Wafunga ndoa baada ya miaka 51 ya uchumba

Wafunga ndoa baada ya miaka 51 ya uchumba

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
226
Reaction score
507
Mzee mwenye umri wa miaka 92, Celestino, pamoja na bibie wa miaka 87, Sevelina, rasmi wamefunga ndoa katika sherehe ya harusi iliyofanyika Kaunti ya Meru, nchini Kenya baada ya miaka 51 ya uchumba wao.

Wawili hao ambao wameishi pamoja kwa zaidi ya miongo mitano bila ndoa, walikutana kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1975 hatimaye wameweka rasmi ahadi yao ya maisha katika sherehe iliyohudhuriwa na wanafamilia na marafiki.

Kisa chao cha kushangaza kimevutia watu wengi na kuwatia moyo mtandaoni, kikiwakumbusha kwamba mapenzi au ndoa hayana kikomo cha umri.
1788160984634.png

1788161007668.png
 
Back
Top Bottom