Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo

Wajumbe,
Huku tukiendelea kusikitika na baraza lisilo na uwakilishi wa watanzania, huenda tukapata misiba mingine very soon!

SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri Mbwambo (36), kuuawa kwa kuchinjwa Aprili 27 mwaka huu, Mbunge wa Jimbo hilo, Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wamedai kupokea ujumbe wa maneno kwenye simu ya kiganjani unaowatishia kuwaua.

Akizungumza mjini hapa, Nassari alisema amepata ujumbe wa kumtishia kumuua na viongozi wa matawi wa jimbo la Arumeru Mashariki ambao walikuwa mstari wa mbele kumpigania kupata ushindi kwenye kampeni.

Alisema ujumbe huo aliupata kupitia simu yenye namba 0753-211 367, ambapo namba hiyo ilituma ujumbe wa kuwatishia kuwachinja, kwa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Gadiel Mwanda, Katibu wa Wilaya hiyo, Totinan
Ndonde.

Mwenyekiti wa Kata ya Seela Sing’isi, Simba Kimunto na aliyekuwa Mkuu wa operesheni ya ushindi wake, John Mrema.

Nassari alisoma ujumbe huo kuwa ni, “Tumekuona unabeba jeneza kwenye gazeti, tunakuhakikishia utabeba majeneza Arumeru Mashariki, mpaka ukimbie Ubunge na baada
ya Mwenyekiti Usa (Msafiri Mbwambo) kumchinja, sasa ni Simba Kimunto muda usiojulikana, utabeba jeneza lake, Jimbo hili tutalichakaza ndani ya miezi sita, nakutakia mazishi mema ya mfululizo.”

Alisema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo akiwa anausoma ukaingia ujumbe mwingine kwa namba hiyo hiyo ukisema, “Bado wewe na Wenyeviti Chadema kwenye kata zako,”
Nassari alisema kuwa mtu huyo asiyejulikana alituma ujumbe kwa Godbless Lema usemao, “Wewe ng’ombe kama Kimunto alikuwekea Wameru 300 kukulinda Arumeru, sasa wewe utamwekea Wachaga wangapi?

Kwa sababu baada ya m/kiti Usa River tunamchinja yeye.” Alisema Lema naye akiwa
anatafakari ujumbe huo uliingia mwingine ukisema,” Baada ya Mwenyekiti wako wa Usa atafuata Mwenyekiti wa kata ya Seela-Sing’isi Samba Kimunto huyu amekuwa kero wilaya hii ya Arumeru Wenyeviti wa Jimbo hili tutakabiliana nao mwezi huu mtamzika sambamba Kimunto unalo la kusema.”

Aidha alisema kuwa baada ya kupata ujumbe huo alifanya mawasiliano na Katibu wa chama chake wa wilaya hiyo, Totinan Ndonde, ambaye alikwenda kituo cha Polisi cha wilaya hiyo, kutoa taarifa na alipewa RB yenye namba USR/RB/1671/2012.

Naye Katibu wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde alipopigiwa simu kuulizwa kuhusiana na hilo, alikiri kupokea ujumbe huo wa vitisho vya kuuliwa na wenyeviti wake wa kata na akatoa taarifa Polisi kwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo, John Marona kupewa RB namba USR/RB/1671/2012.

Sosi: HabariLeo | Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo

Namba hiyo ya simu ukipiga haipatikani.
Naomba turejee kwenye uchaguzi mkuu 2010, simu za vitisho zilikuwepo lakini sikusikia kampuni za VODA, TIGO, AIRTEL zikitoa majina ya wale waliokuwa wanatumia mitandao hiyo kutishia amani. Lakini pia mamlaka ya mawasiliano haikufanya juhudi zozote kuwezesha kukamatwa kwa magenge hayo ya kihalifu.
Jeshi la polisi nalo ndio hilo pangu pakavu hawana uwezo wa kufanya uchunguzi pamoja na kuwa na uwezo wa KIINTELIJENSIA Chadema wakitaka kufanya mikutano yao ya Amani.
Ombi lanu kwenu wanaJF tushirikiane kwa kadri tuwezavyo kuwatia moyo wa ujasiri viongozi wanaotishiwa maisha yao ili waendelee na kazi zao za kuongoza wananchi na MUNGU atakuwa upande wao.

Kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba Waziri wa Mawasiliano bado yupo kazini mpaka sasa.
TCRA ambayo ipo chini ya wizara ya mawasiliano ilitoa agizo watumiaji wa mitandao ya simu kusajili namba zao za simu, lakini cha kushangaza ni kwamba kuna namba za simu bado hazijasajiliwa na zinatumika.

SHAME ON YOU MBARAWA!
SHAME ON YOU TCRA!
SHAME ON YOU KIKWETE!
 
Wajumbe,
Huku tukiendelea kusikitika na baraza lisilo na uwakilishi wa watanzania, huenda tukapata misiba mingine very soon!

SIKU chache baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, Jimbo la Arumeru Mashariki, Msafiri Mbwambo (36), kuuawa kwa kuchinjwa Aprili 27 mwaka huu, Mbunge wa Jimbo hilo, Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wamedai kupokea ujumbe wa maneno kwenye simu ya kiganjani unaowatishia kuwaua.

Akizungumza mjini hapa, Nassari alisema amepata ujumbe wa kumtishia kumuua na viongozi wa matawi wa jimbo la Arumeru Mashariki ambao walikuwa mstari wa mbele kumpigania kupata ushindi kwenye kampeni.

Alisema ujumbe huo aliupata kupitia simu yenye namba 0753-211 367, ambapo namba hiyo ilituma ujumbe wa kuwatishia kuwachinja, kwa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mwenyekiti wa Wilaya ya Arumeru, Gadiel Mwanda, Katibu wa Wilaya hiyo, Totinan
Ndonde.

Mwenyekiti wa Kata ya Seela Sing’isi, Simba Kimunto na aliyekuwa Mkuu wa operesheni ya ushindi wake, John Mrema.

Nassari alisoma ujumbe huo kuwa ni, “Tumekuona unabeba jeneza kwenye gazeti, tunakuhakikishia utabeba majeneza Arumeru Mashariki, mpaka ukimbie Ubunge na baada
ya Mwenyekiti Usa (Msafiri Mbwambo) kumchinja, sasa ni Simba Kimunto muda usiojulikana, utabeba jeneza lake, Jimbo hili tutalichakaza ndani ya miezi sita, nakutakia mazishi mema ya mfululizo.”

Alisema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo akiwa anausoma ukaingia ujumbe mwingine kwa namba hiyo hiyo ukisema, “Bado wewe na Wenyeviti Chadema kwenye kata zako,”
Nassari alisema kuwa mtu huyo asiyejulikana alituma ujumbe kwa Godbless Lema usemao, “Wewe ng’ombe kama Kimunto alikuwekea Wameru 300 kukulinda Arumeru, sasa wewe utamwekea Wachaga wangapi?

Kwa sababu baada ya m/kiti Usa River tunamchinja yeye.” Alisema Lema naye akiwa
anatafakari ujumbe huo uliingia mwingine ukisema,” Baada ya Mwenyekiti wako wa Usa atafuata Mwenyekiti wa kata ya Seela-Sing’isi Samba Kimunto huyu amekuwa kero wilaya hii ya Arumeru Wenyeviti wa Jimbo hili tutakabiliana nao mwezi huu mtamzika sambamba Kimunto unalo la kusema.”

Aidha alisema kuwa baada ya kupata ujumbe huo alifanya mawasiliano na Katibu wa chama chake wa wilaya hiyo, Totinan Ndonde, ambaye alikwenda kituo cha Polisi cha wilaya hiyo, kutoa taarifa na alipewa RB yenye namba USR/RB/1671/2012.

Naye Katibu wa Wilaya ya Arumeru, Totinan Ndonde alipopigiwa simu kuulizwa kuhusiana na hilo, alikiri kupokea ujumbe huo wa vitisho vya kuuliwa na wenyeviti wake wa kata na akatoa taarifa Polisi kwa Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo, John Marona kupewa RB namba USR/RB/1671/2012.

Sosi: HabariLeo | Nassari, Lema wadai kutishiwa kifo

Aliuetuma ujumbe ameshalaanika mbele ya Mungu na M4C. Wala asiogopwe. Imani huleta matumaini na uoga huleta kukata tamaa. Hakuna kuogopa.
 
Kinachoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba Waziri wa Mawasiliano bado yupo kazini mpaka sasa.
TCRA ambayo ipo chini ya wizara ya mawasiliano ilitoa agizo watumiaji wa mitandao ya simu kusajili namba zao za simu, lakini cha kushangaza ni kwamba kuna namba za simu bado hazijasajiliwa na zinatumika.

SHAME ON YOU MBARAWA!
SHAME ON YOU TCRA!
SHAME ON YOU KIKWETE!
Mimi kinachoniuma zaidi January Makamba kapelekwa kulekule.
 
CCM ni hatari sana yani baada ya CHADEMA kuanzisha M4C na wenyewe CCM wameamua kuanzisha nao M4K ( movemebt 4 killing) yao duuuuuu!. Alafu pia hili gazeti la habari leo ni la ccm na wameamua kulitumia mahususi kuandika hii habari ili kwamba kuwatisha wale wote wanaonekana na mapenzi na CDM pia ni mbinu inayotumika kwa ustadi mkubwa na hili gazeti la CCM kuwaogopesha watu wasijiunge na CHADEMa na badala yake waendelee kuwa chini ya CCM ili kuokoa maisha yao.
CHADEMA SHTUKENI JUU YA HUU MCHEZO MCHAFU WA CCM NA MAGAZETI YAKE.
 
...mimi nadhani polisi wangeaza kwa kumhoji msajili wa vyama vya siasa bwana Tendwa kwani huyo ndo mtu wa kwanza kukutana na hao watoa vitisho...nakumbuka kabla ya kampeni za uchaguzi wa Arumeru,Tendwa alisema Lema asiende Arumeru atauwa,ikiuchunguzwa kwa makini kauli hiyo ya Tendwa naamini itagundulika chanzo cha mauji ya mwenyekiti wa Chadema na hivi vitisho vilivyo tolewa sasa...kama hao walio mwambia Tendwa kwamba watamua Lema,kwa nini washidwe kushidwe kumua mwenye kiti wa Chadema?,kama wamefanikiwa kumuua mwenyekiti wa CDM,ni kwa nini sasa wasiendelee na mipango yao ya waali ya kumuua Lema?...
 
umejitahidi!!!ukiandika jaribu akili yako kuwa sambamba na hilo unaloandika,najitahidi kutumia lugha ya hekima kwani uwezo wako wa kuelewa nina mashaka nao!!!naomba ukumbuke kuwa hata huyo mwenyekiti alilalamika kutishiwa maisha watu wakawa kimya matokeo yake yakaonekana,mwakyembe naye alitoa maelezo mkamwona msanii kilichotokea ni kama tamthilia,mifano ni mingi tu kuhusiana na hali hii,usalama wa wabunge wa upinzani na viongozi wao ni mdogo rejea shambulio la wabunge wa chadema mwanza!!!ruhusu akili yako kufanya kazi kabla ya kuandika vinginevyo baki ukiwa unasoma thread za wengine.

Umemjibu vizuri, naamani akitumia ushauri wako hatarudia kosa alilofanya. Asante sana!
 
Hizi ni propaganda za CHADEMA tu ili waonewe huruma........ kwani wameanza kushinda majimbo mwaka huu?? mbona wabunge wao wote wapo hai??? suala la kuuawa kiongozi wa chama, hata CCM aliuliwa mwenyekiti wa wilaya kule mbeya hivi karibuni, je? CHADEMA ndio walimuua?? suala la kuuana arusha halijaanza leo

brain concussion
 
Ah! .....
Wanachadema watapoanzaa kujibu na kuanza kuwachinja wana CCM........
Hapo ndipo kina Saida Mwema IGP, Jack Zoka UWT wataanza kuongea kwa ukali na kusema CHADEMA inastahili kufutwa ..
ikiwa pamoja na kuwafungulia kesi za mauaji kina Dr Slaa, Mbowe,na viongozi wengine wa CDM.

..Sasa CDM itabidi waanzishe Umkotho wa Sizwe ili waweze kujilinda....lasivyo watamalizwa na genge hili la majambazi wa
CCM.
....

Mkuu, hicho kitu kinaitwa Umkhonto we Sizwe aka Spear of the Nation.
Nadhani kama mambo yakizidi kuwa mabaya, huko ndiko tunakoelekea naona.
Vyombo vya usalama viwe makini sana na hali inavyopelekwa, vinginevyo damu zisizo na hatia kila siku tutazipoteza.

Oliver Tambo alikuwa exile kwa miaka 30, lakini mwisho wa siku Uhuru ulipatikana, right kuanzia jela ambako Mandela alikuwa.
Our version; Slaa, Lissu, Mbowe, Kabwe, Mnyika, Nyerere, Mdee, Nassari, Natse, and company.
tunawategemea, na nguvu ya umma siku zote inashinda. tusisahau kuanza na Mungu kama kawaida, na kumaliza na Mungu pia.
 
kama polisi na usalama wa taifa wameoza kiasi hicho hata kutress namba wanashindwa si tuazime hata FBI kumi waje watusaidie?
 
shukuru Nimetoka kifungoni,

wadau nipeni update nilikuwa na ban ya mwezi mzima!

Kesi ya ubunge wa arusha iliishia wapi?
 
Hii thread imeletwa na tume ya katiba mmmhhhhh......... Sijui amepatwa na huruma gani Leo ? Anyway lakini natumaini bado Chama changu kipo imara
 
Wanasiasa waendeshe siasa zisizoacha majeraha nyuma. Kila utakachotendea mwingine nawe utatendewa hivyohivyo. huwezi kutenda unyama ukafikiri utaishi kwa amani. Hata kama kusingekuwa na Mungu kungekuwa na shetani na kama kusingekuwa na shetani kungekuwa na mwanadamu ambaye asingekubali lazima angelipa kisasi. Auwaye kwa upanga atakufa kwa upanga.:israel:
 
Hii thread imeletwa na tume ya katiba mmmhhhhh......... Sijui amepatwa na huruma gani Leo ? Anyway lakini natumaini bado Chama changu kipo imara

Kaka mwenyekiti katuboa jana na uteuzi wake,

Sasa na sisi tutamfanyia fitna hii nchi haitatawalika!
 
Uh habari hii kama inaandikwa na gazeti la HABARI LEO, hii ina maana kuwa lina mkono wa ...wamiliki wa gazeti la Habari Leo. Jichungeni jamani nawa jamaa ni hatari!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom