitisho. Lisemwalo lipo kama halipo linakuja.
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Duh! Hii ni taarifa mbaya ndani ya UMMA bila ya chenga!

  Napenda kujua kama hila la usajili wa simu kama inafanyaga kazi kweli!
  Na kwa mtazamo wangu,Mi naona hili jambo halina haja ya kulipuuza hata punje!
  Hapa ningependa nione ushirikiano kwa jeshi lengwa na hata raia kwani tofauti na hapo yaweza yale Igunga yakawa madogo kwa ya hapa Armr/Mashariki.

  Ila nina IMANI ya kwmb,kama hz mitandao ya VodaCom itatenda haki,bila shaka mwenye matumizi na ile lain hana muda atakuwa mkononi mwao.

  Kwa hili ningependa sana nione ushirikiano pande zote!


  Hii ccm ni JANGA KUBWA kwa Taifa letu!
   
 10. k

  kiche JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tusipoziba ufa tutajenga ukuta!!!siamini kama nchi hii imekosa viongozi wenye hekima,please!serikali chukueni hatua haraka kutokomeza upumbavu huu kwani uwezo mnao ila sina uhakika kama nia mnayo,eleweni kuwa moto ukiwaka hata nyie hampo salama,chonde chonde,mmezoea kudharau mambo lakini hili si la kudharau hata kidogo,hatupendi ya Rwanda kujirudia kwetu,ee Mungu tunaomba utunusuru kwa hali hii.
   
 11. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  anayetaka kukuua hakutumii ujumbe.............
   
 12. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizi ni propaganda za CHADEMA tu ili waonewe huruma........ kwani wameanza kushinda majimbo mwaka huu?? mbona wabunge wao wote wapo hai??? suala la kuuawa kiongozi wa chama, hata CCM aliuliwa mwenyekiti wa wilaya kule mbeya hivi karibuni, je? CHADEMA ndio walimuua?? suala la kuuana arusha halijaanza leo
   
 13. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hi siasa za kuuana zitatupeleka wapi!!!
   
 14. k

  kiche JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  umejitahidi!!!ukiandika jaribu akili yako kuwa sambamba na hilo unaloandika,najitahidi kutumia lugha ya hekima kwani uwezo wako wa kuelewa nina mashaka nao!!!naomba ukumbuke kuwa hata huyo mwenyekiti alilalamika kutishiwa maisha watu wakawa kimya matokeo yake yakaonekana,mwakyembe naye alitoa maelezo mkamwona msanii kilichotokea ni kama tamthilia,mifano ni mingi tu kuhusiana na hali hii,usalama wa wabunge wa upinzani na viongozi wao ni mdogo rejea shambulio la wabunge wa chadema mwanza!!!ruhusu akili yako kufanya kazi kabla ya kuandika vinginevyo baki ukiwa unasoma thread za wengine.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,446
  Likes Received: 19,815
  Trophy Points: 280
  cm kwa nini wanaiharibu nchi?
   
 16. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  wewe wasema..........
   
 17. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  VODA hawako serious,unaweza kutumia chip yao bila ya kusajili kwa mwezi mzima ndo wana block.Hata hivyo kama mtu ana intention hiyo atanunua Simu mpya na laini mpya anazitumia na kuzitupa, akinunua chip na kubaki na simu ni rahisi sana kumkamata.Ni nchi zilizoendelea ndo zinaweza ku trace hata nani aliandika pale hata simu inapotupwa.Kwa Tanzania tusahau.

  Pia hata kwenye kusajili kwenyewe,sehemu wanazosajili haziko serious,ni rahisi mtu ku present details za uongo.
   
 18. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hatuna jeshi huru la polisi Tanzania polisi nao wanatumiwa tu na magamba kisiasa nawaomba viongozi wa cdm Taifa kukaa chini nakupanga watawalinda vipi viongozi hawa pamoja na wengine coz inaonekana huu ni mkakati wa Nchi nzima tunakumbuka yaliyomtokea Kiwia na yule mbunge wa Ukerewe kule Mwanza...afu pia individual hawa waliotishiwa wachukue tahadhari pamoja na viongozi wengine kubwa kuliko yote tuwaombee kwa mwenyezi Mungu kila siku katika sala zetu awalinde nakuwakinga usiku na mchana.
   
 19. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi ni vigezo gani vinamfanya mtu ajiunge na jeshi la polisi?
   
 20. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  sio lazima. nimewahi kununua laini ya simu tena kwenye ofisi za customer
  care na nikaambiwa niisajili kwa simu ndani ya wiki mbili kupitia namba 106 kama sikosei. sasa kama ningekuwa na nia mbaya nini kingenizuia kutuma msg za aina hiyo ndani ya wiki mbili na kutupa lain?
   
Loading...