Nassari kufunga Ndoa Jumamosi

Prayuth

Member
May 20, 2014
10
0
Mh. Makinda amesema ametangaza Bungeni kuwa Mh. Nassari atafunga ndoa Jumamosi, ila hakusema atafunga ndoa na nani? Mh. Nassari ni member humu nadhani atatudokezea kidogo.
Hongera saa Mh. Nassari.

====================

Matukio ya sherehe ya sendoff
MATUKIO YA SEND OFF YA MCHUMBA WA MBUNGE JOSHUA NASSARI.KESHO KUFANYA HARUSI YA ALAIKI.Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimvisha pete ,Mchumba wake Anande Nnko akati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.​

Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.​


"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.​

Na ssari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .

Kwa hisani ya Busagaga's Orijino.

 
Mh. Makinda amesema ametangaza Bungeni kuwa Mh. Nassari atafunga ndoa Jumamosi, ila hakusema atafunga ndoa na nani? Mh. Nassari ni member humu nadhani atatudokezea kidogo.
Hongera saa Mh. Nassari.

mkewe ni Halima Mdee, mmesahau kampeni za arumeru
 
Ile tabia yake ya kutembea na majimama kule Tengeru naona sasa ataiacha...cdm viongozi wake wanapenda michepuko sana.
 
Ameamua kumfuta machozi yule mwimba kwaya mrembo vic aliyeingizwa mkenge majuzi!
 
Hivi harusi ya Dr Slaa tayari??

Bado mkuu! Mtoto bado mdogo wanalea kwanza, nadhani mwakani kamanda atafunga ndoa nae na mama yetu Josephine ya kimila au serikali maana mama yetu alishafunga kanisani, haiwezekani arudi kanisani tena.
 
Ahongereke! Vp anafungia kwa Gwajima?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom