J.K.Rayhope
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 316
- 31
Wanajf.
Nimeamua kuja hapa kuweka mambo haya sawa, Kijana wetu na mdogo wetu Nassari alionekanika ni kijana machachari mbele mwa jamii pale anapokuwa jukwaani na sehemu nyinginezo hili halina ubishi kabisa.
Jana na Juzi kulikuwa na mikutano ya CDM Moshi na Mwanza ambayo Dogo janja alihudhuria na kupewa nafasi ya kuhutubia kama mbunge, Naomba niongelee hili la Mwanza maana la Moshi sikuwepo zaidi ya kusikiliza kwenye Redio.
Nassari inabidi uwe wewe kama wewe acha kucopy na kupaste maana unapocopy ni lazima utaje nukuu ya mtu fulani ila wewe unasema kama wewe ndiyo umefanya hicho kitendo wakati siyo wewe, Mfano Unapenda kuongelea ishu ya Magereza wakati hujawahi kwenda, Jana kwenye mkutano wa hapa Mwanza ulizungumzia kuhusu mateso ya wafungwa walivyokuwa wanakueleza jinsi walivyofungwa kwa kusingiziwa wakati siyokweli kwamba wewe ndiyo ulikuwa magereza bali Alikuwa ni Lema! kwanini unashindwa kusema Na Nukuu kutoka kwa Lema? kama ambavyo Lema Anapenda kunukuu Wanaharakati mbalimbali kama steve Biko, Martin Luther nk.. ni Lazima ubadilike utafute mkakati mwingine wa jukwaani wewe ni kiongozi sasa unaongoza jimbo wananchi wako wangependa kukusikia Nassari na siyo Lema.
Najua waweza kwazika ila huwo ndiyo ukweli kuwa wewe kama wewe Level uliyofikia siyo ya kuwa hivyo, Badilika Tunakupenda ndiyo maana tunakuambia ukweli urudi kwenye mstari maana watu makini hukushusha na kusema umebebwa na upepo.... Natumaini salamu hizi zitakufikia na utazisikia.... jiulize kwanini kamanda Mawazo hakopy na kupaste? Samahani lakini..
Nenda kalale,pitia kwanza ikulu ya nyumba unayoishi,usijepitiwa usingizini uka.....