Nasra Mohamed: Ukatili na unyanyasaji uliovuka mipaka!

Ndugu wadau wa jukwaa letu tukufu,

Kama mtakumbuka, week iliyopita nilirusha thread iliyokuwa inaripoti kisa cha Nasra Mohamedi wa Bunda aliyegongwa kwa gari na mume wake na kuburuzwa kama mita 100 hivi. Story yenyewe hii hapa:

https://www.jamiiforums.com/mahusia...d-ukatili-na-unyanyasaji-uliovuka-mipaka.html


Hivi karibuni, nimepata bahati ya kuongea na mtu ambaye alikuwa maeneo yale ya tukio ingawa hakushuhudia live jinsi tukio livyotokea. Hata hivyo ameweza kunipatia story za ndani kuhusu mkasa wenyewe.

Inasemekana kuwa Nasra na mume wake walikuwa na ndoa nzuri sana. Ilikuwa ni couple ya kupigiwa mfano. Hata hivyo, mume wa Nasra alipitiwa na shetani akatembea nje ya ndoa; na kwa bahati mbaya Nasra alimfumania. Baada ya tukio hilo, ndoa yao haikuwa na amani tena; na Nasra aliamua kutafuta mwanamume wa nje na kutembea naye wazi wazi. Hatimaye walitengana ila Nasra aliendelea kumfuata fuata mume wake kwa kumuonyesa wazi wazi kwamba anatembea na huyo bwana wake mpya. Inasemekana mume wake ni mpole sana na alijitahidi kumpuuza. Hata hivyo vituko vilizidi kiasi kwamba mume alikuwa anafuatwa hata kwenye baa anakoenda. Na mara zote, Nasra alikuwa akifika na huyo bwana mpya. Na kwamba, alifikia mahali pa kukaa meza ambayo iko karibu na mume wake ili amkere. Pia alianza kufanya vituko ili mume wake wa zamani amfumanie, ili naye aumie kama ilivyotokea kwake!

Inasemekana pia kwamba Nasra alifungua kesi mahakamani kuomba talaka na kwamba wagawane mali za ndoa. Taarifa zinasema kwamba, kabla ya kutengana, mume alikuwa amemnunulia Nasra gari. Pia wakati wanatengana, mwanamke aliondoka na pesa za mume kiasi cha shilingi 10mil. Haya yalizidisha uchungu kwa mume ambaye alianza kuwaambia marafiki zake kwamba atamuua huyo mke kisha naye ajiue.

Siku ya tukio, inasemekana Nasra alimkuta mume wake standi ya bus Bunda na kuanza kumtukana matusi machafu sana, tena mbele ya watu wengi waliokuwepo hapo. Baadhi ya mambo aliyomkashifu ni kwamba mume huyo hana nguvu za kiume za kutosha na pia kuwa watoto waliozaa si wake! Inasemekana yule baba aliondoka kwa muda ili kuepuka shari za mke wake. IHata aliporudi tena baada ya muda kidogo, bado Nasra aliendelea kumtukana. Ndipo mwanamume akamuita apite upande wa pili wa gari ili waongee (wakati wote huo, yule baba alikuwa kwenye gari), na hapo hapo mwanamume aliondoa gari na kumburuza hadi karibia na kituo cha polisi. Alipofika hapo, akamtelekeza pomoja na gari na kupotelea kusikojulikana.

Kwa ufupi, huo ndio upande mwingine wa hili tukio ambalo kweli linasikitisha sana,


Babu DC!!
 
If that is the case, basi ni ulimbukeni. Kwenye haya mahusiano, kuna lipi jipya la kuanza kurap barabarani sababu umepata mpenzi mpya? Mpenzi mpya naye anakuja na matatizo pengine yale yale au mapya.!
 
Too hard to judge. Kama ni kweli basi huyo Nasra alijtakia matatizo mwenyewe. Ndo nini kumdhalilisha na kumfedhehesa ex wako hvyo? Inauma sana yani kukashfiwa na kutukanwa hvyo.
 
She deserved that


Binafsi nashindwa kusema lolote kwa sababu picha za Nasra na jinsi alivyojeruhiwa...ameponea kwenye tundu la sindano...zinatia huruma sana!!

Hata hivyo, visa vyake navyo...mhhhh...unatakiwa kuwa na roho ya kinabii kuvivumilia.

Ila njia ya kumuua mwenzio kama ndiyo suluhisho la matatizo haifai hata kidogo!!

Babu DC!!
 
Binafsi nashindwa kusema lolote kwa sababu picha za Nasra na jinsi alivyojeruhiwa...ameponea kwenye tundu la sindano...zinatia huruma sana!!

Hata hivyo, visa vyake navyo...mhhhh...unatakiwa kuwa na roho ya kinabii kuvivumilia.

Ila njia ya kumuua mwenzio kama ndiyo suluhisho la matatizo haifai hata kidogo!!

Babu DC!!

Kuua si uungwana hata kidogo...ila tunatofautiana kwenye reasoning. Maana wengine wanakesha kusikiliza taarabu na wanaishi wakiimba nyimbo za taarabu. Hapo chacha..
 
kwa sababu yoyote ile iwayo huyo mume hakuwa na haki ya kumfanyia hayo mke, huo ni ukatili, angeweza hata kumuacha kwa talaka 3 na akawa huru, huo ni ufinyu wa mawazo
 
Maamuzi ya Kuua hayapaswi kufanywa na binaadamu yeyote yule hata mwenzio awe amekukosea vipi. Huyo bwana alikosea tu hamna kitu kitakachomsafisha kwa kitendo alichofanya.

Kweli ndugu,

Kinachosikitisha ni kwamba aliweza kumpuuza mke wake kwa muda mrefu na hata wakati anatukanwa, huyo baba aliondoka kwanza. Kwa nini alirudi?

Na kwa vile alikuwa karibu na kituo cha polisi na inasemekana ni mtu mwenye pesa pale mjini (indicating kwamba atakuwa na heshima yake mtaani), kwa nini hakuripoti kituoni wakamsweka ndani huyo mama?

Babu DC!!
 
Matatizo mengine ni ya kujitakia kweli, hizo nguvu pungufu aliziona baada ya talaka! haya oeni na kuolewa.
 
Maamuzi ya Kuua hayapaswi kufanywa na binaadamu yeyote yule hata mwenzio awe amekukosea vipi. Huyo bwana alikosea tu hamna kitu kitakachomsafisha kwa kitendo alichofanya.

alistahili Ninyi si mlikuwa mnaunga mkono polisi kuua waandamanaji kwenye ule mdahalo ITV???
 
Aisee!

Kama hii stori ni ya kweli, ingekuwa mimi Nasra angeshakwenda kuzimu siku nyingi sana!

Huyu jamaa alikuwa mvumilivu sana bana!
 
Wanawake mara nyingi ukiwamwaga wao matusi yao kwamba hauwezi kazi joka la kibisa huna nguvu oh mara dushelele kama sigara kali,hv miaka yote hyo alikua haoni??
 
Binafsi nashindwa kusema lolote kwa sababu picha za Nasra na jinsi alivyojeruhiwa...ameponea kwenye tundu la sindano...zinatia huruma sana!!

Hata hivyo, visa vyake navyo...mhhhh...unatakiwa kuwa na roho ya kinabii kuvivumilia.

Ila njia ya kumuua mwenzio kama ndiyo suluhisho la matatizo haifai hata kidogo!!

Babu DC!!

tatzo le2 akna dada 2kiona m2 mkimya 2nataka mpanda kichwan afu hakuna k2 knauma km u r quiet stil then sm1 is putn the finger on yo eye, ndo mana jamaa kafkia uamuz huo n cnc nasra kanususurika heshma itakuepo chacha
 
Huyo Nasra ni Jini! Anastahili yalompata! Kwani bwana alipokosea na kutembea nje,yeye Nasra hajawahi kweli? Na ana utakatifu gani wa kulipa kisasi kwa kufanya uzinzi waziwazi na mume ilishamwomba msamaha? Na amedhihirisha wazi kuwa ni mzinzi pale alipotamka kuwa watoto si wa mumewe! Bora angekufa kabisaa!
 
Aisee!

Kama hii stori ni ya kweli, ingekuwa mimi Nasra angeshakwenda kuzimu siku nyingi sana!

Huyu jamaa alikuwa mvumilivu sana bana!


Kwa nini umuue?

Mie ningempeleka jela akajifunze matusi zaidi....

Babu DC!!
 
Mie siku zote huwa naamini mwanamke aliyeko kwenye ndoa anajiheshimu, anamuheshimu mumewe, anawaheshimu ndugu wa mume na wake pia, ukikuta mwanamke kabadilika mara nyingi chanzo ni mume wake, wanaume wanachangia kwa asilimia nyingi kubadilisha tabia za wake zao,


matatizo yanapotokea ndani ya ndoa sio wote wanaweza kuyamaliza kwa njia za busara babu DC, angalia mf. wa Nasra, kamfumania mumewe na njia pekee aliyoona itamwondolea machungu yake ni kulipa kisasi kwa kuwa na mwanaume mwingine, simlaumu manake hapo ndipo akili na maarifa yake yalipoishia. Mwingine labda angeamua kulewa wakati hapo kabla hakuwahi kutumia kilevi chochote, mwingine labda wangekaa wayazungumze then wasameheane na maisha yasonge... Hapa pia inabidi kumpata mume wa Nasra na kumuuliza ni kwanini aliamua kutoka nje ya ndoa yake... Usishangae pia akikwambia chanzo ni mke wake..

Babu DC ndoa zina siri nyingi usione milango na madirisha ukafikiri kuna amani sana!


Nasra alimkosea heshima mumewe, ila pia hakustahili kufanyiwa ukatili wa namna ile...ndoa ni ngumu babu DC, mie hata nashindwa nimtete yupi...
 
Hata ningelikuwa mimi hiyo ndo ilikuwa size yake unajua wanawake wanakera sana na maneno yao wanayoyacopy kwenye taarabu
 
Kuna thread jana nilichangia hapa kuhusu kwa nini wanawake wengine bila kichapo hawaoni kama wanapendwa.Kuna wanawake wengine ni wa ajabu sana,na huyu ni mmoja wapo.Kwa sisi binadamu uvumilivu una mwisho na unaweza kufanya vitu vya ajabu kweli usipoangalia.
Usije ukasikia mwanaume mwenzio ameua kwa sababu ya mapenzi ukashangaa.Nasra hakuwa na sababu ya kufanya hayo aliyokuwa anayafanya.Na sisi wanaume wengine akili zetu tumeshikiwa kweli,kama ni mtu na busara huwezi kutumika eti kumligishia mwanaume mwenzako kiasi hicho.
Sipalilii yaliyofanywa na huyu bwana lakini na yeye ni binadamu afterall.
 
Back
Top Bottom