stineriga
JF-Expert Member
- Jun 20, 2012
- 2,172
- 887
Anagalau nimesoma upande wa pili wa stori,
STORY YA BABU DC HII HAPA JUU YA KISA HIKI
Ndugu wadau wa jukwaa letu tukufu,
Kama mtakumbuka, week iliyopita nilirusha thread iliyokuwa inaripoti kisa cha Nasra Mohamedi wa Bunda aliyegongwa kwa gari na mume wake na kuburuzwa kama mita 100 hivi. Story yenyewe hii hapa:
Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka!
Hivi karibuni, nimepata bahati ya kuongea na mtu ambaye alikuwa maeneo yale ya tukio ingawa hakushuhudia live jinsi tukio livyotokea. Hata hivyo ameweza kunipatia story za ndani kuhusu mkasa wenyewe.
Inasemekana kuwa Nasra na mume wake walikuwa na ndoa nzuri sana. Ilikuwa ni couple ya kupigiwa mfano. Hata hivyo, mume wa Nasra alipitiwa na shetani akatembea nje ya ndoa; na kwa bahati mbaya Nasra alimfumania. Baada ya tukio hilo, ndoa yao haikuwa na amani tena; na Nasra aliamua kutafuta mwanamume wa nje na kutembea naye wazi wazi. Hatimaye walitengana ila Nasra aliendelea kumfuata fuata mume wake kwa kumuonyesa wazi wazi kwamba anatembea na huyo bwana wake mpya. Inasemekana mume wake ni mpole sana na alijitahidi kumpuuza. Hata hivyo vituko vilizidi kiasi kwamba mume alikuwa anafuatwa hata kwenye baa anakoenda. Na mara zote, Nasra alikuwa akifika na huyo bwana mpya. Na kwamba, alifikia mahali pa kukaa meza ambayo iko karibu na mume wake ili amkere. Pia alianza kufanya vituko ili mume wake wa zamani amfumanie, ili naye aumie kama ilivyotokea kwake!
Inasemekana pia kwamba Nasra alifungua kesi mahakamani kuomba talaka na kwamba wagawane mali za ndoa. Taarifa zinasema kwamba, kabla ya kutengana, mume alikuwa amemnunulia Nasra gari. Pia wakati wanatengana, mwanamke aliondoka na pesa za mume kiasi cha shilingi 10mil. Haya yalizidisha uchungu kwa mume ambaye alianza kuwaambia marafiki zake kwamba atamuua huyo mke kisha naye ajiue.
Siku ya tukio, inasemekana Nasra alimkuta mume wake standi ya bus Bunda na kuanza kumtukana matusi machafu sana, tena mbele ya watu wengi waliokuwepo hapo. Baadhi ya mambo aliyomkashifu ni kwamba mume huyo hana nguvu za kiume za kutosha na pia kuwa watoto waliozaa si wake! Inasemekana yule baba aliondoka kwa muda ili kuepuka shari za mke wake. IHata aliporudi tena baada ya muda kidogo, bado Nasra aliendelea kumtukana. Ndipo mwanamume akamuita apite upande wa pili wa gari ili waongee (wakati wote huo, yule baba alikuwa kwenye gari), na hapo hapo mwanamume aliondoa gari na kumburuza hadi karibia na kituo cha polisi. Alipofika hapo, akamtelekeza pomoja na gari na kupotelea kusikojulikana.
Kwa ufupi, huo ndio upande mwingine wa hili tukio ambalo kweli linasikitisha sana,
Babu DC!!