Nasita kuhamia nyumbani kwa wakwe

Nasita kuhamia nyumbani kwa wakwe

Mie na mume wangu tulipewa nyumba na Baba yangu lakini mume wangu alikataa nimemuomba mpaka nikalia alisema no siwezi kaa kwenu mimi ni mwanamme na as long as umekubali kuolewa na mimi hata nikikaa nyumba ya chumba kimoja utakaa...
Gademit, brother man got some "balls"!! 😉
Na hapo ndio mnapata ujasiri/hasira ya kujenga ya kwenu.
 
Usihamie kwenye hiyo nyumba mkuu kama vipi uza jenga au pangisha, endelea kupigana ujenge kwako !
 
Nimeoa hivi karibuni na wakwe wametukabidhi mjengo kama zawadi. Mwezi mmoja baada ya ndoa ndugu wa mke pamoja na mke mwenyewe wanashauri tuhamie makao mapya tuachane na kupanga. Naona imekuwa ghafla mno na najihisi kama nahamia ukweni vile (wanaume mnaelewa)! Wadau mnasemaje hapa?
Usijipe shida mdogo wangu
Fanya hivi hamia kwenye hiyo nyumba lakini uslaze damu hata kidogo changamka tumia kipato ulichokuwa unakitumia kwa kupanga changanya na michongo yako mingine nunua kiwanja na anza ujenzi fasta
Ikikamilika hiyo nyumba hamieni kwenye hiyo nyumba na hiyo mliyopewa pangisha
Mpka hapo mchezo utakuwa umeisha
Fanya hivyo mdogo wangu vinginevyo watakuona kama maskini jeuri na hujiamini
 
Akihamia tu mke ataota mapembe hata wakipata watoto watakuja gundua mapema hiyo nyumba ni ya zawadi. Ndugu wa mume watapangiwa siku na saa za kuja kusalimia ila ndugu wa mke watageuza makazi hapo.

Wanawake wengine wanajisahau sana hasa kama katokea kwenye familia yenye uwezo
 
Mie na mume wangu tulipewa nyumba na Baba yangu lakini mume wangu alikataa nimemuomba mpaka nikalia alisema no siwezi kaa kwenu mimi ni mwanamme na as long as umekubali kuolewa na mimi hata nikikaa nyumba ya chumba kimoja utakaa...
Huyo ndio mwanaume, huwezi kuweka kambi kwa nyumba ya zawadi ya wakwe hata siku moja.
 
Mmeona ! Mmeona! Mumewooonaaa!
Wote hawa wanakiri na kukubali kuwa cha ukweni cha Mke ni chake chao! Ila cha Mume ni chako chako chetu!

Pili wote hawa wanakiri na kukubaliana na dhana ya mali na ukuu wa kaya! Ati kisa unakaa kwenye hifadhi ya Mke au Ukweni mwanamume au mume hawezi timiliza majukumu yake ya kichwa cha nyumba!

Ama sivyo utafurumishwa kama mbwa koko mkia ameufyatua kwa ndani!

Unaona mawazo hayo ya umaamume ishi, weka akiba, jenga haraka haraka, uwe plan B mambo yakibumburuka!

Hivi mwanaume bila kumiliki nyumba au kuwa na kipato kikubwa kuliko mke huwezi kuwa kichwa cha nyumba? Ndiyo utakuwa baba mwanaume Suruali?

Vilevile, kumbe hii ya wanawake au wake kutokuwa kichwa cha nyumba kumbe ni kutokuwa na mali au nyumba ndani ya familia? Na siyo MFUMO?
 
Jipe muda wa kuishi humo labda miaka 3 wakat huo mnajenga ya kwenu maana usawa huu kulipa kodi huku unajenga ni kazi kubwa sn

Kufedheheka kwa miaka 2 au 3 wakati unajenga kwako sio kitu kibaya sn
 
Mie ni mwanamke lakini siwezi kukaa kwa wakwe sasa wewe mwanaume hata usijaribu hata siku moja
 
Kwa hawa wanawake wa leo,huo ni mtihani mkubwa,kakae kwa malengo,ndani ya miaka 2/3 ujenge yenu...
 
Hivi una akili kweli?umepewa zawadi na wakwe bhado unaleta utoto.
 
Mkuu kuna msemo mmoja wa watu wa kabila la Kimanda huwa wanasema, Mkonu ku donu Macho ku mchuzi. Hamia tu mkuu ila mguu moja hakikisha uko nje, na pia onesha kujiamini since day one, meanwhile hiyo kodi ya pango hifadhi kwa matumizi mengine.
 
Na kwali hii ni dhahiri kabisa wanawake wataendelea kuwa daraja la pili sababu wanaume hawateweza kujiamini ndani ya nyumba zao na kutekeleza wajibu wao kama wababa wa nyumba na ndoa zao pasipo na mali.

Hivyo ukiona kuna jamii ambayo wanawake wengi wamewazidi vipato wanaume zao au wanamali nyingi kuliko wanaume zao ni dhahiri kwenye jamii hiyo kutakuwa na janga kubwa sana la utekelezaji wa majukumu ya kibaba na hii ndiyo inayopelekea kuibuka kwa kasi kwa tabaka la single mothers.
 
Nimeoa hivi karibuni na wakwe wametukabidhi mjengo kama zawadi. Mwezi mmoja baada ya ndoa ndugu wa mke pamoja na mke mwenyewe wanashauri tuhamie makao mapya tuachane na kupanga. Naona imekuwa ghafla mno na najihisi kama nahamia ukweni vile (wanaume mnaelewa)! Wadau mnasemaje hapa?
Umepewa hati? Kuonyesha umiliki wenu wewe na mkeo?
Au maneno tu kwenye sherehe? Huku mkeo ndio kapewa au bado mali ya baba mkwe?
 
Back
Top Bottom