Nassari aambiwa aache Kucopy na Kupaste

Nassari aambiwa aache Kucopy na Kupaste

je kama alitembelea tu magereza , hawezi kujua?
au mpaka naye afungwe ndio ajue matatzo ya wafungwa?
 
kwani kasema alishafungwa magereza? Labda ulimuelewa vibaya lakini kama kuna ukweli basi atabadilika. Nirahisi kujibadilisha, ukiwa unasoma vitabu tofauti vya zamani vitashepu upongo wako kipekee! °
 
We usirudie siku nyingine kukosoa viongozi wako hadharani sio desturi ya chama chenu! Ikibidi mtu wa kukosolewa hadharani ni Zitto kabwe pekee maana hata ukipatikana na hatia uwezekano wa kupewa karipi ni mkubwa badala ya kufukuzwa!

Anakuingiliaga kinyume na Matarajio? make hapa watu wanazungumzia Ishu ya Nasari wewe unataka kubadili maada na kuleta Porojo zingine, Zito anahusika vipi hapa?
 
hahaha unatetea kisa ni mtu wa chama cha zone yenu sio

Mpaka siku tutakapo ondokana na ufinyu huu wa kufikiri, ndipo tutaweza kupiga hatua vizuri katika kuleta maendeleo ya Taifa. Inamaana wewe umekubaliana na maawazo potofu ya mletta mada? Kwani wewe ni mara yako ya kwanza kusikia matatizo ya magereza yetu? Hata serikali yenyewe huwa inatoa taarifa hizi pia. Tuache ushabiki wa kitoto.
 
Acha uccm kwani tunapoamini kuwa yesu aliteswa kwa ajili yetu tulikuwepo wakati huo?
 
dogo alitakiwa awe mk/mtaa kwanza then 2020 ndo agombee ubunge.hafai kwa sasa bdo mtoto.anaropoka,hana busara za kiongozi ana za kishuleshule bado.alipita kwa kuwa chadema inawika tu bt hamna kitu pale.
 
Kwani kuelezea matatizo yaliyopo gerezani ni kukopi, ama ni lazima ufungwe? Kwani chanzo cha taarifa cha mateso ya gerezani ni Lema tu? Hapa hujaeleweka. Nasari kama mbunge ananafasi ya kufatilia kwa undani matatizo mbalimbali kwenye jamii na kuyashughulikia either pamoja na wananchi, kuweka msukumo kwa wahusika ama kulifikisha Bungeni.

Safi sana umemjibu sana
 
We usirudie siku nyingine kukosoa viongozi wako hadharani sio desturi ya chama chenu! Ikibidi mtu wa kukosolewa hadharani ni Zitto kabwe pekee maana hata ukipatikana na hatia uwezekano wa kupewa karipi ni mkubwa badala ya kufukuzwa!
mleta mada aombee kikao cha kamati tendaji kisifike haraka.
 
Wanajf.
Nimeamua kuja hapa kuweka mambo haya sawa, Kijana wetu na mdogo wetu Nassari alionekanika ni kijana machachari mbele mwa jamii pale anapokuwa jukwaani na sehemu nyinginezo hili halina ubishi kabisa.

Jana na Juzi kulikuwa na mikutano ya CDM Moshi na Mwanza ambayo Dogo janja alihudhuria na kupewa nafasi ya kuhutubia kama mbunge, Naomba niongelee hili la Mwanza maana la Moshi sikuwepo zaidi ya kusikiliza kwenye Redio.

Nassari inabidi uwe wewe kama wewe acha kucopy na kupaste maana unapocopy ni lazima utaje nukuu ya mtu fulani ila wewe unasema kama wewe ndiyo umefanya hicho kitendo wakati siyo wewe, Mfano Unapenda kuongelea ishu ya Magereza wakati hujawahi kwenda, Jana kwenye mkutano wa hapa Mwanza ulizungumzia kuhusu mateso ya wafungwa walivyokuwa wanakueleza jinsi walivyofungwa kwa kusingiziwa wakati siyokweli kwamba wewe ndiyo ulikuwa magereza bali Alikuwa ni Lema! kwanini unashindwa kusema Na Nukuu kutoka kwa Lema? kama ambavyo Lema Anapenda kunukuu Wanaharakati mbalimbali kama steve Biko, Martin Luther nk.. ni Lazima ubadilike utafute mkakati mwingine wa jukwaani wewe ni kiongozi sasa unaongoza jimbo wananchi wako wangependa kukusikia Nassari na siyo Lema.

Najua waweza kwazika ila huwo ndiyo ukweli kuwa wewe kama wewe Level uliyofikia siyo ya kuwa hivyo, Badilika Tunakupenda ndiyo maana tunakuambia ukweli urudi kwenye mstari maana watu makini hukushusha na kusema umebebwa na upepo.... Natumaini salamu hizi zitakufikia na utazisikia.... jiulize kwanini kamanda Mawazo hakopy na kupaste? Samahani lakini..

Wakati Naandika andiko hili nilitegemea kabisa watu kulipinga kwakuwa hawataki ukweli kuwekwa wazi, Mimi namkubali sana Nassari, Nilichokisema hapa ni jambo la kawaida tu, Anaposema nilipokuwa magereza siku ya kwanza nilikutana na kijana mmoja aliyekuwa amefungwa Morogoro kwa kesi ya kusingiziwa na kisha kuhamishiwa Magereza ya kisongo sasa siku moja alipokuwa anaandikisha majina maana alikuwa nyapara mara akakutana na jina la mtoto na kisha mbele ya hilo jina likawekwa jina lake alipomuambia mfungwa huyo mpya ataje jina la ukoo wake akakuta ni ukoo wake pia... alipoendelea kumuhoji akakuta ni mtoto wake, Jamani hili lipo wazi maneno haya mara nyingi husema lema na hii Lema alihutubia kwenye mkutano wake wa Kwanza alipotoka Jela, Sasa tunapo muambia Nassari akiongea asiache kutaja chanzo kuna ubaya gani?

Tusibishe kila kitu, Tunahitaji kuwekana sawa kwaajili ya siku za mbeleni, Kwani akisimama na kusema, Nakumbuka kaka yangu ama kamanda mwenzangu Lema aliniambia alipokuwa magereza alikutana na kijana mmoja siku ya kwanza then akaendelea kutiririka kuna ubaya gani?
 
Back
Top Bottom