Nasita kuhamia nyumbani kwa wakwe

Uza hiyo nyumba jenga nyingine

Usawa huu wa Magufuli hata usijiulize mara mbili, hamia fasta.

Kitu cha muhimu hakikisha saving za pango unazitumia kujenga nyumba yako, tena iwe mtaa wa mbali na hapo mtakapokuwa mnaishi, nyumba yako/yenu ikiisha hama hapo na wekeni mpangaji mwendelee kula kodi.

Hakikisha ndani ya miaka 2 ua 3 umemaliza na kuhamia kwenye nyumba yako/yenu.
 
Kama nyumba ipo na umepewa kwa nia nzuri kwanini usihamie huku ukiharakisha kujenga yako?
Ukiendelea kupanga wakati nyumba ipo hawataona sawa.
We nenda kakae huko huku unajenga kwako. Wakianza maneno ondoka urudi kupanga.
 
Nimeoa hivi karibuni na wakwe wametukabidhi mjengo kama zawadi. Mwezi mmoja baada ya ndoa ndugu wa mke pamoja na mke mwenyewe wanashauri tuhamie makao mapya tuachane na kupanga. Naona imekuwa ghafla mno na najihisi kama nahamia ukweni vile (wanaume mnaelewa)! Wadau mnasemaje hapa?
kama wakwe hawaishi hapo hamia tu,ila usibweteke jenga nyumba yako haraka sana kabla dharau haijakomaa
 
Mie na mume wangu tulipewa nyumba na Baba yangu lakini mume wangu alikataa nimemuomba mpaka nikalia alisema no siwezi kaa kwenu mimi ni mwanamme na as long as umekubali kuolewa na mimi hata nikikaa nyumba ya chumba kimoja utakaa...
 
Back
Top Bottom