Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 770
- 2,408
Tunaweza tusikichukulie kwa jicho la tatu ila kitendo kilichofanywa na yanga ni cha kishujaa na manufaa makubwa ya soka letu. Kama hii mechi ingechezwa leo saa 1 usiku basi tayari ndio ingekuwa michezo ya TFF kila siku kucheza na ratiba kwa sababu wangejua kumbe hakuna kitu chochote kinachoharibika.
Ingefikia kipindi ratiba za mechi zingekuwa zinabadilishwa kiholela tu bila sababu za msingi. Mfano, ungekuta siku nyingine mechi ya timu A na timu B inaahirishwa/inasogezwa masaa mbele kwa sababu tu uwanja haujajaa kwa muda huo...au ungekuta siku nyingine watu na timu zipo uwanjani halafu mechi inasogezwa muda mbele ili kupisha tu hotuba au kikao cha watu fulani au labda mechi zingekuwa zinaahirishwa kwa sababu tu kuna dalili mvua itanyesha.
Kiufupi, ingefikia stage mechi zingekuwa zinasogezwa mbele kwa sababu zisizo na mashiko. Lakini leo Yanga wameonesha kuwa uswahili hautakiwi na hawajataka kabisa kulea tabia hii.
Ningewakosoa Yanga endapo tu sababu za kusogeza mechi mbele zingekuwa na mashiko lakini mpaka sasa sababu hazijawekwa wazi. Endapo kama sababu zingekuwa zimewekwa wazi na zina mashiko, hakuna mtu au timu ambayo ingekataa kucheza saa 1. Kutokuwekwa wazi kwa sababu za kusogeza mechi mbele inatufanya sisi tuamini kuwa sababu hazikuwa na mashiko ndio maana zimefichwa...ASANTENI YANGA.